Alhamisi, 28 Aprili 2016

Vote FOR MULASHAN PHILIPO F

✳UPCOMING HALL SIX G/SECRETARY ✳

Vote for ✅MULASHAN PHILIPO F.✅

 

  Kwania njema ya kuboresha mazingira na kutatua matatizo mbalimbali yanayotukumba wakazi wa hall six, nimeamua KUGOMBEA nafasi hii ya UKATIBU, .....✔NAOMBA KURA YAKO ✔

Kwa kushirikiana na atakayekuwa mwenyekiti nitafanya yafuatayo 

    1⃣TATIZO LA KUNGUNI. 

Nikiwa katibu nitapigania kwa uwezo wangu wote kwa kushirikiana na viongozi wengine na nitahakikisha magodoro yote yanapuliziwa dawa na kutokomeza tatizo hilo la kunguni. 

     2⃣MAJI. 

Tunahitaji maji kwa matumizi mbalimbali, ila kwa masikitiko makubwa hapa hall six mara kwa mara upatikanaji wa maji unakuwa ni wa shida ukilinganisha na halls nyingine. Hili tatizo linatokana na kutokujazwa kwa matank kwa wakati. Ukinipa kura yako nitashughulikia jambo hilo kwa nguvu zangu zote. 

     3⃣USAFI.

Nitahakikisha usafi unafanyika kikamilifu na kwa muda unaofaa, pia nitahakikisha sabuni na dawa vinatumika ili kuzuia magonjwa ya mlipuko. 

     4⃣UKARABATI WA MIUNDOMBINU. 

Tunaishi na kutumia miundombinu zilizochakaa, nitahakikisha kwa kila kitu kilichoharibika ndani ya bweni kitafanyiwa ukarabati kwakuwa pesa tunayolipia kwaajili ya kukaa inatosha kufanya ukarabati wa vitu mbalimbali ambavyo vinaharibika. 

    5⃣KUIMARISHA ULINZI. 

Ninahitaji kuimarisha ulinzi hapa hall six na hasa barabara yakutokea yombo mpaka stendi ya kontenda. Nitaanzisha ulinzi shirikishi ili kupunguza wizi

     6⃣UPATIKANAJI WA TAARIFA JUU YA MAMBO MBALIMBALI 

Nitahakikisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali kwa wanafunzi, hasa linapotokea tatizo lolote kama kukatika kwa maji, umeme n.k kama likiwa endelevu mara kwa mara. Na pia nitatoa number ya simu kwa kila mkazi wa hapa ili atoe taharifa endapo tatizo lolote litatokea kwa muda wowote na litatatuliwa au kupelekwa sehemu husika



    ✅Naomba kura yako wewe mkazi wa hall six, ili uweze kunipa fursa mimi MULASHAN PHILIPO FESTO kukufanyia kazi kwa maendeleo yetu wakazi wa hall six. Weka ✅ jina langu litakuwa number mbili. ✅#⃣2⃣✅

 .."Ewe mkazi wa hall six nipo tayari unitume mimi ili niweze kukutumikia kwa maendeleo yetu".. ASANTE SANA 🙏🏿

Jumatatu, 25 Aprili 2016

Video Inayoonyesha Papa Wemba Jinsi Alivyodondoka Jukwaani

Papa Wemba 


Video inayoonyesha jinsi Papa Wemba Alivyodondoka Jukwaani Nchini IvoryCoast.Mungu Ailaze Roho yake mahali Pema Peponi Ameen.   

       

Historia Fupi Ya Papa Wemba hii hapa>>>>

ImageCourtesyImageHistoria ya Papa Wemba

Habari kuwa mmoja wa vigogo wa muziki wa kiafrika Papa Wemba ametutangulia mbele ya haki imepokewa kwa mshtuko mkubwa na mashabiki wake kote duniani.

Video inayosambazwa katika mitandao ya kijamii inamuonesha Papa Wemba akiendelea na kazi yake anayoifahamu zaidi ya uimbaji kisha anaonekana akianguka ghafla jukwaani.

Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba 1949-2016.

Wanabendi wake waliokuwa jukwaani naye huko Abidjan katika tamasha la muziki la #FEMUA wanaendelea kupiga densi tu kabla ya mmoja wao kukimbia kumuokoa baada ya kuona kasalia chini kwa sekunde kadhaa akiwa anatetemeka kisha akazirai.

Shoo hiyo ya Papa Wemba ilikuwa moja katika mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan.

Msemaji wake Henry Christmas Mbuta Vokia, ameiambia Radio Okapi kuwa

''Marehemu Papa Wemba alikuwa ameingia muda mchache tu jukwaani kisha akacheza wimbo wa kwanza, mashabiki wakamuomba awaimbie tena wimbo mwengine akakubali.

lakini dakika chache tu baada ya kuanza kupiga wimbo wa ke wa tatu Papa Wemba alianguka na kuzirai ghafla jukwaani''

Watu wa shirika la msalaba mwekundu walijaribu kumsaidia lakini hakuonesha dalili nzuru kwa hivyo wakampeleka hospitalini kwa dharura lakini baada ya dakika karibu thelathini hivi tukaambiwa kuwa Papa Wemba ametuacha''

Alisema Mbuta Vokia.

Msanii huyo nguli alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Soukus nchini DRC na kote duniani kwa kipaji chake cha kipekee na sauti isiyokuwa na mfano.

Wengi waliitambua sauti hiyo ya na utunzi wake.

Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.

Ni mweledi wa kuimba kucheza ala za muziki na pia kusakata rhumba yaani kunengua kiuno.

Lakini je Papa wemba ni nani ?

Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba.

Yeye alianza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo mno.

Alikuwa akimfuata mamake katika matanga na hivyo akaibukia kuwa mtunzi wa nyimbo za kuomboleza.

Alitunga wimbo wake wa kwanza "Madrigal" akiwa na umri wa miaka

Shungu Wembadio alijiunga na kundi la ''Stukas'' kabla ya kuliacha na kuunda kundi kubwa la Zaiko lana langa mwaka huohuo wa 1969.

Zaiko LangalangaSauti yake ya kipekee na uweledi wake uliisaidia kundi hilo katika utunzi wa "Pauline", "Chouchouna", "Liwa is somo".

Wemba wakati huo alijiunga na wanamuziki wenza wa Zaire (Congo ilivyojulikana wakati huo) Nyoka Longo Jossart, Manuaku Pepe Felly, Evoloko Lay Lay, Bimi Ombale, Teddy Sukami, Zamuangana Enock, Mavuela Simeon, Clan Petrole miongoni mwa wengine.

Wakati huo akianza Papa Wemba , jukwaaa la muziki nchini humo lilikuwa limetawalwa na vigogo wa muziki Franco Luambo wa TPOK Jazz, Tabu Ley Rochereau wa Afrisa, na makundi mengine mapya kama vile Les Grands Maquisards, Le Trio Madjesi, Bella-Bella, Thu Zaina na Empire Bakuba.

Hata hivyo sauti ya kipekee ya Papa Wemba akijulikana wakati huo kwa majina yake kamili Jules Presley Shungu Wembadio ilikonga mioyo ya wapenzi wa Soukus.

Kilele cha ufanisi wa kundi la Zaiko Langa Langa ulikuja miaka ya mapema ya sabini.(1973)

Hapo ndipo Shungu alibadili jina lake na kuanza kuitwa jina la utani ''Papa Wemba''.

Yolele

Miaka mitano baadaye aliihama kundi hilo na kujiunga na "Isifi Lokole" hapo alitunga wimbo maarufu wa "Amazon", wimbo aliokiri kumtungia mkewe.

Mwaka huo hakutulia lengo lake la kupambana na vigogo wa muziki nchini Zaire haikuwa imekamilika.

Alijiunga na kundi lingine la "Yoka Lokole", kabla yake kuunda kundi lake sasa la "Viva La Musica" mapema mwaka wa 1977.

Vibao vyake ni kama Mwasi,Show me the way, Yolele, Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo. ,Emotion,Wake Up, Wake Up,Maria Valencia, Le Voyageur,Rail On, Kaokokokorobo ,Legend

Jela

Papa Wemba aliwahi kukamatwa kwa madai ya ulanguzi wa binadamu.

Tarehe 18 mwezi Februari 2003 maafisa wa idara ya upelelezi nchini Ufaransa walimkamata Papa Wemba kwa tuhuma za kuwaingiza raia wa Zaire (kama ilivyoitwa wakati huo DRC) barani ulaya kinyume cha sheria.

ImagePapa Wemba

Mahakama ya ubelgiji ilimpata na hatia mwezi Juni mwaka wa 2003 na ikamhukumu kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitatu jela.

Aidha mahakama hiyo ya Brussels ilimpiga faini ya euro 22,000.

Hata hivyo alitumikia kifungo cha miezi mitatu u nusu gerezani baada ya mdhamini kulipia dhamana ya Euro €30,000.

Alipoachiwa huru aliwaambia mashabiki wake kuwa aliyokumbana nayo akiwa gerezani yamemfunza mengi tu.

Katika utunzi wa wimbo wake "Numéro d'écrou" (2003)Papa Wemba anasimulia kukutana na mwenyezi Mungu akiwa gerezani.

Aidha anasema kuwa alibadilishwa mawazo na dini akitumikia kifungo.

Jumapili, 24 Aprili 2016

Papa Wemba Afariki Dunia Akiwa jukwaani

Papa Wemba Enzi za Uhai wake 

ImagePapa Wemba ameaga dunia

Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba amefariki dunia

Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.

Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,

Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.

ImagePapa Wemba alianguka katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.

Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa akitumbuiza jukwaani Abidjan.

Papa Wemba Akiwa Amezirai jukwaani muda mfupi baada ya kudondoka.

Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.

Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele, Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo

Jumatano, 20 Aprili 2016

VOTE for KHOMEIN HAMIS


ELECTION JUST GOT REALLY!

 when it comes choosing a leader,we all take a leader who will serve and attend to all our needs and wants in a best possible manner.A leader with the  ability to multi task and comprehend the issues that need his direct involvement,willing to sacrifise his  needs for sake other people's needs.In opening this campaign,i would to present a man whom i am proud to stand along in this run as his campaign manager,but most of all as his close friend ,you all know him,his name is KHOMENI HAMISI. I place my faith on him to be capable of taking this,he did and is still doing  well as a CR  ,i am sure he can be a good university student representative councillor for first year student .I personally like to save the best for last,I need not to say much but we just got started.

             PS:YOUR VISION ,MY MISSION

  well approved and recommed advert by

     KHOMENI HAMISI (running candidate for USRC and still the current CR of udbs first year)

Your vission his mission

Vote for khomein Hamis as your USRC Personally i know him ana a great experience of leadership since his childhood 

Anajitambua anajiamini anaweza we have seen his work as a cr throughout the previous semester

Khomein ni kiongoz ambaye ana weledi wa mambo mbalimbali na uwezo wa kitatua matatizo ya wanachuo and the school at large

Amekua ni kiongoz wa kutafuta solutions rather than kulalamika kwa wana udbs this shows his competence 

Kama utakua haumfahamu vzur basi refer to the pic above then vuta picha na umkumbuke cr #3 mwnye sauti kubwa kuliko cr yeyote wa first year🔥

"YOUR VISION MY MISSION" Vote for Khomein✅💯

New Upcoming Artist 'SPONSE' Anaachia Nyimbo yake soon

Huyu ni msanii mpya kabisa katika industry ya muziki huu wa kizazi kipya,BONGOFLEVA msanii huyu anakwenda kwa jina la SPONSE ambae hivi karibuni atatambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina 'Nalia na wewe'. Sponse itaielezea zaidi ngoma hii ikishatoka official kabisa kwa mara ya kwanza hapahapa MUNISHIJR tutafanya nae interview na stori mbili tatu

Sponse ambae pia ni mwanafunzi katika CHUO KIKUU CHA ARDHI (ARDHI UNIVERSITY) Mjini Dar-es-salaam.Anahitaji support yako wewe kama mdau wa muziki iliaweze kufika level za juu ambazo anazitaka yeye as long as muziki wetu unakua kwa kasi ya ajabu kwaio basi anatumaini atapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwako 

Sponse ameanza kuimba tangu yupo shule anasoma,kwaio kwa mfano inatoke event pale shule bhasi yeye hupata nafasi kupanda jukwaani na kuanza kufanya yake.

