Jumapili, 17 Januari 2016

Diamond na Allykiba vipi tena???

Nasibu Abdul ‘Diamond Platmumz’.

DAR ES SALAAM! Kutokana na mwenendo wa bifu lao la chini kwa chini ni dhahiri mafahari wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platmumz’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ wamefika pabaya kwani safari hii zimeibuka tuhuma za kuzibiana riziki kimataifa, Ijumaa Wikienda linashuka na mchapo kamili.

Chanzo makini kimeeleza kuwa, Team Kiba ambao umoja wao unaonekana zaidi katika Mtandao wa Instagram, wamecharuka vibaya wakimtuhumu Diamond kuwa anawasiliana na vituo vya kimataifa kama MTV na kuwaambia wasipige nyimbo za King Kiba.

Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.

“Jamaa hafanyi fea, anawasiliana na wale wa vituo vya kimataifa na kuwaambia wasipige nyimbo za Kiba, anamzoofisha kweli,” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.

Mara baada ya kusambaa kwa taarifa hizo za Diamond ‘kumficha’ mwenzake kimataifa, Team Kiba na Team Diamond walianza kuporomosheana matusi mazito mtandaoni.

Team Kiba waliapa kufanya ziara nchi nzima kushinikiza Diamond aache ubaguzi huku Team Diamond wakimtetea msanii wao wakisema si kweli kwamba anafanya hivyo bali amekuwa akiwasaidia wasanii wengi hivyo Team Kiba wanatapatapa.

Baada ya ubuyu huo kutua mezani, mwanahabari wetu alimsaka King Kiba kupitia simu yake ya mkononi ambapo alisema kama kweli vituo hivyo vinamsikiliza Diamond, vitakuwa havimtendei haki.

“Kama kweli MTV watakuwa wanampatia jukumu Diamond la kupitisha ngoma zetu basi watakuwa hawafanyi fea, sidhani kama ni kweli wanafanya hivyo na Diamond anaweza kufanya hivyo,” alisema Kiba.

Akijibu tuhuma hizo mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond alikaririwa katika Televisheni ya Taifa (TBC 1), akielezea namna ambavyo amekuwa akisikitishwa na watu kumwambia anawabania baadhi ya wasanii kupigwa kimataifa na kusema wanamuonea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni