Music Industry Inakua kilasiku na Kuzidi kuwa Biashara kubwa sana Yenye Faida Nyingi kama itafanywa kwa Umakini Mkubwa. Pia katika Tasnia hii kilasiku Wasanii wapya Wanaibuka na kufanya kazi nzuri sana Ambazo nyingine zikipata support kubwa kama airtime ya kutosha huwa zinasaidia Msanii mchanga kusikika zaidi kwa muda mfupi kwa watu wengi. Bhas baada ya kusema hayo wadau wangu wa nguvu Leo namtambulisha Msanii Mpya kabisa kutoka Arusha a.k.a Arachuga kwa machalii wa Ara Au sio??
Okei leo nipo na Msanii wa bongofleva mpya kabisa kutoka mkoani Arusha ambae anaitwa DOUBLE DEE
Double Dee amekuja na ngoma yake inaitwa 'Wanna be' ambapo humo ndani amemuimbia mtoto mzuri tu so kwa dadaz wote hii ngoma inawahusu sanaa kwasababu tunajua Mapenzi ndo yapo on fleek sikuhiz. Ngoma hii bado haijafanyiwa video lakini Uongozi wake unashughilikia mpango wa kichupa kikali kabisa ilikuweza kumtambulisha vizuri DOUBLE DEE
Nikiwa napiga stori na Meneja wa msanii huyu ambae pia ni CEO wa MBAGA ENTERTAINMENT ambayo ndo kampuni inayomsimamia kwa sasa Double dee Meneja amesema kwamba wamejipanga vizuri yeye na kampuni yake kuhakikisha kwamba Double dee anafika mbali zaidi kutokana na muziki wa sasa kuwa na ushindani mkubwa.
MENEJA, David Mbaga
Nyimbo ni kali sana kwaio fanya kila uwezalo uhakikishe unaisikiliza Ngoma hii mpya kutoka kwa DOUBLE DEE
Hongera kijana akaze buti katika style yake aiwekeee mahadhi flan ivi itamtoa kimasomaso
JibuFuta