Mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’
MUSA MATEJA, AMANI
DAR ES SALAAM: Siri nzito imefichuka baada ya kusitiriwa tangu mwaka juzi kwamba, mzazi mwenzake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah (35), mwaka huo aliokoka na akabatizwa kwenye kanisa moja la kiroho mjini Kampala, Uganda kisha kuwa muumini wa Kikristo, Amani limeinyaka. ILIKUAJE MPAKA AKAOKOKA? Kwa mujibu wa chanzo makini, Zari alifikia uamuzi wa kuokoka katika kipindi hicho mara tu baada ya kugombana na mumewe wa kwanza, Ivan Ssemwanga aliyezaa naye watoto watatu, Pinto, Didy na Quincy.
ALIBATIZWAJE?
“Nawapa ishu, mwaka juzi Zari aliokoka kabisa na kuwa Mkristo. Tena ili kuwapa uhakika, baada ya kukata shauri la kuokoka, alibatizwa kwenye maji mengi ya bwawa la kutengeneza. Maandiko ya Biblia yanasema mtu akiokoka lazima abatizwe kwenye maji mengi, yawe ya bwawa, kisima, mto, ziwa hata baharini, sawa tu,” kilinyetisha chanzo
chetu.
Zari akibatizwa.
ALIANDIKWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI?
Baada ya kuchukua hatua hiyo, mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vya kielektroniki na magazeti nchini humo viliripoti kwa vichwa vya habari; I AM NOW BORN AGAIN- SAYS ZARI (Zari: Sasa nimeokoka), ZARI IS NOW BORN AGAIN(Zari sasa ameokoka).
MWENYEWE ALISEMA NENO?
Kwa upande wake, kwa mujibu wa chanzo chetu, Zari baada ya kuchukua uamuzi huo, alitupia maneno na picha kwenye mitandao yake ya Twitter na Facebook akisema: “Ni rasmi sasa nimeokolewa.” Zari alionesha ni jinsi gani anampenda Yesu Kristo kwa vile alimuweka kwenye mwanga mpya. Alisema: “Mwenyezi Mungu kama siku moja nitapoteza matumaini, nipe ujasiri ambao hatima yangu ipo mikononi mwako. Sasa nayaona maisha katika mwanga mpya.”
ALIANZA KUYAJUA MAANDIKO?
Mama Tiffah ambaye pia huimba nyimbo za Kizazi Kipya na pia mama wa watoto wanne, Pinto, Didy, Quincy na Tiffah aliyezaa na Diamond alionesha uwezo wake wa kiimani kwa kutupia maandiko kutoka ndani ya Biblia kwenye Twitter yake huku akiendelea kumsifu Mungu na Yesu Kristo kwa kumuokoa.
CHA KUSHANGAZA SASA
Chanzo kilisema kuwa, baadaye Zari aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo kuwa, anatoka kimapenzi na Diamond, wengi walihoji alikouacha ulokole wake na ‘kurejea’ duniani.
“Mbaya zaidi, nasikia hata wachungaji wake waliposikia walishangaa sana. Walijaribu kumtafuta ili wamwelekeze namna ya kuukulia wokovu lakini bila mafanikio. Zari akawa amegandana na Diamond mpaka mimba na hatimaye kujifungua,” kilisema chanzo.
ANGETANGAZA KUACHA ULOKOLE NA KUWA NA DIAMOND?
Chanzo kikaendelea: “Nadhani walichotaka wachungaji wake ni kumrejesha Zari kundini, lakini si kutangaza kwamba ameamua kurejea maisha ya zamani. Ni vigumu sana. Hakuna anayeokoka kisha akatangaza akiacha.” Hata hivyo, chanzo hicho hakikujua jina la kanisa alilopatia wokovu Zari licha ya kusema waliombatiza ni watumishi wa Mungi Wazungu wa mjini Kampala.
HISTORIA FUPI YA UZAZI WA ZARI
Mpaka anabatizwa, Zari alikuwa akijulikana kwa jina la Zarinah Zaituni Hassan Tiale na aliendelea kutumia jina la Zari. Ana mchanganyiko wa kimataifa. Babu yake mzaa mama yake (Halima) ni Mhindi, bibi Mganda. Babu yake mzaa baba ni Msomali, bibi Mrundi.
DIAMOND AAMBIWA, ATOA TAMKO
Kufuatia Zari mwenyewe kuwa Uganda na kutopatikana hewani, gazeti hili lilizungumza na Diamond kuhusu ishu hiyo ambapo aliamua kulitolea tamko: “Najua lakini sina pingamizi na hilo. Mimi siangalii imani ya mtu, kinachotakiwa ni mapenzi ya dhati tu.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni