Rais John Magufuli (Kushoto) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kulia)
Dar es Salaam. Hatimaye Sudan Kusini imeingia rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Rais wa taifa hilo, Salva Kiir kusaini mkataba na Rais John Magufuli unaorasimisha taifa hilo kujiunga katika jumuiya hiyo.
Kwa mantiki hiyo, EAC ina jumla ya wanachama sita ambao ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na mwanachama mpya wa sasa, Sudan Kusini.
Rais Magufuli ambaye ndiye mwenyekiti wa EAC amesema mkataba huo unafungua fursa muhimu kwa Watanzania za kibiashara na uchumi zilizopo katika taifa hilo lililojitenga kutoka Sudan miaka mitano iliyopita.
Rais Salva Kiir ameahidi kufanya mabadiliko makubwa nchini humo ili kuendana na mahitaji ya EAC ikiwemo kuimarisha amani, umoja na mshikamano katika taifa hilo changa lililokumbwa na mapigano ya wao kwa wao.
Rais Magufuli amesema atatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha safari ya Sudan Kusini katika kufikia hatua zilizofikiwa hadi sasa ndani ya EAC ikiwemo soko la pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni