Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kitaifa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kitaifa. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 26 Agosti 2016

Mbunge Lema Akamatwa na Polisi Arusha

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA)

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA)  amekamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake alfajiri  ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo.

Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

Waliokamatwa na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema mkoa (Bavicha), Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP) Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo leo Ijumaa.

Jumamosi, 25 Juni 2016

Prof. Mkilaha wa UDSM amefariki dunia kwa kujipiga risasi

Profesa Mkilaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

By Herieth Makwetta, Mwananchi hmakweta@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema polisi wanaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha tukio hilo.

Dar es Salaam. Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idd Mkilaha, inadaiwa amefariki dunia jioni hii nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam baada ya kujipiga risasi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema polisi wanaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha tukio hilo.

“Ni kweli tukio hilo limetokea, amekufa kwa kujipiga risasi, lakini tunachunguza kubaini kama ilikuwa ni bahati mbaya au alidhamiria kufanya hivyo,” amesema Sirro.

Hata hivyo, amesema taarifa zaidi atazitoa kesho.

Profesa Mkilaha alikuwa pia Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Jumanne, 21 Juni 2016

Askari Aliyetukanwa na Mke wa Waziri Bado Hajapandishwa Cheo

   Koplo Deogratius Mbango.

Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI

Dar es Salaam: Mapya yameibuka kumhusu askari wa usalama barabarani (trafiki), Koplo Deogratius Mbango wa Kituo cha Oysterbay ambaye wiki chache zilizopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliagiza apandishwe cheo kutokana na kufurahishwa na utendaji kazi wake ambapo habari mpya ni kwamba, hadi juzi (Jumapili), bado hakuwa amepandishwa cheo kama rais alivyoagiza.

Trafiki huyo, alipata umaarufu mkubwa baada ya kumdhibiti dereva wa mke wa waziri mmoja (jina kapuni) aliyevunja sheria za usalama barabarani kwa kusimama kwenye alama za pundamilia (zebra) ambazo kimsingi hutumiwa na watembea kwa miguu wanaovuka barabara.

Akiwa anatekeleza majukumu yake, Aprili 24, mwaka huu, inadaiwa kuwa mke wa waziri aliyekuwa amebebwa ndani ya gari hilo, amlijia juu Koplo Deogratius huku akimtolea vitisho kwa kutumia cheo cha mumewe, lakini askari huyo hakutetereka zaidi ya kuendelea kusimamia sheria na kuwataarifu wakubwa wake wa kazi, akiwemo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni (RTO) Awadh Haji.

Katika uchunguzi wake wa chini kwa chini, Uwazi limebaini kuwa bado askari huyo anaendelea kukitumikia cheo chake cha zamani, jambo ambalo ni kinyume na maagizo aliyoyatoa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Ili kujiridhisha zaidi, Uwazi liliwahoji baadhi ya watu wa karibu wa askari huyo ambao kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini kwani siyo wasemaji, walisema Koplo Deogratius hajapandishwa cheo kama Rais Magufuli alivyoagiza kwani kama ingekuwa hivyo, angekuwa anaonekana.

Uwazi halikuishia hapo, lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga na kumuulizia sababu zilizokwamisha afande huyo kupandishwa cheo mpaka sasa ambapo alisema:

“Aaah ni kweli ndugu mwandishi hilo agizo lilitolewa na rais lakini hata mimi sijui kwa nini hajapandiswa cheo mpaka leo. Unajua suala la upandishwaji wa vyeo vya kipolisi hata hawa wa usalama barabarani walio chini yangu, huwa sihusiki bali  anayewapandisha ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. Muulize mwenyewe au mtafute msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimbo wao ndiyo watakaoweza kukupa majibu ya uhakika.”

Gazeti lilianza kumtafuta Advera kwa njia ya simu ambapo simu yake haikuwa hewani kila alipopigiwa. Baada ya kumkosa, Uwazi lilimtafuta, IGP Mangu kwa njia ya simu lakini naye simu yake haikuwa hewani kila alipopigiwa.

Ijumaa, 17 Juni 2016

Askofu Gwajima Anatafutwa na Polisi 'usiku na mchana'

Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima.

By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.

Kamanda wa Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewataka watu wenye taarifa za mahali aliko, Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, waisaidie polisi kwa kuwa bado wanaendelea kumtafuta.

Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.

Sauti kwenye mkanda huo inasema Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo Rais wa sasa, John Magufuli anayashughulikia.

Juzi, askari wa jeshi hilo, walishinda mbele ya geti la nyumba ya askofu huyo kwa saa saba bila kufunguliwa na kuondoka.

Kamanda Sirro  amesema kuwa “Kama amejificha, tukimbaini alipo tutamkamata na atambue bado tunamtafuta.”

Jumanne, 7 Juni 2016

Mikutano na Maandamano Marufuku Tanzania

ImageMaafisa wa polisi nchini Tanzania

Polisi nchini Tanzania wamepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia Jumanne wiki hii hadi hali ya usalama itakapotulia

Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari walinda usalama hao wamewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.

Taarifa hiyo imesema kuwa polisi hawatasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hilo.

Aidha maafisa hao wamewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa taifa la Tanzania.

Polisi nchini Tanzania imeripoti kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya kisiasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano .

Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.

Jumatano, 1 Juni 2016

Walioanzisha Mgomo UDSM Kukiona

IN SUMMARY

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo taaluma Florens Luoga amesema kuwa hadi  sasa mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinendelea na uchunguzi kubaini nani alihusika na ni kwa namna gani na baada ya hapo hatua za kinidhmu zitafuata.


Dar es Salaam. Wanafunzi walioandaa mgomo wa jana Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya Chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha Menejimenti.


Naibu Makamu Mkuu wa Chuo taaluma Florens Luoga amesema kuwa hadi  sasa mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinendelea na uchunguzi kubaini nani alihusika na ni kwa namna gani na baada ya hapo hatua za kinidhmu zitafuata.


“Taratibu na sheria ndogo za chuo haziruhusua mtu kuandaa mkusanyiko ambao haujaidhinishwa na menejimenti na kimsingi taratibu hizo lazima ziheshimiwe ili kuzifanya kuendelea kuwa imara hivyo tunasubiri ripoti ya walio husika endapo itaonesha  kuwa wanamakosa basi watachukuliwa hatua za kinmidhamu,” amesema Luoga


Jumatano, 11 Mei 2016

Falsafa 20 za DONALD TRUMP

ImageGETTYImageTrump amekuwa na mapendekezo makali hasa kuhusu wahamiaji na ugaidi

Donald Trump anaongoza katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea urais atakayewakilisha chama cha Republican katika uchaguzi mkuu mwaka ujao. Wajua sera zake na mambo anayoyaamini?

1. Waarabu-Wamarekani jimbo la New Jersey walishangilia shambulio la Septemba 11, 2001 liliotekelezwa. Hakuna habari za kuthibitisha haya.

2. Kunafaa kuwa na mfumo wa kufuatilia misikiti Marekani kama njia ya kukabiliana na ugaidi.

3. Marekani inafaa kutumia njia kali za kuhoji washukiwa katika vita dhidi ya Islamic State.

4. Trump amesema akiwa rais anaweza kuwaangamiza Islamic State kwa mabomu na pia kuwazuia kupata mafuta.

5. Kuundwe mfumo rahisi wa ulipaji ushuru, watu wanaolipwa chini ya $25,000 (£16,524) wasiwe wakilipa ushuru wa mapato.

6. Watu wenye hazina za uwekezaji ng’ambo hawalipi ushuru wa kutosha. Lakini baadaye alibadilika na kusema watapunguziwa ushuru sawa na watu wa pato la wastani.

7. Anataka kujenga ukuta mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji kutoka Mexico.

8. Anataka kuwafurusha wahamiaji wote 11 milioni ambao waliingia Marekani kwa njia haramu.

9. Yeye na Vladmir Putin wanaweza “kusikizana vyema”.

10. Ili kuzuia visa vya watu kupigwa risasi Marekani, nchi hiyo inafaa kuwekeza katika afya ya akili.

11. Uchina inafaa kuchukuliwa hatua kali katika masuala kadha ili kuhakikisha usawa wa kibiashara kati yake na Marekani.

ImageAFPImageTrump amekuwa akisema haja yake kuu ni kurejesha hadhi ya Marekani

12. Kundi la The Black Lives Matter ambalo hutetea haki za watu Weusi Marekani ni hatari.

13. Takwimu za sasa za Marekani ni za kupotosha. Anasema ukosefu wa ajira umefikia 20% kinyume na takwimu rasmi zinazoonyesha ni 5.1%.

14. Utajiri wake ni $10bn.

15. Mfumo wa kutoa huduma za afya kwa wanajeshi wa zamani unafaa kufanyiwa mabadiliko makubwa.

16. Mpango wa Obamacare ambao ulilenga kuongeza idadi ya Wamarekani wanaopata bima ya afya ni “mkasa”.

17. Mabadiliko ya tabia nchi ni hali ya kawaida tu ya hewa.

18. Ulimwengu ungekuwa pahala pema pa kuishi kama Saddam Hussein na Muammar Gaddhafi wangekuwa bado madalakani.

19. Angewarejesha makwao wahamiaji kutoka Syria wanaotafuta hifadhi Marekani.

harusi ya wapenzi wa jinsia moja, hakufaa kazi hiyo.

20. Yeye ni “mtu mzuri sana” na anataka sana kurejesha hadhi ya Marekani.

Ijumaa, 26 Februari 2016

Majambazi Wavamia Benki Mbagala

Majambazi Dar yavamia benki yapora yaua, yauawa

Majambazi ambao idadi yao haikufahamika wakiwa na mabomu na bunduki za kisasa jana walivamia

Polisi wakiimarisha ulinzi nje ya tawi la Benki ya Access lililopo Mbagala, Dar es Salaam baada ya kuvamiwa na majambazi na kupora fedha. Picha na Raymond Kaminyoge

Dar es Salaam. Majambazi ambao idadi yao haikufahamika wakiwa na mabomu na bunduki za kisasa jana walivamia benki ya Access, tawi la Mbagala wakapora viroba vya fedha, wakaua mlinzi na baadaye wanne kati yao wakauawa na polisi

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema baada ya majambazi hao kufika katika benki hiyo kwa bodaboda nne majira ya saa nane mchana, yalimuua mlinzi wa benki hiyo, kisha kubomoa kwa risasi mlango wa vioo na kuingia ndani na kuzua taharuki kubwa.

Mashuhuda hao walisema katika tukio hilo lililodumu kwa karibu saa moja, mmoja wa majambazi hao aliyekuwa amevaa kininja, alikuwa barabarani akiamuru magari kupita haraka huku akifyatua risasi ovyo.

Ilielezwa kuwa jambazi huyo aliyeonekana kuwa na uzoefu na matumizi ya bunduki alikuwa akifyatua risasi kwa kutumia mkono mmoja na ndiye aliyewajeruhi  baadhi ya wapita njia.

Hivyo, wakati uporaji ukiendelea na jambazi huyo akiimarisha ulinzi barabarani baadaye hakukuwa na magari wala pikipiki zilizokuwa zikipita.

Mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi jirani na benki hiyo, Ramadhani Tairo alisema  baada ya  jambazi huyo kuliona gari la polisi likielekea eneo hilo, alifyatua risasi na kulipiga kabla halijafika ma kupoteza mwelekeo na kutumbukia kwenye mtaro.

Tairo alisema mbali ya jambazi hilo kulipiga risasi gari la polisi pia alilirushia bomu la mkono,  lakini liliangukia barabarani bila kulipuka. Polisi walifanikiwa kulitegua bomu hilo baadaye likiwa halijasababisha madhara kwa wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Rebeca Maliva alisema majambazi walioingia ndani ya benki hiyo walionekana wakitoka wakiwa na viroba vitatu vya fedha ambavyo walivipakata kwenye pikipiki na kuondoka kwa kasi kuelekea Mkuranga kupitia barabara ya Kilwa.

Rebeca alisema polisi zaidi walifika kwenye eneo hilo wengine wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kuwafukuza majambazi hao ambao walipofika eneo la Shule ya St Mary’s, walitupa  kiroba kimoja ambacho wananchi waliokuwa jirani waligombania na kuchukua fedha zilizokuwamo.

“Baada ya milio ya risasi nilikuwa nimejifungia ndani nikawa nachungulia nje nikawaona watu wanagombea fedha, kila mtu aliyekuwa hapo alionekana na burungutu la noti na kukimbia,” alisema Rebeca ambaye yeye na familia yake hawakuthubutu kutoka.

Baada ya nusu saa wakati umati ukiwa bado kwenye benki hiyo, magari ya polisi yalipita katika eneo hilo yakitokea eneo la Mkuranga  yakiwa yamebeba miili ya majambazi waliouawa.

Magari hayo yalikuwa yakisindikizwa na vijana wa bodaboda waliokuwa wakishangilia kazi  iliyofanywa na polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alizungumzia kwa ufupi tukio hilo kwamba majambazi manne yaliuawa na kukamata silaha tatu, lakini hakutaka kuingia kwa undani akisema atatoa taarifa zaidi leo

Jumanne, 9 Februari 2016

Undani wa Sakata La Mwanafunzi Wa Kitanzania Aliyedhalilishwa India

Stori: Mwandishi Wetu, UWAZI na mitandao

DAR ES SALAAM: Lile sakata wa mwanafunzi wa kike Mtanzania (jina linahifadhiwa), kupigwa, kuvuliwa nguo na kisha kulazimishwa kutembea akiwa uchi limetolewa undani wake, Uwazi lina mlolongo wote.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 21 anayesoma Shahada ya Biashara, mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Acharya, Bangalore nchini humo, alifanyiwa ukatili huo akiwa na Watanzania wengine wanne.

GAZETI LA INDIA LILIANZA KUFICHUA
Gazeti la Deccan Chronicle la Mji wa Bangalore ndilo lilikuwa la kwanza kuandika habari hiyo iliyojiri Januari 31, mwaka huu na hivyo kuufungua macho ulimwengu juu ya tukio hilo la kikatili.

BADO YUPO HOSPITALI
Baada ya mwanafunzi huyo kutendewa unyama huo, baadhi ya Watanzania wamesema alifariki dunia katika eneo la tukio lakini ukweli ni kwamba, majeruhi huyo bado amelazwa kwenye Hospitali ya Peenya iliyopo Bangalore nchini humo.

WATANZANIA WAUNGANISHA
Kumekuwa na picha kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ya mwanaume anayedaiwa kuwa ni Mtanzania ambaye alifariki dunia nchini humo kwa ajali ya pikipiki ambapo vyanzo vinasema alijipiga kwenye nguzo ya pembeni mwa barabara.Picha hiyo, ndiyo wengi wamekuwa wakiitumia kusema ni ya mwanafunzi Mtanzania aliyedhalilishwa.

MWANAFUNZI MBONGO
Akizungumza na Uwazi juzi, mwanafunzi mmoja anayesoma kwenye chuo hicho, alisema bado tukio hilo linawagonga vichwa wanafunzi wote Waafrika licha ya Serikali ya India kuchukua hatua inayostahili, ikiwemo kuwawekea ulinzi wanafunzi wa Kitanzania.

MWANAFUNZI ASHAURIWA KURUDI
“Watu wanaweza kusema mengi lakini ni tukio lenye kumbukumbu mbaya sana kwa mwenzetu. Ubaguzi ulitawala kwa wale wachache waliohusika. Tunafikiria kwamba, akipata nafuu arudi nyumbani kupumzika. Kwani kwa kuendelea kusoma sidhani kama ataingiza ‘matirio’ kichwani.

“Kwanza tukio limemjengea hofu. Halafu bado atakuwa katika mji huuhuu na watu atawaona walewale. Vyema arudi kupumzika. Lakini ni ushauri tu, si lazima iwe hivyo na pia itategemea ujasiri aliozaliwa nao,” alisema mwanafunzi huyo akiomba hifadhi ya jina lake.

ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, siku ya tukio, raia wa Sudan aitwaye Ismail Ahad Mohammed (20) inayedaiwa alikuwa ‘amekunywa’, alimgonga mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35, mkazi wa Mji wa Hesaraghatta na kusababisha kifo chake.

KILICHOTOKEA SASA
“Sasa baada ya dakika kama thelathini hivi kupita, Watanzania watano, akiwemo dada yetu aliyevuliwa nguo, walifika eneo hilohilo wakiwa ndani ya gari dogo. Ndipo kundi la watu walipoanza kuwashambulia akiwemo dada yetu. Washambuliaji waliona ni walewale tu.”

UKATILI ULIPO
“Kuwashambulia tumechukulia ni sehemu ya hasira za kuona watu ni walewale, lakini sasa kitendo walichomfanyia sista wetu cha kumvua nguo na kumlazimisha atembee uchi ndiyo kilikuwa kibaya sana.

“Lakini pia kundi hilo la watu lilichoma moto lile gari la kwanza lililosababisha ajali mpaka akafa mwanamke na pia walichoma moto gari alilokuwemo dada yetu na wenzake. Wengine walikimbia lakini dereva wa gari la pili naye alishambuliwa, gari la kwanza alikamatwa na polisi.”

LAWAMA ZA POLISI
Polisi wa mji huo wamebebeshwa lawama kwamba licha ya kuwepo eneo la tukio lakini hawakuchukua hatua yoyote. Mbaya zaidi, mwanaume mmoja raia wa nchi hiyo alijitolea kumsitiri mwanafunzi huyo kwa kumpa T-Shirt (fulana) yake lakini watu hao walimpiga na kuichanachana nguo hiyo.

UKATILI KWENYE DALADALA
Kuna maelezo kwamba, mwanafunzi huyo alipoona hali inazidi kuwa mbaya, alikimbilia kwenye ‘daladala’ la huko akiamini kwamba litaondoka hivyo yeye kunusurika na kipigo na kusitiriwa kwa nguo lakini baadhi ya abiria walimshusha ili aendelee kudhalilishwa hivyo kumfanya aendelee kuwepo mtaani akitembea bila nguo.

DEREVA APIGWA
Mshauri wa masuala ya sheria kwa wanafunzi kutoka Afrika wanaosoma Bangalore, Bosco Kaweesi alisema naye dereva wa gari alilokuwemo Mtanzania huyo, Micah Pundugu alipigwa na kujeruhiwa vibaya.

WATANZANIA BONGO WAONGEA
Baadhi ya Watanzania hapa Bongo wameongea na Uwazi na kuonesha mtazamo wao kuhusu sakata hilo.
Musa Ibrahim, mkazi wa Mabibo jijini Dar yeye alisema:

“Kwa kweli sisi hapa nyumbani Tanzania tunaishi kwa upendo mkubwa na hawa ndugu waishio hapa. Kwa hiyo walichofanya wale si haki. Lakini bahati nzuri ni kwamba, kitendo kile hakijaungwa mkono na raia wote wa nchi ile.

“Ndiyo maana kuna raia alijitolea fulana, lakini pia Serikali ya India imechukua hatua kali sana kwa wahusika ambao wamekamatwa, polisi wamesimamishwa kazi, wengine kufukuzwa.”
Mama Prince, mkazi wa Kimara Baruti yeye alisema: “Mimi sikubaliani kama tukio lile lilikuwa la kila raia wa kule. Ni wale wakorofi tu.

Mbona hata hapa nyumbani kuna Watanzania wanaweza kufanya vile kwa Watanzania wenzao. Unajua kila nchi ina watu wakorofi, wakatili na wapuuzi. Sasa upuuzi wa watu wachache usiwapake matope wote. Ila kama Serikali ya India ingekaa kimya, hapo sasa naamini moto wake ungekuwa mkubwa.”

BALOZI WA TANZANIA
Naye Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alisema ameridhika kwa namna ambayo serikali ya nchi hiyo imeweka mikakati ya kutosha kuwalinda wanafunzi kufuatia kisa hicho.

“Cha muhimu ni kuangalia siku za mbele kwa sababu tusipofanya hivyo tutapotea. Tunahitaji kutatua tatizo la sasa lakini pia tuangalie mikakati ya muda mrefu,” alisema Balozi Kijazi.Akaendelea: “Nimeridhishwa na hatua za kiusalama ambazo zimechukuliwa na Serikali ya India kwani kuna maafisa ambao wamesimamishwa kazi mara moja.”

KILICHOJIRI BAADA YA TUKIO
Mpaka sasa, watu tisa wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku
Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Soldevenahalli akisimamishwa kazi kwa tuhuma kwamba, hakuchunguza kwa undani kisa hicho baada ya mmoja wa wanafunzi hao kutoa taarifa kituoni na konstebo wa polisi mmoja pia amesimamishwa kazi kwa kutochukua hatua kuzuia wanafunzi hao wasishambuliwe na umati.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augostine Mahiga wiki iliyopita Bungeni Dodoma alitolea ufafanuzi sakata hilo jinsi Serikali ya India inavyolishughulikia na kumfanya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kutokwa na machozi kwa uchungu wa simulizi yenyewe.

Gazeti hili bado linachimba habari hii baada ya kuwepo madai kwamba, mwanafunzi huyo atarejeshwa nchini wakati wowote huku akidaiwa kuwa ni mzaliwa wa Mkoa wa Mwanza.

Jumatatu, 8 Februari 2016

Daniel Yona na Basil Mramba Waanza kutumikia kifungo Cha Nje

Daniel Yona akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili Hospitali ya Palestina, Sinza – Dar.Yona na Mramba  wakiwa wameshika vifaa vya kufanyia usafi.
Yona akionesha vifaa vya kufanyia usafi alivyokabidhiwa.
Mramba na Yona wakikabidhiwa vifaa vya kufanyia usafi.
Wakioneshwa mazingira ambayo watakuwa wakiyafanyia usafi kwa kipindi chote cha adhabu yao.Ofisa Mazingira wa Hospitali ya Palestina-Sinza, Bi. Miriam Mongi (mwenye brauzi nyekundu) akimkabidhi Yona vifaa vya kufanyia usafi.Yona na Mramba wakiwa wamevaa ‘ovaroli’.

Ofisa Huduma za Jamii wa Hospitali ya Palestina – Sinza, Bw. Deogratius Shirima akizungumza na wanahabari hospitalini hapo 
Maeneo ya hospitalini hapo.
Gari lao likiwasili.
Yona akiwasili hospitalini hapo.Takataka  katika baadhi ya maeneo hospitalini hapo. 

Wanahabari wakichukua matukio.

 

WALIOKUWA Mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona leo wameanza kutumikia adhabu ya kifungo cha nje, kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza, Palestina, ya jijini Dar, kulingana na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wiki iliyopita kuhusu kesi iliyokuwa ikiwakabili.

Mramba aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini waliwasili mapema leo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Hospitali ya Sinza Palestina ili kuanza kutumikia adhabu hiyo kama mahakama ilivyowaamuru.

Baada ya kuwasili hospitalini hapo, Yona na Mramba walipokelewa na ofisa huduma za jamii Bw. Deogratius Shirima na wananchi wengine waliokuwepo kushuhudia vigogo hao wakitumikia adhabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Shirima alisema kuwa, leo ilikuwa ni siku ya kuwapa maelekezo namna ambavyo watafanya usafi, maeneo ya kufanya usafi pia walikabidhiwa vifaa watakavyovitumia kufanyia usafi kuanzia kesho.

Baadaye Afisa Mazingira hospitalini hapo Bi. Miriam Mongi, aliwakabidhi Yona na Mramba vifaa vya kufanyia usafi ambavyo ni; mifagio, mafyekeo, viatu vya kufanyia usafi maarufu kama “gambuti” na glovusi.

Oktoba 2, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili na si miaka mitatu.

Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya ndipo hivi karibuni baada ya mahakama kupitia upya kesi hiyo ikaamuru wapewe adhabu ya kifungo cha nje huku wakifanya kazi za kijamii kwa muda wa saa nne kila siku kwa miezi sita.

Makamishna Wa Uchaguzi ZEC Wapinga Uchaguzi Kurudiwa

uchaguzi Z’bar

 0

 0

 0

 0

 0

 0

 0

 

Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Ayoub Bakari Hamad akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana kuhusu uchaguzi wa marudio visiwani humo. Kushoto ni mjumbe mwenzake, Nassor Khamis Mohammed. Picha na Salim Shao 

Kwa ufupi

Wajumbe hao wa chombo hicho cha uchaguzi pia wamesema hoja ya kupanga tarehe mpya ya uchaguzi iliyopendekezwa na mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha ilipingwa na wajumbe watatu na kuungwa mkono na wengine watatu.

By Raymond Kaminyoge, Mwananchi

Dar es Salaam. Makamishna wawili wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) wamejitokeza hadharani na kutangaza kupinga kurudiwa kwa uchaguzi wa rais, wawakilishi na madiwani, uamuzi wa kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 uliofanywa na mwenyekiti badala ya tume kinyume na sheria.

Wajumbe hao wa chombo hicho cha uchaguzi pia wamesema hoja ya kupanga tarehe mpya ya uchaguzi iliyopendekezwa na mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha ilipingwa na wajumbe watatu na kuungwa mkono na wengine watatu.

Makamishna hao, Nassor Khamis Mohamed na Ayoub Bakar Hamad walisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba uchaguzi uliofanyika Zanzibar hautafutika kwa kuwa ulikuwa halali kikatiba.

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi na miezi miwili baadaye aliitangaza Machi 20 kuwa tarehe mpya ya kupiga kura.

Uchaguzi huo ulifutwa siku ambayo mshindi wa kiti cha urais alitakiwa atangazwe, huku matokeo ya majimbo 31 yakiwa yameshatangazwa na kura katika majimbo mengine tisa zikiwa zimeshahesabiwa. Pia, washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani walishatangazwa na kupewa hati za ushindi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Nassor aliwataka wajumbe wenzake wa ZEC kutounga mkono uchaguzi wa marudio ili wasiwe sehemu historia mbaya ya nchi hiyo.

Alisema kifungu cha 119 (10) cha Katiba ya Zanzibar hakitoi nafasi kwa mwenyekiti peke yake kufanya uamuzi wa kufuta matokeo kwa jina la tume.

“Uamuzi mkubwa uliofanywa na mwenyekiti hauwezi kuchukuliwa kuwa uamuzi wa Tume na kurudia uchaguzi ni kuiweka nchi katika majaribu,” alisema.

Nassor alisema uchaguzi wa Zanzibar ulishakamilika katika ngazi za uwakilishi na udiwani huku wateule katika nafasi hizo wakikabidhiwa vyeti vyao kuthibitisha ushindi wao.

“Hakuna chombo chochote kinachoweza kubatilisha uchaguzi isipokuwa Mahakama Kuu baada ya kusikiliza shauri. Hao ndio ambao wametajwa kwenye sheria ya uchaguzi,” alisema.

Alisema uchaguzi wa rais wa Zanzibar haukulalamikiwa na mgombea yoyote kati ya 14 waliowania nafasi hiyo.

Nassor alisema yeye na wenzake wameendelea kuwepo kwenye tume hiyo ili kutoa ushauri kwa wenzao na pia kujua kinachoendelea na kuwafahamisha wananchi.

“Kwa hali ya Zanzibar ilivyo sasa anahitajika mpatanishi wa kimataifa ambaye ataziweka pande mbili za vyama vya siasa zinazotofautiana kisiasa katika meza ili kufikia suluhu,” alisema.

Kwa upande wake, Ayoub alisema Jecha anatakiwa kujipima, afanye uamuzi mgumu ili kuiepusha nchi kuingia katika vurugu.

Alisema kama uchaguzi huo ukifanyika, utatoa viongozi batili kwa sababu uchaguzi halali Zanzibar ulishafanyika.

Nassor alidai kuwa siku mbili baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar, Jecha aliitisha kikao na kuomba wajumbe waunge mkono uamuzi huo, lakini nusu ya wajumbe walimuunga mkono na wengine walipinga.

Alisema Januari 21, mwaka huu tume ilikuwa na kikao kingine ili kujadili tarehe ya uchaguzi wa marudio.

“Baadhi ya wajumbe waliamua kuwa Machi 20, 2016 iwe ndiyo siku ya uchaguzi na wengine walipinga uchaguzi wakisema ufutaji wa matokeo ulikuwa batili kikatiba na kisheria,” alisema.

Alisema wakati Rais John Magufuli anachukua hatua nzito kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma, nchi yenye uchumi mdogo kama Zanzibar inatumia zaidi ya Sh7 bilioni kufanya uchaguzi wa marudio.

Jumatano, 3 Februari 2016

Bajeti Mpya Ya Serikali hii hapa


=

WEDNESDAY, FEBRUARY 3, 2016

Funga mkanda yawakuna wasomi

 0

 0

 0

 0

 0

 0

 0

 

 

Kwa ufupi

Katika mwongozo huo, Dk Mpango aliainisha mambo kadhaa ambayo ni vipaumbele vya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016/17 na kutaja mbinu za ukusanyaji mapato, kudhibiti mfumuko wa bei, kuongeza mapato ya kodi na kupunguza matumizi ya Serikali.

By Florence Majani, Mwananchi fmajani@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mpango wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/ 2017 uliotolewa juzi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango katika hotuba yake umepongezwa na wachumi huku wakiwa na wasiwasi kuhusu utekelezaji wake.

Katika mwongozo huo, Dk Mpango aliainisha mambo kadhaa ambayo ni vipaumbele vya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016/17 na kutaja mbinu za ukusanyaji mapato, kudhibiti mfumuko wa bei, kuongeza mapato ya kodi na kupunguza matumizi ya Serikali.

Mengine ni kuimarisha viashiria vya uchumi na maendeleo, marejesho ya kodi, kupunguza gharama, kukuza pato halisi la Taifa na kupunguza nakisi ya Serikali kwenye misaada ya nje kwa zaidi ya asilimia tatu.

Kuimarisha mapato ya ndani

Katika hotuba yake, Dk Mpango alisema shabaha ya bajeti ya mwaka 2016/17 inalenga kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri kufikia asilimia 14.8 ya Pato la Taifa. Alisema mapato hayo yanatakiwa yafikie asilimia 15.3 mwaka wa fedha 2017/18 na asilimia 16.3 ifikapo 2019/20.

Ukusanyaji wa mapato

Katika ukusanyaji wa mapato ya kodi ili yafikie asilimia 13.2 ya Pato la Taifa kwa mwaka 2017/18 na asilimia 13.5 mwaka 2019/20, Dk Mpango alisema Serikali imefuta usimamiaji wa mapato unaofanywa na taasisi za Serikali na badala yake mapato hayo yatakusanywa na Wizara ya Fedha na Mipango.

Maeneo mengine ni kukusanya kodi za majengo, kurasimisha biashara ambazo hazijarasimishwa na kusimamia upatikanaji wa matumizi sahihi ya mashine ya EFD.

Kadhalika, hotuba hiyo ilisisitiza kupitiwa upya mikataba iliyopewa misamaha ya kodi.

Katika kipindi cha 2016/17 bajeti hiyo ililenga kukusanya jumla ya Sh14.1 bilioni kutoka kwenye vyanzo vya ndani ambayo ni asilimia 13.2 ya pato la ndani. Hiyo ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.

Pato la Taifa na mfumuko wa bei

Aliitaka shabaha kuu kuwa ni kukuza pato halisi la Taifa kutoka asilimia saba mwaka 2015 hadi asilimia 7.2 kwa 2016 na kufikia asilimia nane 2017.

Mwongozo huo ulilenga pia kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha unabaki kwenye tarakimu moja na kufikia asilimia sita Juni 2016 na kubaki kati ya asilimia tano na nane katika kipindi cha muda wa kati.

Kupunguza matumizi

Waziri alisema Serikali ina mpango wa kupunguza matumizi yake kutoka asilimia 23.9 ya Pato la Taifa mwaka 2015/16 hadi asilimia 21.5 mwaka 2016/17.

Pia alitaka mashirika ya umma; Tanesco, Tazara, Shirika la Reli (TRL) Shirika la Ndege (ATCL) na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), yajitegemee na kutengeneza faida badala ya kutegemea ruzuku ya Serikali.

Bajeti ya Serikali

Dk Mpango alisema bajeti hiyo inatarajia kupunguza nakisi ya Bajeti ya Serikali kwenye misaada ya nje kutoka asilimia 4.2 mwaka 2015/16 hadi chini ya asilimia 3.0.

Jumla ya Sh22, 991. 5 bilioni zinatarajiwa kukusanywa. Kati ya hizo, mapato ya ndani na ya halmashauri yataongezeka na kufikia Sh15,801 bilioni sawa na asilimia 69.7 ikilinganishwa na asilimia 62.2 ya 2015/16.

Katika jumla hiyo, mapato yasiyo ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya halmashauri yatakuwa Sh584 bilioni, pia Serikali itakopa kiasi cha Sh1,782 bilioni kutoka vyanzo vya nje vyenye masharti ya kibiashara, mikopo ya ndani Sh3,300 bilioni na wadau wa kimaendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh2,107 bilioni katika kipindi hicho.

Changamoto za nusu ya 2015/16

Licha ya kutoa shabaha ya bajeti ya mwaka 2016/17, Dk Mpango alieleza changamoto zilizoonekana kwenye bajeti ya nusu mwaka ya 2015/16 kuwa ni ukwepaji kodi kwa wafanyabiashara wasio waadilifu, mwitikio hasi kwenye matumizi ya EFD, kuongezeka kwa matumizi ya Serikali kusikowiana na hali halisi ya mapato na mazingira magumu ya ukusanyaji wa kodi katika sekta zisizo rasmi.

Wachumi wazungumzia mwongozo

Akizungumzia mkakati wa Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Gaudence Mpangala alipongeza mpango huo akisema katika Awamu ya Nne, Serikali ilikithiri kwa kuwa na matumizi mabaya ya fedha.

“Dk Mpango amefanya vyema kuweka hilo kwenye mwongozo. Kwa mfano, wabunge wasifanye sherehe zisizo za lazima na kupunguza safari za nje, yote hiyo ni azma ya kubana matumizi. Hilo tunalipongeza,” alisema.

Alisema hata Uchaguzi Mkuu ulikuwa na matumizi makubwa yasiyo ya lazima kwani hakukuwa na haja ya kununua magari ya polisi 770 wakati wa uchaguzi.

Kuhusu mashirika ya umma, Profesa Mpangala alisema yakifanya kazi kwa ufanisi yanaweza kujiendesha lakini kikwazo ni ufisadi na rushwa.

“Lakini suala si haya mashirika kujitegemea tu, bali kuweka mikakati dhabiti na kuondoa vikwazo vinavyofanya yasiendelee,” alisema.

Kuhusu mfumuko wa bei na ukusanyaji wa mapato, mchumi na mtafiti wa maendeleo wa Repoa, Profesa Samwel Wangwe alisema kwa kuwa uongozi wa sasa unaonekana makini, malengo hayo yatawezekana.

“Uongozi wa sasa si holela holela, watekelezaji wamefanya kazi yao. Kule kubana matumizi ni sawasawa ili fedha zihudumie watu na si watumishi,” alisema.

Mhadhiri wa uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Stephen Kirama alisema miongozo na shabaha iliyotolewa na Waziri wa Fedha ni ya kisomi lakini ina changamoto kadhaa. Alisema kumlazimisha mfanyabiashara kutumia mashine za EFD ni jambo la moja na kuzitumia ni jambo jingine. “Lakini je, watu watakubali kudai risiti?” alisema.

Aliongeza zaidi kuwa katika suala la ukusanyaji wa kodi atakutana na changamoto za kutambua, kuorodhesha, kurasimisha na namna gani watachukua mkakati wa kukusanya kodi.

Kuhusu kupunguza utegemezi wa fedha za wahisani katika bajeti hadi kufikia asilimia chini ya tatu, Meneja Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa Hakielimu, Godfrey Bonaventure alisema ili kufanikisha hilo ni lazima Serikali ipanue wigo wa ukusanyaji mapato.

Alisema ni lazima bajeti iendane na matumizi kwa kuhakikisha inakusanya mapato kutoka vyanzo vikuu vya mapato.     

Jumamosi, 30 Januari 2016

Panga La JPM Laondoa Vichwa 152

Panga la JPM lachinja vichwa 152

Hakuna shaka kuwa Rais John Magufuli anatimiza ahadi yake ya kutumbua majipu aliyoitoa katika

Rais John Magufuli.

Dar es Salaam. Hakuna shaka kuwa Rais John Magufuli anatimiza ahadi yake ya kutumbua majipu aliyoitoa katika hotuba yake ya kwanza bungeni baada ya zaidi ya watumishi 152 wa Serikali kutimuliwa hata kabla ya siku 100 kutimia.

Hao ni watumishi waliotimuliwa kwa majina au vyeo vyao, lakini ukijumlisha na wengine waliosimamishwa au kufukuzwa kwa matamko bila kutajwa majina, idadi ni kubwa zaidi.

Watumishi hao wamesimamishwa na baadhi wamefukuzwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali za kukiuka Sheria ya Ununuzi wa Umma, Rais kutoridhishwa na utendaji wao, wizi kwenye taasisi zao, ukwepaji kodi, tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na utovu wa nidhamu.

Hatua hizo ni utekelezaji wa ahadi ambazo Rais Magufuli alitoa kwenye hotuba yake ya kwanza bungeni Novemba 2, mwaka jana mjini Dodoma, alipoahidi kupambana na rushwa bila kigugumizi wala haya yoyote.

“Dawa ya jipu ni kulitumbua na mimi nimejipa kazi ya kuwa mtumbua jipu. Najua kutumbua jipu kuna maumivu lakini bahati mbaya halina dawa nyingine,” alisema.

Timuatimua hiyo, ambayo ilimgusa katibu mkuu wa wizara, wakurugenzi wa taasisi na watumishi waandamizi, ilifanywa pia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadhi ya mawaziri wa JPM.

Hadi sasa, taasisi zilizopewa jukumu la kuwachunguza na kuwafikisha mahakamani watumishi walioonekana na matatizo, bado hazijatoa taarifa wala kuchukua hatua.

Akizungumzia kusimamishwa kazi kwa watumishi hao, mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma, Florence Temba alisema iwapo Rais, Waziri Mkuu au Waziri ameagiza mtumishi asimamishwe kazi, huanza kuangaliwa wakati uchunguzi unafanyika.

Alisema iwapo kiongozi atasema mtumishi amefukuzwa kazi, ni dhahiri kuwa huyo ameondolewa kabisa katika ajira za Serikali.

“Hata hivyo, baadhi ya wanaosimamishwa huweza kuendelea kulipwa mishahara yao kulingana na mazingira ya kesi zao,” alisema.

Bosi wa Muhimbili

Hatua za kusimamisha na kutimua zilianza siku nne tu baada ya Rais kuapishwa, ambapo Novemba 9, 2015 alimsimamisha kazi kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hussein Kidanto, na kuivunja bodi hiyo iliyokuwa na wajumbe 11.

Rished Bade

Rais Magufuli alimfukuza kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade Novemba 27.

Bodi ya TPA

Desemba 7 , mwaka jana, Magufuli alivunja bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Profesa Joseph Msambichaka na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe.

Bodi ya TPA ilikuwa na wajumbe wanane, ambao ni Dk Tulia Ackson, ambaye sasa ni Naibu Spika wa Bunge, Mussa Ally Nyamsingwa (Mhandisi wa Ujenzi), Donata Mugassa (mtaalamu wa ununuzi na mjumbe wa Bodi ya Posta), na Haruna Masebu (mkurugenzi mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

Wajumbe wengine ni Flavian Kinunda, Mhandisi Gema Modu, Dk Francis Michael na Crescentius Magori.

Pia, aliwasimamisha kazi wasimamizi wanane wa Bandari Kavu (ICD) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante na James Kamwomwa.

Wengine ambao hawakuwamo kwenye ripoti hiyo ambao ni viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa makontena kutoka ndani ya bandari lakini ni wahusika wakuu ni Shaban Mngazija aliyekuwa meneja mapato, Rajab Mdoe (mkurugenzi wa fedha na mkuu wa Bandari Kavu), Ibin Masoud (kaimu mkurugenzi wa fedha), Apolonia Mosha (meneja msaidizi wa Bandari-Fedha). Jumla ya waliotimuliwa TPA na TRA ni 47.

Dk Hoseah

Akiendelea na kasi yake ambayo ameipa jina “kutumbua majipu”, Desemba 16, 2015 Rais alitengua uteuzi nafasi nyeti ya mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah. Rais alisema alichukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa Takukuru chini ya mkurugenzi huyo.

Maofisa wengine wa taasisi hiyo walisimamishwa kazi kwa kukiuka maagizo yaliyohusu safari za nje. Waliosimamishwa kazi ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas, wakiwa watumishi waandamizi wa taasisi hiyo.

Bosi wa Rahco

Rais JPM alimsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za Reli Tanzania (Rahco), Benhadard Tito Desemba 23, 2015 kwa kile kilichoelezwa ni “ukiukwaji mkubwa wa taratibu za ununuzi” katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati. Pia alivunja bodi ya Rahco yenye wajumbe wanane na bodi ya TRL yenye wajumbe wanane pia.

Katibu tawala Mwanza

Akiendelea na kasi hiyo, Januari 15, alitengua uteuzi na kumfukuza kazi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Faisal Issa kutokana na “utovu wa mkubwa wa nidhamu” aliounyesha katika kikao cha cha kamati ya ulinzi kilichofanyika mjini Mwanza.

Idara ya Uhamiaji

Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia utawala na fedha, Piniel Mgonja Januari 21 ili kupisha uchunguzi baada ya kubaini dosari kadhaa kwenye ofisi hiyo.

Mkurugenzi Nida

Utumbuaji huo wa majipu haukushia hapo. Januari 25, Dk Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu kutokana na matumizi yasiyoridhisha ya Sh179 bilioni.

Wengine waliosimamishwa Nida ni Joseph Makani ambaye ni mkurugenzi wa Tehama, Rahel Mapande (ofisa ugavi mkuu), Sabrina Nyoni (mkurugenzi wa sheria) na George Ntalima, ofisa usafirishaji.

Pia, aliwarudisha nyumbani mabalozi wawili, Dk Batilda Buriani aliyekuwa Japan, Dk James Msekela (Roma, Italia). Pia, Peter Kallaghe (Uingereza) na kurejeshwa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano, Kikanda na Kimataifa.

Waziri Mkuu

Wakati Rais Magufuli akitimua watumishi hao wa umma, Novemba 27, mwaka jana, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimsimamisha kazi Kamishna wa Kodi na Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki, Habibu Mponezya wa kitengo cha huduma kwa wateja, Haruni Mpande na Hamis Ali wa kitengo cha Tehama na Eliachi Mrema wa Bandari Kavu. (ICD).

Baadaye Novemba 29, Majaliwa aliwafukuza wafanyakazi watatu wa TRA, Anangisye Mtafya, Nsajigwa Mwandengele na Robert Nyoni.

Kigoma

Majaliwa aliwasimamisha watumishi tisa wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Januari 8 kwa tuhuma za kuingia mikataba mibovu isiyokuwa na tija na kuisababishia manispaa kupoteza mapato. Pia wanatuhumiwa kulipa fidia batili na kuuza mali za halmashauri kinyume cha sheria.

Ruvuma

Kadhalika, akiwa mkoani Ruvuma Januari 8, Majaliwa alimsimamisha kazi meneja uendeshaji wa kiwanda cha kusindika tumbaku (Sontop), Paul Balegwa akidaiwa kushiriki kwa namna moja au nyingine kufanya ubadhirifu wa fedha za wakulima na hivyo kiwanda hicho kusitisha uzalishaji kwa zaidi ya miaka 18 iliyopita.

Mawaziri

George Simbachawene (Tamisemi) alimsimamisha kazi mtendaji mkuu mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Asteria Mlambo.

Waziri huyo pia alitoa agizo la kusimamishwa kwa ofisa biashara wa Manispaa ya Ilala, Dennis Mrema. Hali kadhalika, Mkurugenzi wa Manispaa za Kigoma, Mhandisi Boniface Nyambele na mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, Suleiman Lukanga.

Simbachawene pia aliwasimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Augustino Kalinga na wenzake kaimu ofisa biashara wa manispaa hiyo, Elias Kamara na Donatila Vedasto kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), amewasimamisha kazi wafanyakazi 15 wa Mamlaka ya Bandari kwa tuhuma za upotevu wa Sh48 bilioni.

Wizara pia iliwasimamisha wakuu wanne wa idara wa kampuni ya huduma za meli (Marine) kwa tuhuma ya ubadhirifu wa zaidi ya Sh600 milioni.

Profesa Jumanne Magembe (Maliasili na Utalii), amemsimamisha kazi mkurugenzi wa mipango na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu wa wakala wa misitu nchini, Mohammed Kilongo na maofisa wa misitu wa mikoa yote nchini.

Mwigulu Nchemba (Kilimo, Mifugo na Uvuvi), amemtimua mkuu wa mnada wa mifugo wa Pugu na watumishi walioshiriki kuiba ushuru wa Serikali.

Pia aliagiza viongozi tisa wa vyama vya ushirika vya Mfyome, Magubike, Kiwemu, Kitai, Mhanga na Kampuni ya Umoja wa Wakulima wa Tumbaku Iringa (ITCOJE Ltd), wakabidhi ofisi zao kutokana na tuhuma za kutapeli trekta za mkopo.

Ummy Mwalimu (Afya), amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Diwani Msemo.

Jenista Mhagama (Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), alimtimua mkandarasi wa mfereji wa Buguruni kwa Mnyamani.

Simiyu

Januari 29, Rais John Magufuli aliwafukuza kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Erica Mussika kwa shindwa kusimamia mradi mkubwa wa barabara wa Sh9.192 bilioni, uliofanikishwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia na amemfukuza kazi Mhandisi wa ujenzi, Ruben Muyungi.

Maoni ya wasomi

Akizungumzia hatua hizo, mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Hamad Salim alisema anapata shaka na aina hiyo ya utendaji.

“Labda kwa Rais ambaye huenda akawa na mkono mrefu wa kupata taarifa kuhusu watendaji anaowachukulia hatua, ila kwa hao wengine napata shaka,” alisema.

Salim alisema anachokiona kwa mawaziri ni ushabiki wa kuiga staili ya utendaji wa Rais Magufuli, ili waonekana wanafanya kazi.

Naye, Dk Benson Bana alisema maamuzi hayo yana matokeo ambayo ni ya sura mbili, hasi na chanya.

Dk Bana, ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema kufanya hivyo kutasababisha watumishi wa umma wafanye kazi kwa woga.

Alisisitiza kuwa kwa wale wanaosimamishwa kupisha uchunguzi, unapomalizika na mtumishi akibainika hana hatia, basi atangazwe kuwa amerejeshwa kazini kuliko mambo kufanyika kimyakimya.

“Kwa sasa wafanyakazi wanafanya kazi wakiwa na hofu kwamba huenda waziri atatokea itakuwaje, “ alisema Bana.

Akizungumzia matokeo chanya, alisema hatua ya kuwajibishwa watendaji hao, imerejesha utendaji mzuri katika ofisi za umma kwa sababu kuna baadhi zilikuwa zimekithiri ufisadi, rushwa na uzembe.

-

Balozi Amina:Bado nautaka Uraisi

Balozi Amina: Bado nautaka urais

Amina Salum Ali, ambaye alishika nafasi ya pili kwenye mbio za urais ndani ya CCM, amesema ndoto

Balozi Amina Salum Ali .

Amina Salum Ali, ambaye alishika nafasi ya pili kwenye mbio za urais ndani ya CCM, amesema ndoto yake ya kushika nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini, haijafa.

Amina, ambaye alikuwa balozi wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, alisema hayo kwenye mahojiano maalum na Mwananchi yaliyofanyika mapema wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Balozi Amina alichomoza kwenye mbio za urais ndani ya CCM baada ya kuingia tano bora, akiwa pamoja na John Magufuli, Asha Rose Migiro, January Makamba na Bernard Membe na baadaye kuingia tatu bora kwa ajili ya kupigiwa kura na Mkutano Mkuu wa chama hicho ambao ulimchagua Magufuli kugombea urais.

Lakini Balozi Amina, ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 59, anasema hilo halijaondoa ndoto yake ya kuingia Ikulu.

“Sikushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa ajili ya kujaribu bahati yangu, bali nilikuwa na nia ya dhati ya kushinda urais na kuwatumikia wananchi,” alisema Balozi Amina.

“Sikushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa ajili ya kujaribu bahati yangu, bali nilikuwa na nia ya dhati ya kushinda urais na kuwatumikia wananchi,” alisema Balozi Amina.

“Nilitamani kweli niwe rais na niseme tu kwamba kwa kweli ndoto yangu hiyo haijafa, ingawa jambo hilo sasa litategemea muda, uhai, afya na mazingira yatakayojitokeza baada ya Rais Magufuli kumaliza muhula wake wa uongozi,” alisema.

Kwa mujibu wa utaratibu wa CCM, kada anayechaguliwa kuwa Rais hupitishwa tena kugombea urais baada ya kipindi chake cha miaka mitano kumalizika ili aongoze nchi kwa vipindi viwili.

Balozi Amina anasema safari yake ya kuelekea Ikulu ilikumbwa na vikwazo viwili, ambavyo alivitaja kuwa ni Watanzania kutokuwa tayari kuongozwa na mwanamke na pia mchakato wa uchaguzi kutawaliwa na wenye fedha.

Alisema bado jamii haijawa tayari kuamini kuwa mwanamke anaweza kuwa kiongozi wa juu wa ngazi kama ya urais, lakini anasema jitihada za CCM kwenye uchaguzi uliopita kumkubali mwanamke zinaweza kubadilisha mtazamo wa jamii.

“Mimi naona tatizo hilo limesababishwa na mambo mengi. Inaweza ikawa tatizo la elimu kwamba watu bado hawajaelewa vya kutosha kwamba mwanamke anaweza,” alisema.

“Lakini pia hili ni suala la mila na desturi. Kuna baadhi ya maeneo nchini mwanamke hachukuliwi kama ana mchango wowote katika maendeleo ya jamii. Lakini ninavyoona hali hii itakwisha na tumeanza kuimaliza baada ya kumpata Makamu wa Rais Mwanamke.”

Amina alibainisha kuwa mawazo kwamba mwanamke hawezi kuwa kiongozi ni potofu, ingawa na yametokana pia na ukweli kwamba baadhi ya wanawake hawajajitambua vya kutosha.

“Kuna uwezekano Tanzania ikaongozwa na mwanamke na watu waondoe mawazo kuwa mwanamke hafai kuwa kiongozi. Wanawake wana uwezo mzuri, ila wanachohitaji kutoka kwa jamii ni kuwaamini tu,” alisema.

Jambo jingine ni mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupitia CCM, na hasa nafasi ya Urais.

Alisema utaratibu unaotumika sasa kuanzia uchukuaji wa fomu mpaka uteuzi, unatengeneza makundi ya walionacho na wasionacho ndani ya chama hicho na hivyo kuwafanya baadhi ya wanachama kushindwa kukabiliana na ushindani.

“Chama kiimarishe process (mchakato) za kutafuta wadhamini, kiangalie upya mfumo na ikiwezekana turudi kwenye mfumo wa zamani wa kamati ya utendaji kuwachuja wagombea,” alisema Kuhusu mkakati wake endapo angepitishwa na baadaye kuchaguliwa kuwa Rais, Balozi Amina alisema alitaka wananchi wanufaike na kukua kwa uchumi.

“Nilitaka nitafsiri kukua kwa uchumi mifukoni mwa wananchi,” alisema.

Amina alisema haina maana kueleza kuwa uchumi wa nchi unakua wakati Watanzania bado wanaishi maisha ya umaskini na hicho ndicho kilikuwa kilio chake.

Alieleza wakati sera zikielekeza kuhusu viwanda na kilimo, dira yake ingekuwa kusimamia uboreshaji wa mazao ya kilimo na viwandani ili yaongezwe ubora kabla ya kuuzwa, kitu ambacho alisema kingesaidia kuongeza ajira kwa vijana.

“Nilitamani kuona kama tunazalisha mazao ya kilimo, tuyasindike kwanza kabla ya kuuza. Na bidhaa za viwandani hivyo hivyo ili tuongeze ubora na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaongeza ajira kwa vijana,” alisema.

Pia, alisema angesimamia ukusanyaji wa kodi kama inavyofanywa sasa na Serikali ya Rais Magufuli, lakini yeye asingeishia kusimamia makusanyo ya kodi inayoingia kupitia bandari pekee, bali angetafuta vyanzo mbadala vya uhakika vya kuongeza mapato ya Serikali.

“Kukusanya mapato bandarini ni sawa, lakini bandari si chanzo cha mapato cha kutegemea sana, kwani bidhaa zinaingia bandarini kama dunia haijachafuka. Ikitokea machafuko kwenye nchi ambazo zinatumia bandari zetu hatuwezi kupata mizigo ya kuitoza kodi. Kumbe ningetafuta vyanzo vingine vya uhakika zaidi vya mapato,” alisema.

Uchaguzi Mkuu ulikuwa huru na wa haki

Kuhusu tathmini ya uchaguzi, Balozi Amina alisema ulikuwa huru kwa vigezo vyote vya ndani na nje ya nchi.

“Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na hata Umoja wa Mataifa unatambua hilo. Pia waangalizi mbalimbali wa kimataifa walieleza kuwa uchaguzi ule haukuwa na shida,” alisema.

-

Alhamisi, 28 Januari 2016

Bungeni Ni Balaa tu

Ni mzobemzobe bungeni

Polisi 35 jana walitumika kuwatoa ukumbini wabunge kutoka vyama vya upinzani baada ya vurugu

Makachero na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge baada ya kuitwa na Mwenyekiti Andrew Chenge ili kuwatoa kwa nguvu wabunge wa upinzani kwa kukaidi amri ya kuwataka waende nje jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma. Polisi 35 jana walitumika kuwatoa ukumbini wabunge kutoka vyama vya upinzani baada ya vurugu kutokea ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria kutokana na tangazo la uamuzi wa Shirika la Utangazaji (TBC) kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge.

Wabunge wa upinzani walitolewa ukumbini wakiwa wamebebwa juu juu au mzobemzobe, wengine wakiwa wamechaniwa nguo na wengine kurushiana makonde na polisi katika tukio lililoweka taswira ya kwanza ya aina yake tangu kurejeshwa kwa siasa za vyama vingi mwaka 1992.

Waandishi wa habari waliokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge, walizuiwa kwanza kuchukua picha za matukio yaliyokuwa yakiendelea ukumbini hapo, na baadaye kuondolewa na kupelekwa kwenye chumba kingine na hivyo kushindwa kufanya vizuri kazi yao ya kuchukua habari.

Kabla ya purukushani hizo kuanza, asubuhi kituo cha televisheni cha TBC1 kilikatisha matangazo yake ya moja kwa moja mara baada ya Waziri wa Habari, Nape Nnauye kutangaza uamuzi wa chombo hicho kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge. Baadaye kituo cha televisheni cha Star TV nacho kikakatisha matangazo na hivyo kubakia Azam TV tu.

Lakini jioni, wakati mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akijiandaa kutangaza uamuzi wa kuwaondoa ukumbini wabunge wa Ukawa, mtangazaji wa Azam TV naye akatangaza kuwa kituo hicho kinakatisha matangazo hayo ya moja kwa moja.

Dalili za vurugu hizo zilianza kuonekana asubuhi wakati wabunge wa upinzani walipopinga kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa Novemba 20 wakati TBC ikiwa imezima matangazo ya moja kwa moja, wakidai wananchi wana haki ya kusikia kinachojadiliwa.

Hoja hiyo ilisababisha Chenge kuahirisha shughuli za Bunge kuipa nafasi Kamati ya Uongozi kujadili na kutolea uamuzi hoja ya mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ya kupinga mjadala wa hotuba ya Rais kutorushwa moja kwa moja na televisheni ya taifa.

Chenge aliahirisha shughuli hizo hadi saa 10:00 jioni wakati vurugu zilipoibuka.

Baada ya mvutano wa dakika 35 kati ya Chenge na wabunge wa upinzani kuhusu kanuni, vurugu hizo zililipuka saa 10:50 jioni.

Askari hao walitumia takriban dakika 25 kuwatoa wabunge hao ukumbini baada ya kuanza mzobemzobe huo saa 10:50 jioni na kuumaliza saa 11:15 jioni.

Wabunge hao walizua sintofahamu baada ya Chenge kueleza uamuzi wa Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana kujadili hoja iliyotolewa asubuhi na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo, Kigoma Mjini), kupinga kusitishwa kurushwa kwa matangazo hayo, kauli ambayo ilisababisha mwenyekiti huyo kuahirisha kikao hicho mpaka saa 10:00 jioni kutokana na shinikizo la wabunge wa upinzani.

Wakati wabunge wakibebwa juu juu na askari hao, ofisa habari wa Bunge, Owen Mwandumbya aliwataka waandishi wote wa habari kutofanya chochote, ikiwa pamoja na kupiga picha, na kuwataka watoke nje ya ukumbi wa Bunge hadi kwenye eneo maalumu lililokuwa na ulinzi wa askari.

Akieleza uamuzi wa kamati ya uongozi, Chenge alisema: “Kwanza kamati imesema mwenyekiti wa Bunge alikuwa sahihi kuahirisha Bunge, pili hakuna haki iliyovunjwa, tatu kamati imeagiza mjadala wa hotuba ya rais uendelee na nne endapo kuna mbunge hajaridhika ni haki yake  kutumia kanuni ya 5 (4) ya kanuni za Bunge ili kuwasilisha malalamiko yake kwa Katibu wa Bunge”.

Uamuzi huo uliwanyanyua wabunge wa upinzani. Safari hii mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliomba mwongozo wa suala hilo, akisema kuwa lilipaswa kutolewa uamuzi na mwenyekiti wa Bunge au Spika na  si kamati ya uongozi.

Katika hoja yake ya pili, Lissu alisema suala hilo ni la kikanuni na lilipaswa kutolewa ufafanuzi na Kamati ya Kanuni na si Kamati ya Uongozi, jambo ambalo lilipingwa na Chenge aliyesema kuwa kamati ya uongozi inaweza kujadili masuala ya kanuni.

Majibu ya Chenge yaliwanyanyua wabunge wote wa upinzani, huku Pauline Gekul (Babati Mjini) na John Heche (Tarime Vijijini) wakiomba mwongozo ambao Chenge alijibu kwa kurejea uamuzi wa Kamati ya Uongozi.

 Kutokana na wabunge hao kugoma kukaa huku wakipiga kelele, kujibiwa na wabunge wa CCM waliokuwa wakishangilia kwa mtindo wa kupiga meza, saa 10:50 jioni Chenge aliamuru askari wa Bunge kuwatoa wabunge hao.

Kabla ya uamuzi huo, Chenge aliamuru Lissu, Ester Bulaya (Bunda), Gekul na Godbles Lema (Arusha Mjini) kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa maelezo kuwa ndio walikuwa vinara wa vurugu hizo.

Hata hivyo, wabunge hao waligoma huku Lema akisimama na kuvua koti na tai, akisema kuwa hakuwa akizungumza chochote.

Baada ya Chenge kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, polisi wanane waliingia kuwatoa wabunge hao bila mafanikio, na kulazimika kuita polisi 18 waliokuwa wamevaa sare pamoja na wengine nane waliovaa kiraia.

Licha ya wingi wa askari hao ambao walizunguka eneo wanalokaa wabunge wa upinzani, walishindwa kuwatoa na kulazimika kuwaita askari tisa wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuongeza nguvu.

Wabunge kadhaa walitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge huku wakiwa wamebebwa juu juu na kuchaniwa nguo zao, kusababisha baadhi yao kurushiana makonde na askari hao.

Baada ya askari hao kufanikiwa kuwatoa nje, wabunge waliosalia ambao ni kutoka CCM waliendelea kujadili hotuba ya Rais, huku waandishi wa habari nao wakitakiwa kurejea ukumbini.

 

Kauli ya Ukawa

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi, Serikali ilibadili mjadala kutoka gharama za kurusha matangazo hayo na kuibuka na madai kuwa watumishi wa Serikali hawafanyi kazi kwa sababu ya kuangalia matangazo ya Bunge.

“Pia Serikali ilileta hoja kuwa wakati wa mchana wananchi hawatazami televisheni na usiku ndio wanakuwa na muda zaidi. Sisi tulipinga hoja hizo kwa kutambua kuwa huo ni mkakati maalumu wa Serikali na ulianza tangu wakati wa kampeni, sasa umefikia hatua ya kufungia vyombo vya habari,” alisema Mbowe.

“Walianza siku nyingi na hata kufikia hatua ya kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara. Uamuzi huu utawafanya wananchi kutosikiliza taarifa za Serikali.”

Alisema walirejea kwenye kikao cha Bunge jioni kwa nia ya kupinga uamuzi wa Serikali kuzuia matangazo hayo kwa lengo la kuijulisha dunia juu ya kinachofanywa na Serikali ya CCM.

“Watu wanafukuzwa kazi bila kufuata taratibu, mfano ni mabalozi waliotakiwa kurudi nyumbani haraka. Huku ni kujenga misingi ya udikteta katika taifa. Mawaziri nao wanafukuza watu hovyo, wakuu wa wilaya ya mikoa nao, halafu  sisi tunasema ni majipu?” alihoji Mbowe.

“Tunalaani Serikali ya Magufuli kwa kutozingatia uhuru wa wananchi kupata habari, uhuru wa Bunge kusikilizwa. Tutapaza sauti ndani na nje ya Bunge. Hatuwezi kuruhusu mambo haya kuonekana ni utaratibu wa kawaida.”

Alisema kuna taarifa kuwa Serikali inahofia kujadiliwa kwa suala la Zanzibar, yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu,“Tutaonyesha upande wa pili wa Serikali ya Magufuli,” alisema.

 Alisema vyombo vya dola vinatumika kuziba haki na uhuru wa wananchi, kama majeshi yanavyotumika kudhibiti wananchi baada yakufutwa kwa uchaguzi Zanzibar.

“Sasa tumeonyeshwa kuwa Bunge ni pamoja na FFU, polisi na mbwa. Tulichokitaka ni mjadala wa kutetea wananchi kupata habari. Chenge kakimbia kiti na kuacha Bunge kuongozwa na askari,” alisema Mbowe.

Alipoulizwa kama watashiriki katika kikao cha Bunge cha leo, Mbowe alisema: “Kesho (leo) tutaingia bungeni. Tambueni kuwa hata nyinyi (waandishi) mlifukuzwa. Ipo siku mtafukuzwa kabisa maana Serikali haitaki kuambiwa ukweli. Serikali ikifanya jema tutawapongeza, isipofanya jema tutasema.”

Alisema kuna wabunge wameumizwa kwa kipigo, kuibiwa saa, pochi na simu.

“Bunge kuendelea ni unafiki wa wabunge wa CCM. Asubuhi wakati tunashinikiza Bunge lijadili hoja hii, wabunge wa CCM walituandikia vikaratasi kutuunga mkono ila jioni wametugeuka,” alisema.

Baadhi ya waandishi waliojiwa na Mwananchi baada ya sakata hilo walisema inasikitisha kuona wanafanyiwa vitendo hivyo.

 

Kauli za wanahabari

Mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Elias Msuya alisema: “Ni jambo la kusikitisha maana tumepewa vitambulisho kwa ajili ya kuandika habari za Bunge, lakini leo hii tunafukuzwa. Imeniuma sana.”

 Kwa upande wake mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Ibrahim Yamola ambaye aliporwa simu yake na askari baada ya kupiga picha, alisema: “Ni tukio la kusikitisha, ni kama tulizuiwa kufanya kazi yetu.”

Wakati huo huo, msemaji wa Bunge, Owen Mwandumbya amesema kuwa waandishi wa habari saba watarudishwa na hawataruhusiwa kuripoti habari za Bunge kwa kile kilichoelezwa kukiuka kanuni na taratibu za Bunge.

Hata hivyo, hakuwataja moja kwa moja waandishi hao wa habari na kusema sababu kubwa ni kugoma kutii maagizo ya kutotakiwa kwenye baadhi ya maeneo ya Bunge na zaidi wakati wa vurugu hizo.     

-