Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Biashara. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Biashara. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 27 Januari 2016

Toyota Yaongoza kwa Mauzo Duniani

ImageReutersImageKampuni ya magari ya Toyota

Toyota inaendelea kuongoza kama kampuni inayotengeza magari kwa mwaka wa nne mfululizo.

Kampuni hiyo iliuza magari milioni 10.15 kwa jumla mwaka 2015 na kuvunja rekodi ya matarajio ya wengi.

Kampuni ya Ujerumani ya Volkswagen imekuwa ya pili ikiwa imeuza magari milioni 9.93,ikifuatiwa na General Motors kutoka Marekani iliouza magari milioni 9.8.

Volkswagen ilikuwa inaongoza nusu ya mwaka wa 2015 kabla ya kashfa ya magari yake kutoa moshi mchafu kupunguza mauzo yake.

Biashara katika masoko makubwa kama vile Marekani na Japan na masoko yanayoinuka imepungua kutokana na kuanguka kwa uchumi duniani.

ImageAFPImageToyota

Mwaka 2014,Toyota iliibuka kidedea kwa kuuza magari milioni 10.23.

Kampuni hiyo imepata sifa kwa magari yake aina ya Prius hybrid,Camry,Corolla Sedan na Lexus.

Mauzo Ya Simu Za iphone Yapungua Duniani

ImageGettyImageMauzo ya simu ya Iphone yapungua

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple imeripoti kupungua kwa mauzo ya simu za iPhone katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho mwaka uliopita.

Kampuni hiyo iliuza simu milioni 75 mwaka uliopita ikiwa ni mauzo ya chini zaidi tangu mwaka 2007.

Hii ni kutokana na kuyumba kwa uchumi wa China.

Hata hivyo faida ya kampuni ya Apple iliongezeka katika kipindi hicho kwa zaidi ya dola bilioni 18.

Mhariri wa masuala ya Teknolojia katika mtandao wa CNET Ian Sherr, amesema huenda soko la simu za mkononi limefurika.