Alhamisi, 13 Aprili 2017

Wayne Rooney Kuondoka Man Utd Mwisho wa Msimu

Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney.

Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ndiye aliyevujisha siri, kwamba Rooney hana raha na anaona ni wakati mwafaka kwake kuondoka Old Trafford kwa kuwa hapati nafasi ya kucheza.

Kocha Jose Mourinho anaonyesha kutomuweka Rooney kama chaguo la kwanza lakini mara kadhaa, naye amekuwa akiumia.

Rooney ambaye amecheza Man United kwa miaka 13 tokea alipojiunga nayo akiwa kinda kutoka Everton, amekuwa akiandamwa na mamumivu ambayo pia yamechangia akose mechi kadhaa.

Imeelezwa, hana uhakika pia kucheza mechi ijayo ya Man United ambayo itakuwa ya Europa League dhidi ya Anderlecht na itapigwa nchini Ubelgiji, Ahamisi.

Club Ya Simba Yapewa Pointi 3 Baada ya Kushinda Rufaa


KLABU ya Simba imezidi kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar ambao imethibitika mbele ya Kamati ya Saa 72 kuwa mchezaji wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi alicheza mechi ya Simba akiwa na kadi tatu.

Simba ilikata rufaa ikitaka ipewe pointi tatu kwa kuwa Kagera Sugar ilimchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano. Katika mechi hiyo, Simba ililala kwa mabao 2-1 na baada ya hapo, ikatangaza kutangaza kukata rufaa.

Kulingana na kanuni za TFF, Kamati hiyo imeipa Simba point zake 3 na magoli mawili baada ya kushinda rufaa yao hiyo dhidi ya Kagera Sugar. Simba imefikisha pointi 61 mbele ya wapinzani wao Yanga wenye Pointi 56.

HAWA NDO MARAIS NA WAFALME WALIOCHAGAULIWA WAKIWA NA UMRI MDOGO ZAIDI

Katiba za nchi mbalimbali zimeweka wazi umri unaofaa kwa mtu kugombea nafasi ya uongozi hasa Rais ingawa kiwango hicho hutofautiana kulingana na nchi; kwa mfano, Tanzania mgombea wa Urais lazima aanzie miaka 40 na kuendelea.

Zipo pia nchi nyingine ambazo kigezo cha umri sio muhimu sana kumfanya mtu agombee nafasi hiyo na wakati mwingine nafasi hiyo hurithiwa…sasa leo April 13 nimekutana na list ya Maraisi waliowahi kuchaguliwa wakiwa na umri mdogo duniani hadi kufikia 2017 ambapo Rais sasa wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa ndiye Rais mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa.

1: Kim Jong Un 

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Unanashikilia rekodi ya kuwa Rais mdogo zaidi kuwahi kuchaguliwa duniani ambapo aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 26 mwaka 2011 akirithi kiti cha baba yake Kim Jong Il. Sasa Rais Kim ana umri wa miaka 33.

2: Tamim Bin Hamad 

Ni Rais wa Qatar ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 30. Tamim Bin Hamadana umri wa miaka 35 kwa sasa akikamata nafasi ya pili kuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi duniani.

3: Jigme khesar

Huyu ni Mfalme wa Bhutan, nchi ndogo katika Bara la Asia inayopakana na China na India. Mfalme wa nchi hii ndiye kiongozi mdogo zaidi kuwahi kuteuliwa wakati anaanza uongozi wake. Jigme khesar aliteuliwa kuwa Mfalme wa nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 25 mwaka 2006. Sasa ana umri wa miaka 37.

4: Atifete Jahjaga

Atifete Jahjaga anashikilia rekodi ya kuwa Rais mdogo mwanamke kuwahi kuchaguliwa duniani. Jahjaga alikuwa Rais wa Kosovo kuanzia April 2011 akiwa na umri wa miaka 35 na kumaliza muda wake mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 40.

5: Andrzej Sebastian Duda

Andrzej Duda ni Rais wa sita wa Polandambaye alichaguliwa mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 42. Kabla ya kuwa Rais wa nchini alikuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya.

6: Joseph Kabila 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila alichaguliwa mwaka 2001 siku kumi baada ya kifo cha baba yake Laurent Kabila wakati huo akiwa na umri wa miaka 28. Joseph Kabila ana umri wa miaka 45 kwa sasa.