Alhamisi, 11 Februari 2016

Magari Yanayojiendesha Kuruhusiwa Barabarani

ImageGoogleImageGari linalojiendesha

Mfumo wa magari ya kujiendesha wa kampuni ya Google hivi karibuni huenda ukaidhinishwa na kuwa sawa na gari linaloendeshwa na dereva ,na hivyobasi kutoa fursa kwa magari yasio na usukani ama hata vikanyagio kuwa barabarani.

Shirika la usimamizi wa barabara kuu nchini Marekani ,ambalo hubuni sheria na utaratibu katika barabara za Marekani lilitoa wazo lake katika barua kwa kampuni ya Google uliowekwa wazi wiki hii.

Hadi kufikia sasa ,gari lolote lisilo na dereva halikuweza kuidhinishwa kama linaloweza kuendeshwa barabarani.

Lakini kutokana na maendeleo ya kiteknolojia,shirika hilo limebadili maono yake.

''Iwapo hakuna binaadamu aliye ndani anaweza kuliendesha gari hilo, ni rahisi sana kumtambua dereva kama chochote badala ya yeyote anayeliendesha gari,''lilisema.

ImageGettyImageGari la google linalojiendesha

Hii inamaanisha kwamba teknolojia ya gari la kujiendesha ,ambayo haina udhibiti wa gari hilo kama katika magari mengine ni hatua moja muhimu ya kuruhusiwa katika barabara za hadhara.

Huku Shirika hilo likitoa baraka zake kwa gari hilo ,gari hilo sasa limeafiki mahitaji ya usalama wa magari nchini humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni