Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mapenzi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mapenzi. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 14 Februari 2016

Mapenzi Yanaua Asikwambie Mtu

Hichi ni kisa cha ukweli kabisa ambacho kimetokea huko visiwani Zanzibar mwaka huu Ni Baada ya Kufahamu kuwa mali yake inaibiwa.Jamaa huyo ambae jina liko kapuni Alifanikiwa kumfumania mke wake katika hotel flani hivi huko Zanzibar akivunja 'amri ya sita' live kwa macho yake kwaio sasa baada ya kufuma tukio hilo yule jamaa Aliumia sanaa Lakini sasa Cha kushangaza Alibadilika baada ya muda mfupi Akajifanya eti Amemsamehe Mke wake na anataka Maisha yaendelee.
Bhasi baada ya jamaa kusema hayo akawa sasa kama anamkumbatia mkewe kuonyesha kwamba mambo yaishe Hapo ndipo balaa lilipoanzia Yule Mwanaume baada ya kumkumbatia mke wake a.k.a kumhagi kama wasemavyo wadhungu Yule jamaa hakumuachia mke wake kamwe na alichofanya ni kumng'ang'ania mpaka karibu na dirisha alafu kilichofata ni kujirusha nae mpaka chini yaani kutoka ghorafani mpaka chini.
Hiyo chini hapo ni video ya tukio 👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Tafadhali sana kama unajijua unamoyo mwepesi usifungue maana inatisha sana pia watoto chini ya miaka 18 tafadhali msifungue

Jumapili, 17 Januari 2016

Zijue sifa saba za mwanamke anayeweza kukucheat

Kama mke wako, demu wako au side chick wako ana tabia zifuatazo, amesha-cheat kwako au ipo siku ataku-cheat.


1) Ana boreka haraka – Wanawake wanaoboreka haraka nirahisi kutafuta mwanaume mwingine wa kum-entertain, muda sio mrefu huyo mwanaume atachoka kum-entatain rafiki asiye na faida na ndio hapo atakapo anza kudai faida zake na wanaishia kuwa friends with benefits.

2) Marafiki wengi wa kiume – Mwanamke mwenye marafiki wengi wa kiume ni rahisi ku-cheat kwasababu anapata muda mwingi wa kuongea na wanaume wengine, watamsifia anavyopendeza, kama wewe unamwambia amependeza mara moja kwa wiki basi wenzako watamwambia anapendeza kila wanapoonana. Wataabza kumtoa out na mwisho wake ataona hao wanaume wamanjali kuliko wewe na kulala nao.

3) Anapenda attention – Wanawake wanaopenda attention ni rahisi kudanganyika. Wanaume wengi hasa ambao hawataki kuwa committed kwenye mahusiano yoyote wanatoa sana attention kwa wanawake. Mwanamke anayependa sana attention hawezi ridhishwa na attention ya mwanaume mmoja.

4) Anapenda vitu “material things”Wanawake wengi wanaopenda material things wanashindwa kupata kila kitu kutoka kwa waume zao au maboyfriend zao na kuishia kutafuta mwanaume mwingine ambaye ana uwezo wa kumnunulia vitu anavyotaka ili awatese wenzake kwenye instagram.

5) Ana marafiki ambao ni michepuko – Umeshasikia usemi kuwa ndege wanaofanana huruka pamoja, hata kama demu wako hana tabia ya ku-cheat, akiwa anakaa sana na marafiki ambao wana-cheat na yeye atashawishika kujaribu. Kama mke wako au demu wako ana kupigia story za marafiki zake wanao-cheat mwambie aachane nao haraka sana.

6) Anapenda kufanya ngono kuliko wewe – kila mkimaliza kufanya tendo la ndoa mwenzako anakwambia anataka tena, na wewe humtimizii basi lazima tatafuta serengeti boy ambaye anamsikiliza na kumpa anachotaka.


7) Anaujuzi kitandani kuliko wewe – Wewe kama umeshawahi kuingia kwenye dancing floor na kucheza na mtu ambaye anajua kucheza kuliko wewe, unasubiria tu wimbo ukiisha ukakae chini kabla hujaaibishwa, au kama wewe ndio unayejua kucheza vizuri utatafuta mtu mwingine anayejua kucheza kama wewe. Kwenye tendo la ndoa ni hivyo hivyo kama mwenzako ana ujuzi kuliko wewe, inabidi ufanye mazoezi ufikie kwenye ujuzi wake la sivo muda sio mrefu atasubiri wimbo ukiisha akakae chini au atafute mtu mwingine anayejua kucheza kama yeye.

Demu wako au mchepuko wako una tabia moja wapo kati ya nilizozitaja hapo juu? Usisite kuacha comments hapo chini


http://www.munishijr.blogspot.com