Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Michezo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Michezo. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 13 Aprili 2017

Wayne Rooney Kuondoka Man Utd Mwisho wa Msimu

Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney.

Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ndiye aliyevujisha siri, kwamba Rooney hana raha na anaona ni wakati mwafaka kwake kuondoka Old Trafford kwa kuwa hapati nafasi ya kucheza.

Kocha Jose Mourinho anaonyesha kutomuweka Rooney kama chaguo la kwanza lakini mara kadhaa, naye amekuwa akiumia.

Rooney ambaye amecheza Man United kwa miaka 13 tokea alipojiunga nayo akiwa kinda kutoka Everton, amekuwa akiandamwa na mamumivu ambayo pia yamechangia akose mechi kadhaa.

Imeelezwa, hana uhakika pia kucheza mechi ijayo ya Man United ambayo itakuwa ya Europa League dhidi ya Anderlecht na itapigwa nchini Ubelgiji, Ahamisi.

Club Ya Simba Yapewa Pointi 3 Baada ya Kushinda Rufaa


KLABU ya Simba imezidi kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kushinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar ambao imethibitika mbele ya Kamati ya Saa 72 kuwa mchezaji wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi alicheza mechi ya Simba akiwa na kadi tatu.

Simba ilikata rufaa ikitaka ipewe pointi tatu kwa kuwa Kagera Sugar ilimchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano. Katika mechi hiyo, Simba ililala kwa mabao 2-1 na baada ya hapo, ikatangaza kutangaza kukata rufaa.

Kulingana na kanuni za TFF, Kamati hiyo imeipa Simba point zake 3 na magoli mawili baada ya kushinda rufaa yao hiyo dhidi ya Kagera Sugar. Simba imefikisha pointi 61 mbele ya wapinzani wao Yanga wenye Pointi 56.

Alhamisi, 30 Juni 2016

Ibrahimovic Huyoo Man United

ImageAFPImageIbrahimovic hakufunga bao hata moja Euro 2016

Mshambuliaji nyota kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovicn amethibitisha kwamba atajiunga na klabu ya Manchester United.

Amethibitisha hayo kupitia mitandao ya kijamii.

"Ningependa kuufahamisha ulimwengu. Kwamba ninaelekea Manchester United," ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada yake kuondoka Paris St-Germain.

Anatarajiwa kutia saini mkataba wa mwaka mmoja Old Trafford.

Ibrahimovic atakuwa mchezaji wa pili kununuliwa na meneja mpya wa United Jose Mourinho, aliyemrithi Louis van Gaal mwezi Mei.

Beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 22, alikuwa wa kwanza kununuliwa.

United walilipa £30m kumchukua kutoka Villarreal ya Uhispania.

United pia wanaendelea kumuwinda Henrikh Mkhitaryan, 27, raia wa Armenia anayechezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

ImageEPA

Ibrahimovic aliongoza ufungajji mabao Ligue 1 msimu uliopita, akifunga mabao 38.

Hata hivyo, hakuweza kufaa sana taifa lake la Sweden ambalo liliondolewa michuano ya Euro 2016 hatua ya makundi. Ibra hakufunga hata bao moja.

Jumatano, 15 Juni 2016

Ufaransa Yatinga hatua ya 16 bora Euro

HABARI

POSTED 2 HOURS AGO

Ufaransa yatinga 16 bora ya Euro

By Mwandishi wetu, Mwananchi

IN SUMMARY

Katika mchezo huo wa awali wa kundi A uliofanyika katika Uwanja wa Stade Velodrome mjini Marseille, mabao ya wenyeji yalifungwa na Antoine Griezmann and Dimitri Payet.

Paris, Ufaransa. Timu ya soka ya Ufaransa imekuwa ya kwanza kutinga katika hatua ya mtoano wa michuano ya mataifa ya Ulaya (Euro 2016) itakayokuwa na timu 16, baada ya kuitungua Albania mabao 2-0.

 Katika mchezo huo wa awali wa kundi A uliofanyika katika Uwanja wa Stade Velodrome mjini Marseille, mabao ya wenyeji yalifungwa na Antoine Griezmann and Dimitri Payet.

 Kutokana na ushindi huo Ufaransa imefikisha pointi sita katika michezo miwili iliyocheza.

 Mchezo mwingine wa kundi hilo uliopigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes ulishuhudia Uswisi ikitoka sare ya 1-1 na Romania. Matokeo hayo yameifanya Romania ifikishe pointi sita wakati Uswisi ina moja mkononi.

 Kipute kingine kilikuwa kati ya Slovakia na Russia ambacho kilishuhudia Russia ikitoka ulimi nje kwa kubugia mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade Pierre-Mauroy mjini Lille.

Jumanne, 14 Juni 2016

Brazil Yamtimua kocha wake, Carlos Dunga


Brazil imemtimua kocha wao Carlos Dunga baada ya kikosi hicho kushindwa hata kuingia hatua ya mtoano ya michuano ya Copa America kufuatia nchi hiyo kutupwa nje na Peru..

Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, limetoa taarifa ya kumtimua Dunga ambaye pia alitarajiwa kuiongoza Nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ambayo itachezwa nchini Brazil mwezi Agosti.

Pamoja na Dunga, pia Wasaidizi wake wote wa Benchi la Ufundi wameondolewa, na CBF imesema itateua Watu wengine kuingoza Timu hiyo.

Brazil ilifungwa 1-0 na Peru, Goli linaloelezwa kuwa la mkono, na kutupwa nje ikiwa ni mara yao ya pili tu katika Historia ya Miaka 100 ya Mashindano hayo kushindwa kuvuka hatua ya Makundi.

Dunga, ambae alikuwa nahodha wa Brazil Mwaka 1994 walipobeba Kombe la Dunia, aliteuliwa kuwa Kocha wa Brazil mara baada ya Nchi hiyo kutolewa kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zilizochezwa kwao Brazil.

Lakini tangu atwae wadhifa huo, ikiwa ni mara yake ya pili kuwa Kocha wa Brazil, Nchi hiyo haijafanya vyema na kutolewa Nusu Fainali ya Copa America ya 2015 kwa Penati na Paraguay ambayo ilifanyika nchini Chile

Jumanne, 7 Juni 2016

Check Hapa Mfululizo wa Maisha Ya Muhammad Ali >>>>>

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha zinazosimulia matukio muhimu katika maisha ya Muhammad Ali, bingwa wa ndondi na mwanamichezo mashuhuri.

OTHER

Muhammad Ali alizaliwa na kupewa jina Cassius Marcellus Clay mjini Louisville, kentucky mnamo 17 Januari 1942. Alianza kucheza ndondi akiwa na umri wa miaka 12 na baadaye akaishia kushinda dhahabu katika uzani wa light-heavyweight Michezo ya Olimpiki ya Roma mwaka 1960.

OTHER

Ali alianza kucheza ndondi ya kulipwa Oktoba 1960 akiwa na umri wa miaka 18 na akashinda mara 18 mfululizo kabla ya kusafiri kwenda London Juni 1963 kwa pambano lake la kwanza la kulipwa ng'ambo. Alibashiri kwamba angemshinda bingwa wa Uingereza henry Cooper kupitia knockout raundi ya tano.

OTHER

Cooper alimbwaga Ali raundi ya nne lakini Mmarekani Ali alitimiza ubashiri wake kwa kumshinda raundi ya tano mbele ya watazamani 55,000 uwanja wa Wembley.

OTHER

Ali alijaribu kupigania taji la ubingwa duniani februari 1964 alipokabiliana na bingwa wa dunia Sonny Liston. Liston alisema: "Nafikiri nitampiga vibaya sana kijana huyo."

OTHER

Alidunishwa na wataalamu wengi wa masumbwi kabla ya pambano hilo lakini Ali alicheza kwa ustadi mkubwa Miami na kumlazimisha Liston kusalimu amri kabla ya raundi ya sita. Ali alitawazwa bingwa wa dunia uzani wa heavyweight akiwa na umri wa miaka 22.

OTHER

Ushindi wa Ali dhidi ya Liston ulikuwa, na bado ni, moja ya matokeo ya kushangaza zaidi katika historia ya ndondi. Ali alijisifu: "Mimi ndiye bingwa zaidi! Mimi ndiye bora zaidi! Mimi ni mfalme wa dunia!".

OTHER

Ali, alitangaza kujiunga na kundi la Nation of Islam na akaacha kutumia majina yake ya awali na kuwa Muhammad Ali baada ya pambano hilo dhidi ya Liston. Alitetea ubingwa wake dhidi ya Liston mjini Lewiston, Maine mwezi mei 1965.

OTHER

Ali alishinda Liston baada ya kumpiga knock-out dakika ya kwanza ya raundi ya kwanza. Hadi wa leo, wengi wanaamini Liston aliuza pambano hilo, lakini Ali amesisitiza kwamba alishinda kwa njia safi.

OTHER

Novemba 1965, Ali alitetea taji lake dhidi ya bingwa wa zamani Floyd Patterson akishinda kwenye raundi ya 12. Patterson alikuwa amemshambulia sana Ali kuhusu msimamo wake kisiasa na kidini.

OTHER

Ali alirejea London kupigana na Henry Cooper kwa mara ya pili Mei 1966 katika uwanja wa zamani wa Arsenal wa Highbury. Mashabikji wake Uingereza, ambao hawakuwa wamemtambua mara ya kwanza, walimshabikia sana.

OTHER

Angelo Dundee, anayeonekana hapa akifunga mikono ya Ali kabla yake kupambana na Cooper, alikuwa akimsaidia Ali tangu alipoanza kucheza ndondi. "Kuna Cassius Clay mmoja," alisema Dundee. "Namshukuru Mungu."

OTHER

Ali alimshinda Cooper baada ya raundi sita na kumuumiza vibaya karibu na jicho lake la kushoto. Baada ya kifo cha Cooper 2011, Ali alisema: "Nitamkosa sana rafikin yangu wa zamani - alikuwa mpiganaji hodari na mwanamume muungwana."

OTHER

Ali alitetea taji lake mara ya nane dhidi ya Ernie Terell Februari 1967. Ali alimchezea Terrel ambaye alikuwa ametumia jina lake la kuzaliwa kumrejelea yeye kabla ya mechi, kwa raundi 15. Kila mara alikuwa akimwuliza: "Jina langu ni nani, Mjomba Tom?"

OTHER

Baada ya kutetea taji lake tena mara nyingine dhidi ya Zora Folley, Ali alipokonywa taji lake baada ya kukataa kujiunga na jeshi la Marekani lililokuwa likipigana vita Vietnam. Ilikuwa ni miaka mitatu baadaye aliporejea ulingoni tena.

OTHER

Ali alishindwa mara ya kwanza na bingwa mpya wa dunia Joe Frazier katika Madison Square Garden mwezi Machi 1971. Pambano hilo hujulikana tu kama "The Fight" yaani Pambano Lenyewe. Ilikuwa mara ya kwanza kwa mabingwa wawili wa dunia wa heavyweight ambao hawakuwa wameshindwa kukutana ulingoni.

OTHER

Ali alishinda marudio ya pambano hilo dhidi ya Frazier ingawa pambano lake linalosifika sana lilijiri baadaye 1974 alipopigana na George Foreman katika pambano linalojulikana kama "Rumble in the Jungle" maana yake "Mngurumo Msituni". Ali alikaa raundi nane za kwanza akiwa amejibanza kwenye kamba, mbinu aliyoiita 'rope-a-dope'.

OTHER

Lakini alichomoka raundi ya nane na kumwangusha Foreman kwa ngumi kali na kuwa mwanamume wa pili kutwaa tena ubingwa wa heavyweight, akiwa na umri wa miaka 32.

OTHER

Ali alimshinda Mwingereza Joe Bugner mjini Kuala Limpur, malysia Juni 1975. Miezi minne baadaye, Ali alipata ushindi mwingine dhidi ya hasimu wake mkuu Frazier katika pambano la 'Thrilla in Manila'. Ali baadaye alisema lilikuwa jambo la kukaribia kifo zaidi alilowahi kuhisi.

OTHER

Ali alipoteza taji lake kwa Leon Spinks 1978 kabla ya kulitwaa tena kwa mara ya tatu baadaye mwaka huo. Alitangaza kustaafu kwake miezi tisa baadaye. Lakini alirejea 1980 na kupigana na bingwa mpya Larry Holmes.

OTHER

Baada ya kushindwa an Holmes, Ali alipigana pambano moja, dhidi ya Trevor Berbick ambapo alishindwa kabla ya kustaafu kabisa akiwa na umri wa miaka 40. Kuondoka kwake kuliacha pengo katika tasnia ya ndondi, lililojazwa tu na kufika kwa Mike Tyson katikati mwa miaka ya 1980.

OTHER

Ali aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa Parkinson (ugonjwa wa kutetemeka) mwaka 1984 lakini alikabiliana na hali hiyo kwa ujasiri na staha. Mwaka 1996, alitazamwa na ambilioni ya watu akiwasha mwenye wa Olimpiki mjini Atlanta.

OTHER

Atlanta pia, alipewa tena nishani yake ya dhahabu kutoka kwa Michezo ya Olimpiki ya 1960. Ali alidai aliirusha nishani tyake ya kwanza Mto Ohio baada ya kukosa kuhudumiwa katika mgahawa wa Wazungu pekee, ingawa wengi hutilia shaka hilo.

OTHER

Wakati wa kufunga karne, Ali alijizolea sifa tele. Watazamaji wa BBC walimpigia kura kuwa Mchezaji Bora zaidi wa Karne, mwaka ambao bondia wa Uingereza Lennoz Lewis alishinda tuzo kuu.

OTHER

Bintiye Ali, laila alianza kucheza ndondi akwia na umri wa miaka 15 na akaanza kucheza ndondi ya kulipwa 1999 kabla ya kumshinda bintiye Frazier, jackie Frazier-Lyde mwaka 2001. Laila alishinda taji la super-middleweight mwaka 2002 kabla ya kustaafu 2007.

OTHER

Mwaka 2001, filamu kuhusu maisha ya Ali ilitolewa, Ali akiigizwa na Will Smith. Ali aliendelea kusifika kote duniani, licha ya afya yake kudorora.

OTHER

Baada ya kutimiza umri wa miaka 70, afya yake ilidhoofika zaidi. "Nafikiri kuugua kwangu ugonjwa wa Parkinson ni njia ya Mungu kunikumbusha ni nini cha muhimu zaidi," ndivyo alivyosema. Amefariki akiwa na umri wa miaka 74.

Jumanne, 9 Februari 2016

Liverpool 'OUT' Michuano ya FA

ImageGettyImageRaha ya mechi bao, wachezaji wa West Ham United wakishangilia

Wagonga nyundo wa London West Ham United imewatupa nje majogoo wa Anfield Liverpool katika mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA.

West Ham walianza kuandika bao lao la kwanza kupitia kwa Michail Antonio katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza baada ya kunganisha krosi nzuri Enner Valencia's

Liverpool wakachomoa bao hilo kupitia kwa kiungo Philippe Coutinho aliyepiga mpira wa adhabu na kujaa nyavuni moja kwa moja.

ImageGettyImageWest Ham sasa watakutana na Blackburn raundi ijayo

Dakika tisini zikamalizika kwa sare ya bao 1-1, katika dakika 30, za nyongeza West Ham wakapata bao kupita kwa Angelo Ogbonna,

West Ham watawavaa Blackburn ugenini katika mchezo wa raundi ya tano ya michuano hiyo hapo Februari 21.

Jumatatu, 8 Februari 2016

Wenger:Arsenal Itaichakaza Leicester Jumapili

JUMAPILI

By Meshack Brighton

19:24ENGLISH FOOTBALLSHARE

0

Getty

Arsene Wenger anaamini Arsenal yake ina uwezo wa kutosha kuwapiga vinara wa Ligi Kuu Leicester City Jumapili ijayo

Washika mtutu wa London wapo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya ushindi mwepesi dhidi ya Bournemouth. Magoli kutoka kwa Mesut Ozil na Alex Oxlade-Chamberlain yaliyopishana kwa muda wa sekunde 88 – kuhitimisha mwenda wa Arsenal wa saa tano na nusu bila ya goli.

 “[Kuifunga Bournemouth] ni vizuri sana kwa ajili ya mustakabali kwani sasa tuna mechi kubwa nyumbani dhidi ya Leicester ambao wana nafasi kubwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu,” Wenger alikiambia Arsenal.com. “Ushindi kwa namna Fulani unakuweka katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo unaofuata.

“Tuna wiki moja ya kujiandaa na mchezo huo na ninautafakari sana. Leicester ni timu imara lakini nasi tupo imara pia. Nyumbani tukiwa na mashabiki wetu tutawafunga tu.”

Mfaransa huyo aliwamwagia misifa Chamberlain na Gabriel kwa kushiriki kuwezesha ushindi kupatikana Jumapili.

 “Oxlade-Chamberlain ana nguvu, mbinu na mwenye uwezo wa kufunga magoli lakini anaweza kutengeneza nafasi pia,” aliongeza Wenger. “Mara nyingi hana bahati [na mashuti yake] lakini nadhani hilo litamshawishi kujaribu Zaidi na Zaidi.

“Gabriel amefanya vizuri. Ameonyesha kiwango safi na kwa ujumla nadhani anazidi kujiamini kadiri anavyocheza mechi nyingi, jambo linalofurahisha.”

 

Zouma Kukaa Nje Miezi 6

ImageReuters

Beki wa klabu ya Chelsea Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia goti kwenye mchezo dhidi ya Manchester United.

Zouma, atafanyiwa upasuaji kwenye kwenye goti lake ambalo aliumia Jumapili uwanjani Stamford Bridge baada ya kutua vibaya aliporuka kupiga mpira kwa kichwa.

Uchunguzi umethibitisha kwamba aliumia vibaya na hivyo anapaswa kufanyiwa upasuaji kutibu tatizo hilo.

Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL

Kawaida, Mchezaji akipata majeruhi ya aina hii, basi huwa nje ya uwanja si chini ya Miezi hivyo mchezaji huyu atakosa michezo yote ya msimu uliobaki.

ImageReutersImageZouma alionekana kuhisi uchungu mwingi baada ya kuanguka

Zouma, ambaye amekuwa kama pacha wa John Terry uwanjani, ameichezea Chelsea mechi 32 msimu huu.

Ameshaichezea Ufaransa mechi 2 za Kimataifa.

Cristiano Ronaldo:Nataka kubaki RealMadrid

ImageGettyImageCristiano Ronaldo

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema hataki kuondoka klabuni hapo kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka 2018.

Mreno huyo mwenye miaka 31 amekua akihusishwa na kurudi kujiunga na timu yake ya zamani ya Manchester United, ambayo ilimuuza mwaka 2008 au Paris St-Germain, ya Ufaransa.

"Nataka kubakia hapa kwa miaka miwili zaidi, miaka miwili ninayozungumzia itanichukua mpaka mwisho wa maktaba wangu, "alinukuliwa mchezaji huyo.

Ronaldo alizungumza hayo wakati ya ghafla ya uchukuaji tuzo ya Pichichi, amabpo alishinda tuzo hiyo baada ya kuwa mfungaji bora mismu uliopita kwa kufunga mabao 48.

"Hii ni ligi bora duniani, japo kuwa pia nimecheza ligi ya England, ni ligi ya ushindani na inawachezaji wazuri."

Alhamisi, 4 Februari 2016

Jose Mourinho Huyoo OldTrafford

TRAFFORD

By Meshack Brighton

18:33TRANSFER ZONESHARE

0

Getty Images

Michael Owen alikaririwa akisema kuwa Mauricio Pochettino ndiye anayefaa kuwa kocha wa Manchester United lakini tetesi zinadai Jose Mourinho anakaribia kutua Old Trafford

Kuna taarifa zilizozagaa leo katika vyombo vya habari barani Ulaya kuwa kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho anakaribia kukubali na kusaini mkataba wa kuwa meneja wa Manchester United kwa msimu wa 2016/2017.

Mtandao wa habari wa Sky Sport Italia umethibitisha kuwepo kwa taarifa hizo.

Mreno huyo anayesemwa kuwa moja kati ya makocha bora na wenye mafanikio makubwa barani Ulaya amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na‘mashetani wekundu’ Manchester United tangu atimuliwe kibaruani na klabu ya Chelsea.

Taarifa zinaeleza zaidi kuwa Mourinho ameamua uamuzi huo wa kujiunga na Manchester United siku chache baada ya klabu ya Manchester City kutangaza ujio wa kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola.

Mourinho ambaye alikuwa na uhasimu mkubwa sana na Guardiola walipokuwa wote katika ligi kuu ya Hispania, La Liga kama atafanikiwa kujiunga na Manchester United basi watafanikiwa kurejesha uhasimu wao kwa mara nyingine tena.

Kwa sasa klabu ya Manchester United ipo nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ikiwa na pointi 40 nyuma ya Arsenal iliyopo nafasi ya 4 kwa jumla ya pointi 45.

Arsene Wenger Amekubali Yaishe Kuhusu Ubingwa EPL

ARSENE WENGER ASALIMU AMRI ARSENAL

By Meshack Brighton

04:15PREMIER LEAGUESHARE

0

Getty Images

Arsene Wenger amekiri ni za haki na za kweli hukumu za EPL baada ya kulazimishwa sare tasa na Southampton Emirates na tumaini la ubingwa halipo tena

Kama ilikuwa imepangwa vile, wameshindwa kufunga mechi ya tatu mfululizo katika mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Barclays na sare ya nyumbani ya 0-0 dhidi ya Southampton imeitupa Arsenal mbali kabisa katika mbio za ubingwa.

Arsenal wana pengo la pointi tano kutoka kwa vinara wa ligi Leicester na pointi tatu nyuma ya Manchester City wakikaribia kufikiwa na Tottenham wanaoshika nafasi ya nne.

Je! hali ni ile ile ya siku zote na hadithi zile zile za Profesa Wenger?

Arsene Wenger amekubali kuwa klabu yake ipo kwenye wakati mgumu katika mbio za ubingwa wa Ligi ya Uingereza kwa sasa.

Katika mahojiano na Daily Mail Arsene Wenger alinukuliwa akisema maneno haya kufuatia mwendo mbovu wa timu yake katika mechi tatu mfululizo.

“Tutaona mwisho wa msimu huu. Ni mapema sana kusema chochote”.

“Ni dhahiri tumekuwa na msimu mbaya hasa kuanzia ile mechi ya kwanza dhidi ya Liverpool na ile mechi dhidi ya Stoke ambayo kimsingi tumekuwa na tofauti kubwa sana katika michezo yetu miwili”, alisema Wenger.

 Pia kuhusu usajili wa mshambuliaji bora katika umaliziaji Arsene Wenger amekuwa akijitetea mara kwa mara na kusema kuwa hakuna washambuliaji bora sokoni kwa sasa ambao wanaweza kuimarisha safu aliyo nayo.

Amesema washambuliaji hawatafutwi mtaani bali kila mshambuliaji mkubwa yupo kwenye timu yake na ana mkataba.

"Huwezi tu kupita mtaani ukaanza kutafuta mshambuliaji."

"Wala huwezi kupata mshambuliaji atakayekwambia nipo hapa njoo unisajili."

Hayo ndiyo maneno ya Wenger, ni dhahiri ameona maji yamefika shingoni na hakuna ujanja anaweza kufanya.

Jumatano, 3 Februari 2016

Samatta Ameiokoa Simba

Samatta aikomboa Simba, aijengea uwanja

SIMBA sasa wamekaa mkao wa kula, kwani mwaka huu ni wa neema kwao. Kwanza watapata mgawo wa

Mbwana Samatta     

ADVERTISEMENT

SIMBA sasa wamekaa mkao wa kula, kwani mwaka huu ni wa neema kwao. Kwanza watapata mgawo wa asilimia 20 za mauzo ya straika wao wa zamani, Mbwana Samatta ambaye ameuzwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe, pili wanasubiri kulipwa Dola 300,000 zaidi ya Sh 600 milioni ambazo wanaidai Etoile due Sahel ya Tunisia.

Katika mkataba wa Mazembe walipokuwa wanamnunua mchezaji huyo akitokea Simba uliwataka kuwapa Simba asilimia hizo watakapomuuza klabu nyingine jambo ambalo limetimia na wanatarajia kupokea Sh 349 milioni kutoka kwenye mauzo ya Dola 800,000 ambazo mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi amepewa na Genk huku Samatta akikunja fedha ndefu.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) liliiamuru Etoile kuilipa Simba ndani ya siku 60 ambazo zinakaribia kumalizika na Simba wamegoma kulipwa nusu nusu, wanataka pesa yao ilipwe kwa wakati mmoja na Etoile wakishindwa kuilipa Simba watakumbana na adhabu ya kushushwa daraja. Hivyo pesa hizo zikilipwa na zile za Samatta basi tatizo la ukata kwao litapungua.

Etoile walimnunua Emmanuel Okwi lakini hawakulipa hata shilingi na baadaye kuachana naye na Simba kulazimika kufungua kesi hiyo ya madai.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kuwa kwasasa wanasubiri kupata mgawo wao huo na wamepanga pesa hizo kuzipeleka kwenye ujenzi wa uwanja wao uliopo Bunju B ambao utaanza kujengwa hivi karibuni. Kwa makadirio uwanja wa mazoezi na uzio wa nyavu unaweza kutumia Sh 150 milioni hivyo pesa hiyo itatosha kukamilisha ujenzi huo.

“Tunasubiri meneja wa Samatta arudi maana amekwenda Lubumbashi, ndipo tujue mgawo wetu tunapataje, ila tumepanga kuipeleka pesa hiyo kwenye ujenzi wa uwanja mzuri kabisa, fedha za Okwi bado hawajatulipa tunasubiri, muda waliopewa haujaisha, hatutaki kulipwa nusu tunahitaji fedha,’’ alisema Aveva.