Amekua mshindi mara nyingi tu kwenye majukwaa ya shuleni kama unavyoona kwenye picha hapo juu...

Hiyo nyimbo ikitoka tutamtafuta Sponse na kufanya mahojiano nao nae hapa Munishijr.

Jumapili, 17 Aprili 2016

Ronaldo 'HATTRICK MACHINE' Mvunja rekodi Ulaya

Christiano Ronaldo

ADVERTISEMENT

CHEZA na wachezaji wote, lakini usimchezee Cristiano Ronaldo linapokuja suala la Ligi ya Mabingwa. Anatisha kama njaa. Usibishe sana, rekodi zake zipo wazi na hat-trick ya juzi dhidi ya Wolfsburg ilikuwa ya tatu ndani ya msimu mmoja.

Hakuna mchezaji yeyote ambaye amewahi kufanya hivyo tangu kuanzishwa kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Lakini Ronaldo ana rekodi nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo itakusisimua na kumpigia saluti.

Ronaldo ni mchezaji pekee katika historia ya michuano hiyo kufunga mabao 15 na zaidi kwa misimu miwili mfululizo ikiwa ni baada ya kufunga mabao 17 msimu uliopita huku mabao yake matatu ya juzi yakimfanya afikishe idadi ya mabao 16 na anakaribia kuvunja rekodi yake mwenyewe.

Mashabiki wa Arsenal hawatapenda kuisikia hii. Ronaldo amefunga mabao matatu zaidi kuliko mabao yote ambayo Arsenal wamefunga katika Ligi ya mabingwa msimu huu. Mpaka sasa Arsenal wamefunga mabao 13 na wameshatolewa katika michuano.

Chelsea nao hawatapenda kuisikia hii. Mpaka sasa Ronaldo amefunga bao moja zaidi kuliko mabao yote ambayo Chelsea wamefunga katika Ligi ya Mabingwa msimu huu. wakati Ronaldo akiwa amefunga mabao 16, Chelsea imefunga mabao 15.

Kama vile haitoshi, Ronaldo ana rekodi ya kufunga mabao mengi kuliko idadi ya mechi katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Amefunga mabao 40 katika idadi ya mechi 35 za Ligi ya Mabingwa Ulaya zilizochezwa dimba la Santiago Bernabeu.

Hakuna mechi muhimu zaidi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kama mechi za mtoano. Ronaldo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 31, amefunga mabao 34 katika mechi 36 za mtoano za Madrid Ligi ya mabingwa Ulaya.

Kwa msimu huu, Ronaldo amezidi kuonyesha ubabe kwa wachezaji wenzake Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa sababu amefunga mabao manane zaidi dhidi ya mastaa wawili wanaomfukuzia ambao ni Luis Suarez na Roberto Lewandowski wenye mabao manane kila mmoja.

Kama vile haitoshi, wote wanaosema Ronaldo huwa hajitokezi katika mechi muhimu wanakosea sana. Ronaldo amefunga mabao 15 katika mechi za robo fainali Ligi ya Mabingwa wa Ulaya ukijumlisha na mabao matatu aliyofunga juzi.

Ronaldo anaongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa akiwa amefunga mabao 93 katika mechi 125 na hat trick yake ya juzi ilikuwa ya 37 tangu ahamie Madrid akitokea Manchester United kwa ada ya uhamisho wa dunia wa Pauni 80 milioni katika dirisha la majira ya joto mwaka 2009.

