Jumanne, 5 Aprili 2016

Aubameyang Avunja rekodi Nchini Ujerumani

ImageapImageAubameyang amefunga mabao 23 Bundesliga msimu huu

Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amevunja moja ya rekodi za uchezaji soka nchini Ujerumani.

Mchezaji huyo kutoka Gabon ndiye mchezaji kutoka Afrika aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi kuu ya soka ya Ujerumani Bundesliga msimu mmoja.

Aubameyang, ambaye alitawazwa mchezaji bora wa mwaka 2015 Afrika wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) alifunga bao lake la karibuni zaidi dhidi ya Werder Bremen Jumamosi na kufikisha 23, idadi ya mabao aliyofunga msimu huu.

Rekodi ya awali ilikuwa ya mabao 22 na iliwekwa na Cisse Papiss wa Senegal msimu wa 2010/11.

Papiss kwa sasa huichezea Newcastle United ya Uingereza.

Samatta, Aubameyang majogoo wa AfrikaAubameyang:Yaya Toure aliniudhi sana

Msimu huu wa 2015/16 pia, Aubameyang alikuwa ameweka rekodi kwa kufunga bao katika kila mechi mechi nane za kwanza za msimu wa Bundesliga, akiipita rekodi ya awali kwa mechi mbili.

Kwa kuwa alikuwa amefunga mabao mechi mbili za mwisho za msimu wa 2014-15, alivunja rekodi nyingine ya kufunga mabao mfululizo katika mechi 10 za Bundesliga. Mtu pekee aliyekuwa ameifikia ni Klaus Allofs miaka 30 iliyopita.

Maoni 2 :

  1. Hakika hawa wawil ni vipaji na kujituma vyawapeleka hapo walipo sasa

    JibuFuta
  2. Hakika hawa wawil ni vipaji na kujituma vyawapeleka hapo walipo sasa

    JibuFuta