Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Burudani. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Burudani. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 11 Mei 2016

Msanii KINYAMBE Afariki dunia

 Mchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah  "KINYAMBE" amefariki dunia leo usiku huko nyumbani kwako Mbeya. Mmoja wa wanandugu wa Kinyambe ameithibitishia Saluti5 kuwa msanii huyo wa filamu  ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/05/mchekeshaji-kinyambe-afariki-dunia.html?m=0

Msanii huyu alikua mahiri sana kwa staili yake ya uchekeshaji kama tahira hivi,Alifanya kazi nyingi na kampuni ya Alriyam production iliopo Jijini Tanga na wasanii wengine kama masele,kazi,masai, 

Pia kinyambe alishawahi kuimba muziki na nyimbo zake zipo nyingi tuu mtandaoni 

 

 

Hapo juu 👆👆👆 ndo post ambayo watu wengi waliiona katika mtandao wa kijamii wa FACEBOOK hapo habari za kifo cha msanii huyu zilipoanza kusambaa kwa kasi sana

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya msanii wetu KINYAMBE .......REST IN PEACE KINYAMBE

Jumapili, 14 Februari 2016

Baba Diamond:Acha Nife Studio kwa Diamond

Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma alipofika getini kwenye studio ya Diamond.

Na Musa Mateja Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Abdul Juma ambaye ni baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa akiwa katika studio ya mwanaye iliyopo Sinza Mapambano jijini Dar akidaiwa kusaka suluhu ya ugomvi wake na mwanaye, Risasi Jumamosi lina habari kamili.

Akimpigia simu Diamond

Katika kusaka suluhu ya ugomvi wao huo wa muda mrefu, chanzo kilieleza kuwa, mzazi huyo hakujali ugonjwa wa miguu unaomsumbua kwa muda mrefu, kwani alikuwa tayari hata kufia studioni hapo ilimradi afanikiwe kuonana na Diamond, wamalize tofauti zao.

Diamond

TUJIUNGE NA CHANZO
Februari 10, mwaka huu, mwanahabari wetu alipokea simu iliyoeleza kuwa mzazi huyo alikuwa akimsaka Diamond ambapo alilazimika kuweka makazi ya muda kwenye jengo lililo studio hiyo huku akiwa mgonjwa, akiwa na lengo moja tu, kumaliza tofauti zao.

Akitafta mahala pa kukaa ili amsubiri Diamond

“Njooni hapa Mapambano kwenye studio ya Diamond, baba Diamond amefika hapa, anaonekana mgonjwa hata tembea yake anazunguka hapa mara atoke geti hili, mara aende lingine maana nyumba hii ya studio ina mageti mawili.

“Anasema bora afie hapa lakini lazima leo aonane na Diamond ili moyo wake uridhike. Ameongozana na mwanaume mmoja nafikiri ndiye anayempa msaada wa karibu,” kilisema chanzo hicho.

RISASI MZIGONI
Baada ya kupata maelezo hayo kutoka kwa chanzo, mwanahabari wetu kwa kutumia usafiri wa bodaboda, alifika fasta katika studio ya Diamond na kumkuta mzee huyo aliyeonekana kuumwa miguu iliyokuwa imevimba, akihaha kugonga geti la nyumba hiyo ya studio.

Kwa kutumia kamera za kidaku zaidi, mwanahabari wetu alikita kambi maeneo ya jirani na studio hiyo tangu saa 5 asubuhi hadi jioni akisubiri kuona namna itakavyokuwa wawili hao watakapoonana, huku akimfotoa picha tofauti mzazi huyo na mpambe aliyeongozana naye.

WACHOKA, WAKAA
Kuna wakati mwanahabari wetu alimshuhudia baba Diamond na mwenzake wakiwa wamechoka kugonga mageti ya nyumba hiyo na kuamua kukaa chini katika mawe yaliyokuwa jirani.
“Mzee anaonekana anaumwa yule, ona anavyokaa pale anaonekana ana maumivu mwilini ila atakuwa anajikaza tu, si bora angepumzika tu nyumbani akatafuta njia mbadala ya kuonana na Diamond,” alisikika shuhuda mmoja.

RISASI LAMVAA BABA DIAMOND
Baada ya kumfotoa picha za kutosha, Risasi Jumamosi lilimfuata mzazi huyo na kumuuliza kulikoni afike studio hapo angali mgonjwa na kwa nini asiwasiliane na mwanaye kwenye simu? Mzee huyo alifunguka:

“Yametokea mengi huko nyuma, lakini nahisi ni muda muafaka wa kumaliza hizi tofauti zetu. Katika pitapita zangu maeneo haya, nikaoneshwa hapa ndiyo studio kwake, nikaona bora nishinde hapa kutwa nzima nikiamini lazima atafika tu japo naumwa lakini sikuona haja ya kuondoka ni bora nifie hapa lakini leo hadi nionane naye.

“Nimegundua Diamond hana makosa. Mimi ndiyo kuna maeneo nilikuwa siko sahihi. Mama yake tulishamaliza tofauti zetu, tuko vizuri na ndiyo maana nikaona nimsake Diamond kwa udi na uvumba.”

AAMBULIA PATUPU
Licha ya kushinda kwa matumaini studio hapo hadi jioni, Risasi Jumamosi lilimshuhudia mzazi huyo akiondoka bila mafanikio kwani licha ya wasanii wa Diamond kudaiwa huwa wanafanya mazoezi karibu kila siku kwenye nyumba hiyo, siku hiyo geti halikufunguliwa hadi mzazi huyo alipokata tamaa na kuamua kuondoka zake.

DIAMOND HAPATIKANI
Gazeti hili lilifanya juhudi za kuwasiliana na Diamond kuhusu suala hilo lakini halikuweza kupata mawasiliano yake ya moja kwa moja baada ya marafiki zake kudai kuwa yupo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

TUMEFIKAJE HAPA?
Diamond na baba yake waliingia kwenye bifu zito baada ya mzazi huyo kumtuhumu mwanaye kuwa hamjali kwa sababu tu ana ugomvi na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’.

Alhamisi, 4 Februari 2016

Nuh Mziwanda Amuomba Shilole Msamaha kwa Mara nyingine tena

Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

Musa Mateja, AMANI
STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.

“Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho.

Akiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole.

Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi.

“Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana. Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.STAA wa Wimbo wa Msondo Ngoma, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anasemekana amemwangukia kwa mara nyingine aliyekuwa mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumtaka warudiane.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mbongo Fleva huyo amekuwa katika wakati mgumu tangu alipoachana na Shilole hivyo kulazimika kumpigia simu na kumwandikia ujumbe wa maneno akimuomba amsamehe na warejeshe penzi lao kama ilivyokuwa zamani.

“Ndugu yangu nikikwambia kuwa, Nuh maji yamemfika shingoni basi huna haja ya kuuliza mara mbili namna yalivyomfika kwani, juzikati nilikuwa naongea na Shilole akalalamika kwamba, jamaa huyo ameanza tabia ya kumpigiapigia simu akimwomba warudiane jambo ambalo Shilole analitolea nje,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupenyezewa ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Shilole kwa nia njema ya kutaka kujua ukweli wa madai hayo ambapo alisema ishu hiyo ipo ila hawezi kuanika wazi.

“Suala la Nuh kwa sasa sitaki kuendelea kuongea kwani nitakuwa nampigia debe mtu na kazi hiyo niliifanya sana.

Unachotakiwa kujua kutoka kwangu ni kwamba mimi naendelea kupigania maisha tu ili niweze kusonga mbele na hapa nipo kipesa zaidi hivyo sina tena muda wa kuendelea kumpa nafasi bwana wa aina yeyote kwani hapo nyuma maisha yangu yalirudi nyuma hatua nyingi sana,” alisema Shilole.

Jumamosi, 30 Januari 2016

Gari La Wema Halina Vibali

Mama kijacho Wema Sepetu ‘Madam’

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Mama kijacho Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ kwa mara nyingine ametengeneza kichwa cha habari, safari hii amewekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kuendesha gari aina ya Range Rover Evogue bila kuwa na vibali,Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.

Tukio hilo lililodumu kwa takriban saa tatu lilijiri Jumanne iliyopita maeneo ya Aficana, Mbezi Beach jijini Dar wakati mrembo huyo alipokuwa ‘kiguu na njia’ kwenda kwenye bethidei ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Kibadude.

Gari lake likikaguliwa na maofisa wa TRA

NI LILE ALILODAI KUJIZAWADIA

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichokuwepo eneo la tukio, gari hilo alilokamatwa nalo Madam ni lile alilojizawadia kwa mbwembwe nyingi mwishoni mwa mwaka jana katika siku yake ya kuzaliwa ambalo lina thamani ya shilingi milioni 200 za Kibongo.

“Nimepiga picha. Wamemtaiti hapa Mbezi Africana, naona maofisa wa TRA wanamhoji. Lina tatizo katika uhalali wa kuingia nchini. Hapa sasa naona wanaomhenyesha ile mbaya. Si kawaida.”

AMWAGA CHOZI

“Sasa namuona Madam machozi yanamtoka yenyewe… anahaha, mara aende huku mara kule. Nahisi so litakuwa limemkalia vibaya maana kila simu anayopiga hapati msaada,” kilinyetisha chanzo hicho.

Ukaguzi ukiendelea

TRA WABAINI FIGISUFIGISU

Gazeti hili lilizungumza na ofisa mmoja wa TRA ambaye alikuwepo kwenye tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa mamlaka hiyo aliweka wazi kuwa, walibaini figisufigisu katika gari hilo.

Range la Wema

“Hili gari ni moja kati ya magari ambayo yanaingia nchini kutokea nchi ya Msumbiji. Hata namba zake za usajili zinaonesha hivyo. Sasa huwa yanakatiwa vibali vya miezi mitatu au kulipiwa ushuru na kununuliwa. Liliingia nchini tangu mwaka jana.

“Tumekuta halina vibali maana vibali vya miezi mitatu vimeisha, tumemuuliza atoe nyaraka za gari, anasema zipo nyumbani, tukamwambia twende huko nyumbani ukazitoe, akabadili lugha, akasema anazo Steve (Nyerere). Inaonekana hili gari lina matatizo makubwa ya ushuru,” alisema ofisa huyo.

FIGISU NYINGINE

Kumbukumbu zinaonesha gari hilohilo la Wema ambalo alisema amejinunulia kwa fedha zake, ndilo alilodaiwa kununuliwa na mbunge machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye aliwahi pia kutajwa kuwa ndiye baba kijacho wake kabla ya Idris Sultan kuibuka na kujinadi kuwa ndiye ‘mmiliki’ halali wa tumbo hilo.

KIGOGO SERIKALINI AMUOKOA

Paparazi wetu alimtafuta mtu wa karibu kabisa na Wema ambaye alieleza kuwa, Madam baada ya kuhaha kwa muda mrefu eneo hilo huku akiwa chini ya ulinzi wa polisi wenye bunduki, alipata wazo la kumpigia kigogo mmoja serikalini (jina tunalo) ambaye alimpa msaada kwa masharti.

“Alimpigia simu… (anataja jina la kigogo), akamweleza matatizo yaliyomkuta, naye akazungumza na maofisa wa TRA, wakakubaliana kwa masharti kwamba asilitumie gari hilo ndani ya wiki moja mpaka apeleke vibali vya gari hilo,” alisema mtu huyo wa karibu na Wema.

HUENDA LIKATAIFISHWA KAMA LA WOLPER

Kwa mujibu wa taratibu na sheria za TRA, endapo Wema atashindwa kutoa nyaraka muhimu za gari hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na  kutaifishwa kwa gari hilo kama ilivyomtokea mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye mwaka 2014, gari lake aina ya BMW X6 lilikamatwa na kutaifishwa kwa kushindwa kulipia ushuru na kukosa vibali halali.

WEMA ASAKWA

Baada ya kupewa taarifa hizo, gazeti hili lilimtafuta Wema kwenye simu yake ya mkononi lakini muda wote iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

MENEJA WA WEMA ANENA

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, meneja wa msanii huyo, Martin Kadinda alisema yeye alisikia kwa watu kuhusu taarifa za Madam kukamatwa na gari hilo lakini alipomuuliza alimwambia si kweli, ni uzushi tu na hata gari hilo lipo nyumbani aende kuliona jambo ambalo alilifanya na kweli akajionea gari hilo.

“Ni uzushi tu. Nimeongea na Madam, akanihakikishia kwamba hamna kitu kama hicho. Nikaenda kulitazama gari, nikalikuta nyumbani kwake Ununio, shwari kabisa,” alisema Martin.

Gazeti ndugu na hili, Amani, toleo la Alhamisi iliyopita, ukurasa wa nyuma kulikuwa na habari yenye kichwa; Range la Wema layeyuka. Msingi wa habari hiyo ni taarifa kuwa, Wema haonekani akiwa na gari hilo licha ya kujinadi kuwa ni lake. Amekuwa akitumia kigari kidogo ‘ki-kirikuu’ kuendea kwenye shughuli zake.

Ilidaiwa kuwa, Wema alilipeleka gereji au yadi ya kuuzia magari, gari hilo hali iliyowafanya mapaparazi wa OFM kulisaka bila mafanikio huku ikielezwa kuwa, gari hilo si lake bali huwa anapepewa kwa muda kujiachia nalo.

Jumatatu, 18 Januari 2016

LULU NA MAMA KANUMBA KULIKONI TENA???

Staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’

Stori: Mayasa Mariwata, Wikienda
Dar es Salaam: Bifu jipya! Kwa mara nyingine, baada ya kurushiana vijembe kwa muda mrefu, mama mzazi wa aliyekuwa stadi wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Flora Mtegoa amemuonya staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuwa amemchosha kwa vijembe mitandaoni hivyo anamuomba amuache.

NI KATIKA MAHOJIANO MAALUM
Katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda, mama Kanumba alisema Januari 7, mwaka huu ilikuwa ni ‘bethidei’ yake ya kutimiza umri wa miaka 60, ikiwa ni siku moja tu kabla ya ile ya Kanumba (Januari 8) hivyo kwa umri huo hataki kuendekeza mabifu na Lulu aliyekuwa mwandani wa mwanaye kabla ya kukutwa na umauti Aprili 7, 2012.
Mama Kanumba alifunguka kuwa anamshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka 2015 lakini hawezi kuusahau mwaka huo kutokana na mambo aliyomfanyia Lulu ambayo hapendi kuyakumbuka.

Flora Mtegoa “Mama Kanumba.”

MAMA KANUMBA LAIVU
“Kwa sasa nina umri wa miaka 60, ni mara tatu ya umri wa Lulu. Sitaki tena malumbano na Lulu kwani amenichosha na ninachowaombeni mwaambieni aniache.

KISA VIJEMBE MTANDAONI
“Lulu ni mtoto mdogo sana kwangu, mara kwa mara huwa anaposti (kutumbukiza) vijembe mtandaoni akinikejeli kwa kuwa anajua situmii mitandao ya kijamii lakini ndugu zangu huwa wananiambia kunionesha kila kitu.

“Ninachomuomba akome hiyo tabia ya kunisakama mitandaoni, kama ameamua kuvunja ukaribu na mimi aache kunidharua japokuwa mimi nilimsamehe kwa moyo mmoja lakini hajathamini hilo.

“Lakini yote kwa yote namshukuru Mungu mwaka 2015 ulivyoisha maana ni mwaka ambao Lulu alinibadilikia na kuanza kunikosea heshima.

MAUMIVU ZAIDI
“Hakuna kitu kilichoniumiza kama siku aliposti mwanaume mmoja akisema kuwa huyo ndiye mtu wake wa karibu ni wazi kuwa hicho kilikuwa kijembe kwangu.
“Pia kitendo cha kutohudhuria kumbukumbu ya kifo cha Kanumba pamoja na kwamba nilimuomba na alikubali kiliniumiza mno.

AJUTA KUMSAMEHE
“Niliwaza sana kuwa ni Lulu huyuhuyu aliyenifuata akanipigia magoti na kuniomba msamaha juu ya mwanangu nami nikamsamehe kwa moyo mmoja? Wakati mwingine hata najuta kumsamehe.

“Lulu anapaswa kuangalia vitu vya kuandika mitandaoni au anyamaze kimya kwa sababu anatakiwa kujua kuwa kuna kesi ya msingi haijaisha.
“Vizuri akakumbuka kuwa bado mimi nina maumivu na chozi la kifo cha mwanangu linanitoka hivyo asiendee kunichokonoa,” alifunga mjadala mama Kanumba.

LULU ANASEMAJE?
Kama ilivyo sheria ya gazeti hili kutafuta mzani wa habari, mwanahabari wetu alimtafuta Lulu kisha kumsomea tuhuma zake kutoka kwa mama Kanumba alizungumza kwa kifupi kisha akakata simu:

“Sina cha kuzungumza kuhusu hilo kama kweli huyo mama (mama Kanumba) angekuwa na shida na mimi angenipigia mwenyewe au angeniambia nimpigie.”

TUMEFIKAJE HAPA?
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 kwa kuanguka katika mazingira yaliyodaiwa kutokana na ugomvi kati yake na Lulu. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa Kanumba, Sinza ya Vatcan, Dar.

Baada ya kifo hicho, Lulu alikamatwa na kuwekwa Mahabusu ya Segerea jijini Dar na baadaye kuachiwa kwa dhamana.

Baada ya kutoka mahabusu, Lulu na mama yake, Lucresia Karugila walimfuata mama Kanumba na kuomba msamaha ambapo mama huyo aliupokea na kusema anamwona Lulu kama mtoto wake na yote ya nyuma yamepita.

Kuanzia hapo, Lulu na mama Kanumba wakawa na ukaribu wa kindugu huku kila mwaka wakifanya kumbukumbu ya Kanumba pamoja kabla ya mwaka jana kutibuana na sasa hali ni tete.

Jumapili, 17 Januari 2016

Diamond na Allykiba vipi tena???

Nasibu Abdul ‘Diamond Platmumz’.

DAR ES SALAAM! Kutokana na mwenendo wa bifu lao la chini kwa chini ni dhahiri mafahari wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platmumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wamefika pabaya kwani safari hii zimeibuka tuhuma za kuzibiana riziki kimataifa, Ijumaa Wikienda linashuka na mchapo kamili.

Chanzo makini kimeeleza kuwa, Team Kiba ambao umoja wao unaonekana zaidi katika Mtandao wa Instagram, wamecharuka vibaya wakimtuhumu Diamond kuwa anawasiliana na vituo vya kimataifa kama MTV na kuwaambia wasipige nyimbo za King Kiba.

Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

“Jamaa hafanyi fea, anawasiliana na wale wa vituo vya kimataifa na kuwaambia wasipige nyimbo za Kiba, anamzoofisha kweli,” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.

Mara baada ya kusambaa kwa taarifa hizo za Diamond ‘kumficha’ mwenzake kimataifa, Team Kiba na Team Diamond walianza kuporomosheana matusi mazito mtandaoni.

Team Kiba waliapa kufanya ziara nchi nzima kushinikiza Diamond aache ubaguzi huku Team Diamond wakimtetea msanii wao wakisema si kweli kwamba anafanya hivyo bali amekuwa akiwasaidia wasanii wengi hivyo Team Kiba wanatapatapa.

Baada ya ubuyu huo kutua mezani, mwanahabari wetu alimsaka King Kiba kupitia simu yake ya mkononi ambapo alisema kama kweli vituo hivyo vinamsikiliza Diamond, vitakuwa havimtendei haki.

“Kama kweli MTV watakuwa wanampatia jukumu Diamond la kupitisha ngoma zetu basi watakuwa hawafanyi fea, sidhani kama ni kweli wanafanya hivyo na Diamond anaweza kufanya hivyo,” alisema Kiba.

Akijibu tuhuma hizo mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond alikaririwa katika Televisheni ya Taifa (TBC 1), akielezea namna ambavyo amekuwa akisikitishwa na watu kumwambia anawabania baadhi ya wasanii kupigwa kimataifa na kusema wanamuonea.

Jumamosi, 16 Januari 2016

IDRISS SULTAN AMTUSI DIAMOND

Idris Sultan na Wema Sepetu

DAR ES SALAAM: Hii dharau! Siku chache baada ya staa wa Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kudaiwa kushika ujauzito ambao mhusika bado ni fumbo, balaa limezuka kufuatia Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2015, Idris Sultan kudaiwa kumtusi zilipendwa wa mrembo huyo, Mbongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Risasi Jumamosi linakujuza.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Idris amekuwa akijitapa mitaani kuwa yeye ndiye kidume aliyeweza kumpa mimba Wema na kwamba ni daktari bingwa wa magonjwa sugu, yakiwemo ya uzazi kwani kwake kunapatikana tiba mbadala.

Majigambo hayo yanadaiwa kuharibu urafiki uliokuwepo baina ya wawili hao, kwani Diamond anachukulia kama ni kumtusi kwa vile aliwahi kujihusisha kimapenzi na Wema kwa muda mrefu bila kupata ujauzito.

Diamond na Wema Sepetu, enzi zilee.

KAMA KUNA URAFIKI NI KIINI MACHO
“Kitu ambacho watu hawaelewi ni kwamba hivi sasa urafiki wa Diamond na Idris ni kiini macho tu, kwani majivuno ya Idris ya kutoka na Wema yameleta uhasama mkubwa, hasa baada ya kujigamba kuwa ameweza kumpa ujauzito.

“Inadaiwa juzikati Idris akiwa na Wema sehemu, rafiki zake wakawa wanampongeza kwa taarifa zilizosambaa kuwa yeye ndiyo amemdunga mimba mrembo huyo ambapo kijana huyo alisikika akisema hakuna mwanamke asiyezaa duniani, isipokuwa kinachotokea ni kuto-match (kuendana) kwa damu za wawili. Eti kwa kitendo hicho yeye ndiye kidume cha mbegu,” kilisema chanzo hicho.

Ommy Dimpoz

OMMY DIMPOZ NAYE ATAJWA
Ommy Dimpoz ambaye ni rafiki wa karibu wa Diamond, naye anatajwa kuwemo katika watu wanaompiga vijembe kwa kufurahia kitendo cha Idris kumjaza mimba Wema kwa kile kinachosemwa kuwa wawili hao wana ka-bifu ka chini kwa chini, kisa kikiwa siri yao.

“Ommy Dimpoz naye ni miongoni mwa watu wanaosapoti kwa asilimia kubwa Idris kumpachika mimba Wema na kwamba anaonesha wazi kuunga mkono kila kitu kinachofanywa na kijana huyo katika kumuumiza Diamond kupitia mimba hiyo.”

DIAMOND ANASA UBUYU
Habari zinasema kuwa maneno yaliyokuwa yakitembea katika kundi la Idris yalimfikia staa huyo wa muziki wa kizazi kipya nchini, ambaye alisikitishwa na kitendo cha kuonekana kama hakuwa na uwezo wa kumpa mimba Wema, akitamka kuwa wanaomsema hivyo hawajui jinsi yeye na Wema walivyokuwa wakiishi kimapenzi.

Idris Sultan

IDRIS HUYU HAPA, MSIKIE
Baada ya kumegewa ubuyu huo, juzi paparazi wetu alimtafuta mshindi huyo wa BBA aliyejishindia dola 300,000 (zaidi ya shilingi milioni 500) na kubahatika kukutana naye ana kwa ana katika eneo moja, nje kidogo ya jiji.

Alipoulizwa kuhusu ukweli wa madai ya kumtusi rafiki yake huyo, huku akichekacheka, Idris alishindwa kufunguka moja kwa moja, badala yake akasema hategemei kuja kuwa na tatizo na Diamond kwa sababu ya ujauzito wa Wema, hasa kwa kuwa tayari ana mtoto (Tiffah) aliyempata kwa mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari’.

“Diamond hawezi kuwa na mawazo hayo kwani haoni tatizo lolote kwangu kuwa karibu na Wema, hata nikizaa naye, kwa sababu uhusiano wao ulishamalizika.

