Tekno ameungana na Alikiba, Davido na wengine kama mwanafamilia mpya wa label ya Sony Music.
Hitmaker huyo wa Pana, amesaini dili hilo wiki hii mbele ya promota maarufu wa Nigeria, Paulo O wa kampuni ya Upfront & Personal ambaye alipost video ya utiaji saini huo uliofanyika kwenye ofisi yake.
Miaka ya hivi karibuni, Tekno amegeuka kuwa hitmaker maarufu kutoka Afrika, huku nyimbo zake zikiwashika hadi wasanii wakubwa wa Marekani.
Tekno alitumbuiza kwenye tamasha la Fiesta, Novemba 5 jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni