Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Vijimambo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Vijimambo. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 1 Juni 2016

Wazungu Sasa Wafakamia Kwa Mamantilie......HAPA KAZI TU.

Watalii ‘wafakamia’ chakula cha mamantilie

By Daniel Mjema, Mwananchi dmjema@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini watalii wengi wanaolala Moshi Mjini na maeneo ya jirani, hawali vyakula na vinywaji katika hoteli hizo.

Moshi. Ujio wa watalii wengi wanaoingia mjini Moshi kwa ajili ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kutembelea vivutio vya utalii, imegeuka shubiri kwa wamiliki wa hoteli, baada ya watalii kwenda kula kwenye vibanda vya mamantilie.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini watalii wengi wanaolala Moshi Mjini na maeneo ya jirani, hawali vyakula na vinywaji katika hoteli hizo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, hoteli nyingi zimeishia kuona idadi kubwa ya watalii wanaolala katika hoteli hizo, lakini hawaoni wakitumia migahawa yao kwa ajili ya chakula.

 

 

 


Vyanzo hivyo vimedokeza hali hiyo inajitokeza baada ya watalii kugundua vyakula wanavyouziwa kwenye hoteli hizo ni ghali, wakati chakula kama hicho wanakipata mitaani kwa bei ya chini.

Mathalan, baadhi ya hoteli za kitalii, vyakula huuzwa kati ya dola nane za Marekani (Sh17,000 za Tanzania) hadi dola 20 za Marekani (Sh43,000), lakini wanapata chakula hicho mitaani kwa Sh5,000 hadi Sh6,000.

Pia, baadhi ya watalii wanakwenda kunywa pombe kwenye baa za mitaani, ambako bia huuzwa kati ya Sh2,000 na Sh4,000 wakati katika hoteli hizo huuzwa kati ya Sh4,000 na Sh8,000.

Mkurugenzi wa Hoteli ya Leopard ya mjini Moshi, Priscus Tarimo, alisema hali hiyo imechangiwa na hoteli nyingi kupika aina zile zile za vyakula ambavyo watalii wanavipata nchini kwao.

“Kosa kubwa ni kutoweka vyakula vya asili. Unapomuekea vyakula kama wanavyokula kwao halafu ukampigia kwa standard (viwango) vya chini moja kwa moja ataikimbia hoteli yako,” alisema.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya King of Kilimanjaro Expedition, Shatiel Mhina, alisema tatizo ni hoteli kujikita kupika vyakula vya kizungu.

“Hao watalii wanakuja wakiwa na information (taarifa zote). Anakuambia anataka kula pilau au mtori au machalari (ndizi nyama) na atakuambia na bei ya huko mitaani. Hotelini hawapiki,” alisema.

Mamalishe Mwajuma Hamisi, alisema japo hafahamu Kiingereza, lakini watalii wanaofika kwenye kijiwe chake hutaka vyakula vya asili ambavyo havijawekwa kwenye friji muda mrefu.

Mfanyabiashara huyo alisema bei za vyakula vyake ni ya chini na kutolea mfano kuwa sahani moja ya pilau huuza kwa Sh2,000, bei ambazo watalii hao huzifurahia kuwa ni za chini tofauti na hoteli.

Jumamosi, 21 Mei 2016

Makanisa Kuwekewa Wi-fi hotspot Nchini Ujerumani

ImageISTOCKImageKanisa la French Cathedral, Berlin litakuwa miongoni mwa makanisa ya kwanza kunufaika

Makanisa ya Kiprotestanti maeneo ya kati nchini Ujerumani yatakuwa yakiwapa waumini fursa ya kuingia katika mtandao, kwa kuwawekea huduma ya wi-fi bila malipo.

Huduma hiyo itapatikana katika maeneo ambayo, kwa kufuata ‘hostpots’ ambalo ni jina la vitovu vya huduma, yamepewa jina "Godspots".

Huduma hiyo ya Wi-fi itawekwa katika makanisa 220 katika majimbo ya Berlin na Brandenberg.

Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha RBB, mpango huo baadaye utatekelezwa katika makanisa 3,000.

Makaburi matatu kuwekwa wi-fi Moscow

Makanisa ya kwanza kupata huduma hiyo yatakuwa kanisa kuu la French Cathedral eneo la Gendarmenmarkt na kanisa la Kaiser Wilhelm Memorial Church.

Watu wataweza kutumia huduma hiyo kutoka ndani nan je ya kanisa.

Wanaotumia huduma hiyo watalakiwa na ukurasa wa tovuti yenye maelezo kuhusu kanisa lenyewe, jamii na maelezo ya kidini.

Lakini baadaye, wataweza kuchakura chochote watakacho katika mtandao wote.

Jumamosi, 7 Mei 2016

Msichana Asiye na Mikono Ashinda Tuzo ya Mwandiko Mzuri

ImageMsichana asiye na mikono ashinda shindano la muandiko bora Marekani

Msichana wa miaka saba aliyezaliwa bila mikono ameshinda shindano la muandiko mzuri nchini Marekani.

Anaya Ellick kutoka Chesapeake,Virginia hatumii viungo vya kumsaidia wakati anapoandika.

Wakati anapoandika yeye husimama huku akishikilia kalamu yake katika mikono.

Mwalimu wake mkuu Tracy Cox kutoka shule ya Greenbrier Christian amemtaja kuwa mtu wa mfano mwema.

''Yeye uhakikisha kuwa hakuna kitu kinachomzuia kufanya atakalo'',alisema Cox.''Ni mkakamavu na ana muandiko mzuri katika darasa lake''.

Msichana huyo anadaiwa kuwashinda washindani wengine 50 ili kushinda taji hilo la kitaifa.

Orodha hiyo ya tuzo huwazawadi wanafunzi wenye akili, matatizo ya kimwili, au ulemavu endelevu

Jumapili, 14 Februari 2016

Mapenzi Yanaua Asikwambie Mtu

Hichi ni kisa cha ukweli kabisa ambacho kimetokea huko visiwani Zanzibar mwaka huu Ni Baada ya Kufahamu kuwa mali yake inaibiwa.Jamaa huyo ambae jina liko kapuni Alifanikiwa kumfumania mke wake katika hotel flani hivi huko Zanzibar akivunja 'amri ya sita' live kwa macho yake kwaio sasa baada ya kufuma tukio hilo yule jamaa Aliumia sanaa Lakini sasa Cha kushangaza Alibadilika baada ya muda mfupi Akajifanya eti Amemsamehe Mke wake na anataka Maisha yaendelee.
Bhasi baada ya jamaa kusema hayo akawa sasa kama anamkumbatia mkewe kuonyesha kwamba mambo yaishe Hapo ndipo balaa lilipoanzia Yule Mwanaume baada ya kumkumbatia mke wake a.k.a kumhagi kama wasemavyo wadhungu Yule jamaa hakumuachia mke wake kamwe na alichofanya ni kumng'ang'ania mpaka karibu na dirisha alafu kilichofata ni kujirusha nae mpaka chini yaani kutoka ghorafani mpaka chini.
Hiyo chini hapo ni video ya tukio 👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Tafadhali sana kama unajijua unamoyo mwepesi usifungue maana inatisha sana pia watoto chini ya miaka 18 tafadhali msifungue

Jumatano, 27 Januari 2016

Azikwa Na Mali Zake Zote

Azikwa na kreti za bia na soda Kahama

Wakati serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama bado ni kitendawili

TWEET

Kahama. Wakati serikali ikipigia kelele kukemea imani za kishirikina, wilayani Kahama bado ni kitendawili baada ya mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwamande, Kata ya Mwanase katika Halmashauri ya Msalala kufariki na baadaye wanakijiji kumzika na mali zake zote yakiwemo makreti ya bia na soda aliyokuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya baa.

Tukio hilo limetokea  jana katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo, Mahushi Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya kumzika na mali zake zote kwa imani ya kwamba kifo chake kimetokana na kurogwa na wao kuhofia kwamba wakibaki na mali zake nao watakumbwa na mauti.

Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Mwanase, Samson Masanja, Lutaja baada ya kifo chake alizikwa na baisikeli moja vitanda vinne na magodolo yake pamoja na masanduku ya nguo zake zote na vitu vingine vidogovidogo alivyokuwa akivitumia

Pia Masanja alisema, Lutaja alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla ya kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji kwenye kijiji hicho cha Mwamande ambapo  tukio hilo limehusishwa na imani za kishirikina

Wakati akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake ulitokana na kurogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa kutokana na kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao alirogwa