“Hata hivyo hayo yatabaki kama madai. Mimi kuitwa kidume itatokana na namna waitaji watakavyokuwa wamenichukulia. Ila kiukweli sidhani kama kuna mtu anaweza kuja kuninunia kisa Wema maana suala la uhusiano au kuwa karibu na mtu inategemea tu na watu wenyewe jinsi wanavyoweza kuchukuliana na kuwaziana.”

KUANIKA KUHUSU MIMBA YA WEMA
“Suala la mimba ya Wema nitakuja kuliweka vizuri baada ya mwezi mmoja. Kwa sasa niache kwanza maana nina mambo mengi ya kufanyia kazi, sitaki kabisa kuanza kuvuruga mudi za watu na ndiyo maana naona hakuna haja kwa muda huu kuongelea ishu hiyo ila yasemwayo yanaweza kuwa na maana kama yameelezewa vizuri,” alisema Idris.

Mbongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’.

DIAMOND NAYE HUYU HAPA
Gazeti hili lilifanikiwa pia kumnasa mkali wa kibao cha Utanipenda? Diamond ambaye baada ya kuelezwa kilichopo alisema kwa sasa hana muda wa kusikiliza maneno ya watu wala kujibu kila anachosikia, zaidi anahangaikia maisha yake ili kuweza kufikia ndoto alizojipangia kwa vile maneno yapo kila siku na hayaepukiki.

“Dah! Mimi sioni kama kuna kitu cha ajabu wala kuzungumzia hapo, zaidi naweza kusema mimi sina muda tena wa kuanza kuzungumzia mtu ila kila mmoja atabeba mzigo wake.

“Kwa sasa nawaza kukuza muziki wangu kwa namna moja au nyingine, siwezi kuendelea kuwawazia watu wakati mwenyewe nina mambo mengi ya kujiwazia,” alisema Diamond.

Alhamisi, 14 Januari 2016

Kimenuka!!! Zari aokoka na kubatizwa

Mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’

MUSA MATEJA, AMANI
DAR ES SALAAM: Siri nzito imefichuka baada ya kusitiriwa tangu mwaka juzi kwamba, mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah (35), mwaka huo aliokoka na akabatizwa kwenye kanisa moja la kiroho mjini Kampala, Uganda kisha kuwa muumini wa Kikristo, Amani limeinyaka. ILIKUAJE MPAKA AKAOKOKA? Kwa mujibu wa chanzo makini, Zari alifikia uamuzi wa kuokoka katika kipindi hicho mara tu baada ya kugombana na mumewe wa kwanza, Ivan Ssemwanga aliyezaa naye watoto watatu, Pinto, Didy na Quincy.
ALIBATIZWAJE?
“Nawapa ishu, mwaka juzi Zari aliokoka kabisa na kuwa Mkristo. Tena ili kuwapa uhakika, baada ya kukata shauri la kuokoka, alibatizwa kwenye maji mengi ya bwawa la kutengeneza. Maandiko ya Biblia yanasema mtu akiokoka lazima abatizwe kwenye maji mengi, yawe ya bwawa, kisima, mto, ziwa hata baharini, sawa tu,” kilinyetisha chanzo
chetu.

Zari akibatizwa.

ALIANDIKWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI?
Baada ya kuchukua hatua hiyo, mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vya kielektroniki na magazeti nchini humo viliripoti kwa vichwa vya habari; I AM NOW BORN AGAIN- SAYS ZARI (Zari: Sasa nimeokoka), ZARI IS NOW BORN AGAIN(Zari sasa ameokoka).

MWENYEWE ALISEMA NENO?
Kwa upande wake, kwa mujibu wa chanzo chetu, Zari baada ya kuchukua uamuzi huo, alitupia maneno na picha kwenye mitandao yake ya Twitter na Facebook akisema: “Ni rasmi sasa nimeokolewa.” Zari alionesha ni jinsi gani anampenda Yesu Kristo kwa vile alimuweka kwenye mwanga mpya. Alisema: “Mwenyezi Mungu kama siku moja nitapoteza matumaini, nipe ujasiri ambao hatima yangu ipo mikononi mwako. Sasa nayaona maisha katika mwanga mpya.”

ALIANZA KUYAJUA MAANDIKO?
Mama Tiffah ambaye pia huimba nyimbo za Kizazi Kipya na pia mama wa watoto wanne, Pinto, Didy, Quincy na Tiffah aliyezaa na Diamond alionesha uwezo wake wa kiimani kwa kutupia maandiko kutoka ndani ya Biblia kwenye Twitter yake huku akiendelea kumsifu Mungu na Yesu Kristo kwa kumuokoa.

CHA KUSHANGAZA SASA
Chanzo kilisema kuwa, baadaye Zari aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo kuwa, anatoka kimapenzi na Diamond, wengi walihoji alikouacha ulokole wake na ‘kurejea’ duniani.

“Mbaya zaidi, nasikia hata wachungaji wake waliposikia walishangaa sana. Walijaribu kumtafuta ili wamwelekeze namna ya kuukulia wokovu lakini bila mafanikio. Zari akawa amegandana na Diamond mpaka mimba na hatimaye kujifungua,” kilisema chanzo.

ANGETANGAZA KUACHA ULOKOLE NA KUWA NA DIAMOND?
Chanzo kikaendelea: “Nadhani walichotaka wachungaji wake ni kumrejesha Zari kundini, lakini si kutangaza kwamba ameamua kurejea maisha ya zamani. Ni vigumu sana. Hakuna anayeokoka kisha akatangaza akiacha.” Hata hivyo, chanzo hicho hakikujua jina la kanisa alilopatia wokovu Zari licha ya kusema waliombatiza ni watumishi wa Mungi Wazungu wa mjini Kampala.

HISTORIA FUPI YA UZAZI WA ZARI
Mpaka anabatizwa, Zari alikuwa akijulikana kwa jina la Zarinah Zaituni Hassan Tiale na aliendelea kutumia jina la Zari. Ana mchanganyiko wa kimataifa. Babu yake mzaa mama yake (Halima) ni Mhindi, bibi Mganda. Babu yake mzaa baba ni Msomali, bibi Mrundi.

DIAMOND AAMBIWA, ATOA TAMKO
Kufuatia Zari mwenyewe kuwa Uganda na kutopatikana hewani, gazeti hili lilizungumza na Diamond kuhusu ishu hiyo ambapo aliamua kulitolea tamko: “Najua lakini sina pingamizi na hilo. Mimi siangalii imani ya mtu, kinachotakiwa ni mapenzi ya dhati tu.”

Miss TANZANIA apewa Talaka

Miss Tanzania 2011, Salha Israel.

IMELDA MTEMA, AMANI
DAR ES SALAAM:Ndoa ya Miss Tanzania 2011, Salha Israel aliyofunga na Abdulatif Fundikira ‘Tiff’ ambaye ni mtalaka wa mwanamitindo Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ aliyeko gerezani kwa msala wa madawa ya kulevya huko Macau, China, inasemekana kuingia mdudu mbaya baada ya mrembo huyo kudaiwa kupewa talaka moja.

Kwa mujibu wa chanzo makini, kumekuwa na kutoelewana kati ya wanandoa hao, jambo ambalo limewafanya kuwa kwenye sintofahamu kila wakati huku wakimsaka mchawi wa ndoa yao.

Salha Israel akiwa na mumewe.

“Awali wale watu walikuwa wanapendana sana lakini cha ajabu kumekuwa na migogoro midogomidogo kwenye ndoa yao hadi kufikia wakati wenyewe wanajiuliza mchawi ni nani ilihali wao wanaonekana wanapendana sana,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao.

Baada ya ishu hiyo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alianza kwa kumsaka Tiff ambaye alipoulizwa kuhusu taa nyekundu kuiwakia ndoa yake alifunguka kuw anachokijua yeye ni kwamba amepata mke mwema lakini kuna watu wanataka kumharibia ndoa yake huku akimwachia Mungu kumsimamia. “Hakuna asiyejua kama mimi nimepata mke mwema sana lakini kuna watu hawapendi kuona ndoa yangu inaendelea.

Mimi namuachia Mungu kwani yupo pamoja nasi siku zote,” alisema Tiff huku akishindwa kukubali au kukataa kumtwanga talaka Salha. Salha na Tiff walifunga ndoa ya siri ya kiserikali mwaka 2014, nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini Dar, mwaka 2014