Ijumaa, 26 Agosti 2016

Mbunge Lema Akamatwa na Polisi Arusha

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA)

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA)  amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake alfajiri  ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.

Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

Waliokamatwa na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema mkoa (Bavicha), Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP) Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo leo Ijumaa.

Jumatatu, 15 Agosti 2016

DOWNLOAD Ngoma Mpya Ya YOUNGKILLER -Mtafutaji Mp3

Msanii kutoka Rockcity Mwanza Anaejulikana kwa jina la YOUNGKILLER MSODOKI ameachia Ngoma Mpya inayokwenda kwa jina la MTAFUTAJI audio imefanywa na Mr.T touches

DOWNLOAD HAPA 

Jumanne, 2 Agosti 2016

Meneja wa Diamond 'Babutale' Amekamatwa na Polisi

HABARI

Meneja wa Diamond akamatwa tena

Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’

By James Magai na Hadija Jumanne, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.

ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT

Dar es Salaam. Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Mwanafunzi Wa UDOM Auwawa Akitokea Bar

HABARI

Mwanafunzi wa Udom auawa akitokea baa

By mwananchipapers@mwananchi.co.tz Rachel Chibwete, Mwananchi

IN SUMMARY

Tukio hilo limetokea jana usiku eneo la Chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akigalagala njiani.

ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT

Dodoma. Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Fredrick Joseph (25), ameuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akitoka baa.

Tukio hilo limetokea jana usiku eneo la Chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akigalagala njiani.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa, amesema mwanafunzi huyo ambaye ametokea Musoma mkoani Mara ameshambuliwa kwa kupigwa na watu wasiofahamika