DAR ES SALAAM: Hii dharau! Siku chache baada ya staa wa Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kudaiwa kushika ujauzito ambao mhusika bado ni fumbo, balaa limezuka kufuatia Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2015, Idris Sultan kudaiwa kumtusi zilipendwa wa mrembo huyo, Mbongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Risasi Jumamosi linakujuza.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, Idris amekuwa akijitapa mitaani kuwa yeye ndiye kidume aliyeweza kumpa mimba Wema na kwamba ni daktari bingwa wa magonjwa sugu, yakiwemo ya uzazi kwani kwake kunapatikana tiba mbadala.
Majigambo hayo yanadaiwa kuharibu urafiki uliokuwepo baina ya wawili hao, kwani Diamond anachukulia kama ni kumtusi kwa vile aliwahi kujihusisha kimapenzi na Wema kwa muda mrefu bila kupata ujauzito.
Diamond na Wema Sepetu, enzi zilee.
KAMA KUNA URAFIKI NI KIINI MACHO
“Kitu ambacho watu hawaelewi ni kwamba hivi sasa urafiki wa Diamond na Idris ni kiini macho tu, kwani majivuno ya Idris ya kutoka na Wema yameleta uhasama mkubwa, hasa baada ya kujigamba kuwa ameweza kumpa ujauzito.
“Inadaiwa juzikati Idris akiwa na Wema sehemu, rafiki zake wakawa wanampongeza kwa taarifa zilizosambaa kuwa yeye ndiyo amemdunga mimba mrembo huyo ambapo kijana huyo alisikika akisema hakuna mwanamke asiyezaa duniani, isipokuwa kinachotokea ni kuto-match (kuendana) kwa damu za wawili. Eti kwa kitendo hicho yeye ndiye kidume cha mbegu,” kilisema chanzo hicho.
OMMY DIMPOZ NAYE ATAJWA
Ommy Dimpoz ambaye ni rafiki wa karibu wa Diamond, naye anatajwa kuwemo katika watu wanaompiga vijembe kwa kufurahia kitendo cha Idris kumjaza mimba Wema kwa kile kinachosemwa kuwa wawili hao wana ka-bifu ka chini kwa chini, kisa kikiwa siri yao.
“Ommy Dimpoz naye ni miongoni mwa watu wanaosapoti kwa asilimia kubwa Idris kumpachika mimba Wema na kwamba anaonesha wazi kuunga mkono kila kitu kinachofanywa na kijana huyo katika kumuumiza Diamond kupitia mimba hiyo.”
DIAMOND ANASA UBUYU
Habari zinasema kuwa maneno yaliyokuwa yakitembea katika kundi la Idris yalimfikia staa huyo wa muziki wa kizazi kipya nchini, ambaye alisikitishwa na kitendo cha kuonekana kama hakuwa na uwezo wa kumpa mimba Wema, akitamka kuwa wanaomsema hivyo hawajui jinsi yeye na Wema walivyokuwa wakiishi kimapenzi.
IDRIS HUYU HAPA, MSIKIE
Baada ya kumegewa ubuyu huo, juzi paparazi wetu alimtafuta mshindi huyo wa BBA aliyejishindia dola 300,000 (zaidi ya shilingi milioni 500) na kubahatika kukutana naye ana kwa ana katika eneo moja, nje kidogo ya jiji.
Alipoulizwa kuhusu ukweli wa madai ya kumtusi rafiki yake huyo, huku akichekacheka, Idris alishindwa kufunguka moja kwa moja, badala yake akasema hategemei kuja kuwa na tatizo na Diamond kwa sababu ya ujauzito wa Wema, hasa kwa kuwa tayari ana mtoto (Tiffah) aliyempata kwa mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Diamond hawezi kuwa na mawazo hayo kwani haoni tatizo lolote kwangu kuwa karibu na Wema, hata nikizaa naye, kwa sababu uhusiano wao ulishamalizika.
“Hata hivyo hayo yatabaki kama madai. Mimi kuitwa kidume itatokana na namna waitaji watakavyokuwa wamenichukulia. Ila kiukweli sidhani kama kuna mtu anaweza kuja kuninunia kisa Wema maana suala la uhusiano au kuwa karibu na mtu inategemea tu na watu wenyewe jinsi wanavyoweza kuchukuliana na kuwaziana.”
KUANIKA KUHUSU MIMBA YA WEMA
“Suala la mimba ya Wema nitakuja kuliweka vizuri baada ya mwezi mmoja. Kwa sasa niache kwanza maana nina mambo mengi ya kufanyia kazi, sitaki kabisa kuanza kuvuruga mudi za watu na ndiyo maana naona hakuna haja kwa muda huu kuongelea ishu hiyo ila yasemwayo yanaweza kuwa na maana kama yameelezewa vizuri,” alisema Idris.
Mbongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’.
DIAMOND NAYE HUYU HAPA
Gazeti hili lilifanikiwa pia kumnasa mkali wa kibao cha Utanipenda? Diamond ambaye baada ya kuelezwa kilichopo alisema kwa sasa hana muda wa kusikiliza maneno ya watu wala kujibu kila anachosikia, zaidi anahangaikia maisha yake ili kuweza kufikia ndoto alizojipangia kwa vile maneno yapo kila siku na hayaepukiki.
“Dah! Mimi sioni kama kuna kitu cha ajabu wala kuzungumzia hapo, zaidi naweza kusema mimi sina muda tena wa kuanza kuzungumzia mtu ila kila mmoja atabeba mzigo wake.
“Kwa sasa nawaza kukuza muziki wangu kwa namna moja au nyingine, siwezi kuendelea kuwawazia watu wakati mwenyewe nina mambo mengi ya kujiwazia,” alisema Diamond.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni