Jumapili, 1 Mei 2016

VOTE for MSHANGAMA SHAMIRA Daruso Vice President

Habari za mda huu ndugu zangu wana UDSM.

Jina langu kamili ni MSHANGAMA SHAMIRA  mgombea nafasi ya umakamu wa Raisi DARUSO 2016/2017 kwa moyo mkunjufu ndugu zangu wa udsm naomba mnipe ridhaa hii ya kuwatumikia ili nikatimize matakwa ya wana udsm ya mda mrefu niliyoyafanyia utafiti jinsi gani ya kuyatekeleza:

1. Nitarudisha utaratibu wa kuwepo na revolution square movement ambayo ni haki yetu, eneo hili huwa linatumika na wana udsm haswa wana harakati kujadili mambo ya msingi yanayohitaj ufafanuzi na utatuzi, mfano kwa boom kutoka 5000-7500 movement yake ilianzia revolution square... Nikiwa kama makamu wa raisi nikishirikiana na raisi wangu kikatiba tutamwandikia barua DVC academic juu ya matakwa yetu ya kukutana revolution square na kuweza kufanya makutano hayo kama students by-law inavyosema.

2. Ili kujiridhisha na utendaji wa viongozi wetu tuliowachagua, nitahakikisha suala la students BARAZA linakuwepo angalau Mara mbili kwa semester kama katiba inavyoelekeza katika ibara ya 28, ili kujadili masuala mbali mbali kati ya wanafunzi na viongozi na kupitia utendaji kazi wa kila kiongozi ikiwa pamoja na taarifa za mapato na matumizi ya DARUSO, viongozi kuhojiwa, kukosolewa na kushauriwa.

3. Katiba ya DARUSO inaainisha ushirikiano wangu na raisi katika kuunda baraza la mawaziri katika ibara ya 15(3) ya katiba ya Daruso nitahakikisha tunapanga baraza dogo la mawaziri, wizara ziwe 10 na mawaziri 22, kutoka wizara 11 na mawaziri 25 waliopo hivi sasa, hii itapunguza gharama za DARUSO kujiendesha na hizi pesa zitatumika katika mambo mengine yatakayotukabili ikiwemo kuzitumia katika majanga yanayojitokeza.

4. Nitahakikisha kwa kushirikiana na Rais, ofisi ya bunge na cabinet tunamshauri na kumtaka DEAN OF STUDENTS katika utekelezaji wa majukumu yake azingatie majukumu yake halisi ambayo ni kushauri tu na siyo kuliingilia au kulitisha bunge, wanafunzi au viongozi wa Daruso au kususia vikao ili vikose uhalali.

Hili litawezekana kwani kisheria, Dean of students mamlaka yake yanatajwa katika ibara ya 28 (3), ya kwamba atakuwa mshauri mkuu mwenye 'uhalali' wa kuhudhuria vikao vya Daruso.

5. Nitaendeleza timu ya mpira wa miguu ya wanawake ambayo tumeshaanza nayo mazoezi ili iwe bora na chuo chetu kipate sifa kwenye sekta ya mpira wa miguu...timu ya wanaume ntahakikisha inapata mechi nyingi za kirafiki na timu kubwa za uraiani ili kukitangaza vyema chuo chetu lakini pia nitasimamia kuhakikisha Inter-colleges competitions inafanyika ili kutafuta wachezaji katika college zote za UDSM.



6. Nitahakikisha kila waziri anatimiza wajibu wake ipasavyo kwa kufanya monthly review mwenyewe kama makamu wa raisi na kumshauri raisi kuondoa wote wanaofanya kazi kwa uzembe, Lakini pia nitahakikisha serikali yote ya Daruso haihamii main campus na badala yake angalau Naibu au waziri katika wizara za Makazi (accomodation), Ulinzi na wizara ya usafiri na wanakuwa wakazi wa Mabibo ili kukabiliana kero zinazojitokeza na kuhojiwa na wana UDSM juu ya kero za masuala tajwa na kuzitatulia ufumbuzi.

7. Nitahakikisha Mimi na raisi tunateua waziri wa elimu mchapakazi na atakayeshirikiana na wenyeviti, makatibu na wabunge wa college zote na kuhakikisha mazingira ya usomaji ambayo ni rafiki wa wana udsm wote, kukabiliana na changamoto zote za kitaaluma na pia kuzingatia makundi maalum ya walemavu.

8. Katika uchaguzi wa mafood tester watawekwa mafood tester ambao watakua wanafuatuliwa ufanyaji wao wa kazi wao kila wiki na kuondoa wote wanaozembea kwa kutoka Fanya kazi zao.

9. Nitahakikisha nashirikiana bega kwa bega na raisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku kwa kumshauri, kumkumbusha na kumshinikiza katika masuala ya msingi yanayotuhusu wana DARUSO .

10. Kwa wenzetu mnaosoma COICT na SJMC kwa kushirikiana na raisi nitahakikisha kunakuwa na permanent shuttle kwa ajili ya route za kila Siku.

Kuhimiza kuharakishwa kwa ukarabati mdogo uliosalia wa hosteli za CoICT- Kijitonyama zenye uwezo wa kubeba wanafunzi takribani 500 ukamilike kwa wakati ili kupunguza angalau kidogo adha ya tatizo la hostel.

MUNGU atubariki tufikie matarajio yetu, naombeni kura zenu.

MSHANGAMA SHAMIRA

mgombea nafasi ya umakamu wa Rais, Daruso.

Jina langu litakuwa la pili katika ballot paper siku ya Jumatatu.



MIMI NI MTUMWA WENU, NITUMENI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni