Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Teknolojia. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Teknolojia. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 11 Februari 2016

Magari Yanayojiendesha Kuruhusiwa Barabarani

ImageGoogleImageGari linalojiendesha

Mfumo wa magari ya kujiendesha wa kampuni ya Google hivi karibuni huenda ukaidhinishwa na kuwa sawa na gari linaloendeshwa na dereva ,na hivyobasi kutoa fursa kwa magari yasio na usukani ama hata vikanyagio kuwa barabarani.

Shirika la usimamizi wa barabara kuu nchini Marekani ,ambalo hubuni sheria na utaratibu katika barabara za Marekani lilitoa wazo lake katika barua kwa kampuni ya Google uliowekwa wazi wiki hii.

Hadi kufikia sasa ,gari lolote lisilo na dereva halikuweza kuidhinishwa kama linaloweza kuendeshwa barabarani.

Lakini kutokana na maendeleo ya kiteknolojia,shirika hilo limebadili maono yake.

''Iwapo hakuna binaadamu aliye ndani anaweza kuliendesha gari hilo, ni rahisi sana kumtambua dereva kama chochote badala ya yeyote anayeliendesha gari,''lilisema.

ImageGettyImageGari la google linalojiendesha

Hii inamaanisha kwamba teknolojia ya gari la kujiendesha ,ambayo haina udhibiti wa gari hilo kama katika magari mengine ni hatua moja muhimu ya kuruhusiwa katika barabara za hadhara.

Huku Shirika hilo likitoa baraka zake kwa gari hilo ,gari hilo sasa limeafiki mahitaji ya usalama wa magari nchini humo.

Alhamisi, 4 Februari 2016

Mambo Matano ambao hujui kuhusu Teknolojia

Habari tano za teknolojia ambazo hazifai kukupita

3 Februari 2016

Mshirikishe mwenzako

Teknolojia hubadilika mara kwa mara na kila siku kuna mambo mapya yanayovumbuliwa na mitindo pia kubadilika.

Hapa, kuna makala tano kuhusu teknolojia ambazo hazifai kukupita.

1. Li-fi ina kasi mara 100 zaidi ya Wi-fi

Teknolojia mpya ya kutuma data ijulikanayo kama Li-fi imefanyiwa majaribio.

Li-fi ina uwezo wa kumfanya mtumiaji kupata huduma ya mtandao mara 100 zaidi ya Wi-Fi na hutoa kasi ya hadi Gigabait moja kwa kila sekunde. Soma zaidi hapa: Li-fi ina kasi mara 100 zaidi ya Wi-fi

ImageTHINKSTOCK

2. Choo kinachojifungua na kujiosha

Choo cha kisasa ambacho kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na pia kujiosha, ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki Las Vegas.

Choo hicho, kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi. Soma zaidi hapa: Choo kinachojifungua na kujiosha

ImageToto

3. Mercedes yazindua lori linalojiendesha

Mwanzo ilikuwa ni magari madogo sasa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Daimler Mercedes-Benz imezindua lori linalojiendesha lenyewe!

Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo yenye asili yake nchini Ujerumani,Wolfgang Bernhard alibofya kidude na mara lori likachukua usukani na kuenda lenyewe pasi na kusababisha ajali ya aina yeyote. Soma zaidi hapa: Mercedes yazindua lori linalojiendesha

4. Je una simu ya Android? Soma utafiti huu

Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana.

Uchunguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake. Soma zaidi:Je una simu ya Android?

ImageGetty

5. Samsung yakiri TV zake zinanasa sauti

Samsung imewaonya wateja wake kuhusu kutojadili mambo yao ya kibinafsi mbele ya televisheni zao.

Onyo hilo ni kwa wale watazamaji ambao hudhibiti televisheni zao kwa kutumia sauti.

Baadhi ya runinga hizo za kisasa husikiliza mambo ambayo wanasema na zinaweza kuwasilisha ujumbe kwa Samsung au mashirika yanayohusiana na Samsung kibiashara. Soma zaidi hapa:Samsung yakiri TV zake zinanasa sauti

Jumatano, 3 Februari 2016

Kampuni Ya GOOGLE Imeizidi Thamani Kampuni Ya APPLE

Kampuni ya Google yaizidi Apple kwa thamani

2 Februari 2016

Mshirikishe mwenzako

ImageGettyImageGoogle imenufaika sana kutokana na matangazo kwenye simu

Kampuni ya Alphabet, inayomiliki Google, imeipita Apple na kuwa kampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani.

Kwa mujibu wa ripoti ya mapato ya karibuni zaidi ya kampuni hiyo, faida yake ilifikia $4.9bn (£3.4bn) kwa robo ya tatu ya mwaka, ikipanda kutoka $4.7bn mwaka jana.

Tangazo hilo limesababisha bei ya hisa zake kupanda 9%.

Hii ina maana kwamba Alphabet sasa ina thamani ya $568bn, ikilinganishwa na Apple, ambayo thamani yake ni $535bn.

Hii ni mara ya kwanza kwa Alphabet kutenganisha mapato ya biashara ya Google, ambayo hujumuisha kisakuzi na YouTube, kutoka kwa biashara yake ya "Other Bets" ambayo hujumuisha miradi ya uvumbuzi kama vile magari ya kujiendesha na vipute vya kusambaza huduma za mtandao wa intaneti.

Kwa mwaka, Alphabet ilipata $16.3bn lakini takwimu zinaonyesha biashara yake ya "Other Bets" ilipoteza $3.6bn kipindi hicho, huku mapato ya jumla ya biashara ya Google yakipanda hadi $23.4bn, as kutokana na kuongezeka kwa matangazo mtandaoni.

"Inaonekana Google imeendelea kufanikiwa katika kufaidi kutoka kwa matangazo kwenye simu,” amesema Neil Doshi, meneja mkurugenzi wa utafiti katika kampuni ya Mizuho Securities.

"Miaka miwili au mitatu iliyopita, sekta ya simu ilitatiza sana Google. Kulikuwa na wasiwasi kwamba ingeathiri biashara zilizotegemea kompyuta, lakini huku simu sikianza kutumiwa sana kuchakura mtandaoni, matangazo kwenye simu yanakaribia yale ya kompyuta za kawaida kwa thamani.”

Jumatano, 27 Januari 2016

Toyota Yaongoza kwa Mauzo Duniani

ImageReutersImageKampuni ya magari ya Toyota

Toyota inaendelea kuongoza kama kampuni inayotengeza magari kwa mwaka wa nne mfululizo.

Kampuni hiyo iliuza magari milioni 10.15 kwa jumla mwaka 2015 na kuvunja rekodi ya matarajio ya wengi.

Kampuni ya Ujerumani ya Volkswagen imekuwa ya pili ikiwa imeuza magari milioni 9.93,ikifuatiwa na General Motors kutoka Marekani iliouza magari milioni 9.8.

Volkswagen ilikuwa inaongoza nusu ya mwaka wa 2015 kabla ya kashfa ya magari yake kutoa moshi mchafu kupunguza mauzo yake.

Biashara katika masoko makubwa kama vile Marekani na Japan na masoko yanayoinuka imepungua kutokana na kuanguka kwa uchumi duniani.

ImageAFPImageToyota

Mwaka 2014,Toyota iliibuka kidedea kwa kuuza magari milioni 10.23.

Kampuni hiyo imepata sifa kwa magari yake aina ya Prius hybrid,Camry,Corolla Sedan na Lexus.

Mauzo Ya Simu Za iphone Yapungua Duniani

ImageGettyImageMauzo ya simu ya Iphone yapungua

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple imeripoti kupungua kwa mauzo ya simu za iPhone katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho mwaka uliopita.

Kampuni hiyo iliuza simu milioni 75 mwaka uliopita ikiwa ni mauzo ya chini zaidi tangu mwaka 2007.

Hii ni kutokana na kuyumba kwa uchumi wa China.

Hata hivyo faida ya kampuni ya Apple iliongezeka katika kipindi hicho kwa zaidi ya dola bilioni 18.

Mhariri wa masuala ya Teknolojia katika mtandao wa CNET Ian Sherr, amesema huenda soko la simu za mkononi limefurika.