Kutokana na mabao yake ya juzi, Ronaldo ambaye msimu huu amejikuta katika wakati mgumu mbele ya mashabiki wake wa Santiago Bernabeu alijigamba kwamba mabao yapo katika damu yake na ataendelea sana kufunga.

“Haikuwa bora, lakini ulikuwa moja kati ya usiku wangu bora katika Ligi ya Mabingwa. Mabao yapo katika DNA yangu na nataka kuendelea kufunga kwa sababu ya timu,” alisema Ronaldo ambaye pia alizungumzia kuhusu rekodi yake ya upachikaji mabao.

“Ni wazi kwamba (Kufikia rekodi yake ya msimu uliopita) siyo kitu ninachokitafuta, lakini nina matumaini ya kuvunja rekodi hiyo na kufunga zaidi ya mabao 17. Itakuwa kitu kizuri. Itakuwa vizuri kwangu na kwa timu. Nitarajibu kadri niwezavyo,” alisema Ronaldo.

Jumamosi, 16 Aprili 2016

Filamu nyingine Ya AVATAR Kutolewa tena

Filamu ya kwanza ya Avatar ilitolewa 2009 na iliwashirikisha Sam Worthington na Zoe Saldana

Watengenezaji wa filamu ya Avatar franchise wamesema kutatolewa filamu zaidi katika mwendelezo huo wa filamu, filamu ijayo ikitarajiwa kutolewa 2018.

Mwelekezi wa filamu hizo James Cameron ametangaza kwamba filamu hizo zitaendelezwa hadi makala ya tano itakayotolewa 2023.

Alikuwa tayari amethibitisha kwamba filamu tatu zaidi zingetolewa lakini amefichua kwamba kuna mambo mengi sana ya kuelezwa kwenye hadithi hiyo na makala zijazo tatu hazitoshi.

Image20th Century Fox

Kote duniani, Avatar inasalia kuwa filamu iliyofanikiwa zaidi katika historia.

Filamu hiyo imezoa $2.7bn tangu kutolewa wake 2009.

Filamu ijayo ya Avatar itatoka 2018, na hizo nyingine 2020, 2022 na 2023

Barabara ya kwanza ya juu(FLYOVER) Kujengwa jijini DSM

ImageMradi wa ujenzi ukizinduliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara Jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018.

Sherehe ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika kando ya eneo la makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Mameya wa Jiji la Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida.

Barabara hiyo ya juu itakuwa ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake umepangwa kugharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.

Barabara ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema barabara hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali yake ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam, ambao kwa mwaka 2013 pekee utafiti umeonesha ulisababisha upotevu wa shilingi Bilioni 411.55

Rais Magufuli amebainisha juhudi nyingine za kukabiliana na msongamano wa magari Jijini Dar es salaam kuwa ni pamoja na kujenga barabara ya njia sita ya Dar es salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na Flyover tano, ujenzi wa barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo na ujenzi wa daraja jipya la Salander lenye urefu wa kilometa 6.23 kuanzia Coco Beach hadi hospitali ya Agha Khan.

Juhudi nyingine ni ujenzi wa awamu ya pili wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Kilwa, Chang'ombe na Kawawa, na ujenzi wa awamu ya tatu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Nyerere - Gongo la Mboto na Uhuru - Azikiwe.

Aidha, Rais Magufuli amezungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, kuwa serikali yake imelazimika kusimamisha kuanza kwa huduma hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa mzigo mzito wa viwango vikubwa vya nauli, na amewahakikishia wananchi wa Dar es salaam kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika.

Dkt. Magufuli pia amezungumzia usafi wa Jiji la Dar es salaam kwa kuwataka viongozi wa Manispaa zote za Jiji, kuhakikisha wanatafuta namna ya kudhibiti utupaji hovyo wa takataka ikiwemo kutoza faini kubwa kwa watakaokamatwa wakitupa takataka hovyo.

Tetemeko Laikumba Kumamoto Japan

ImageAPImageTetemeko hilo lilisababisha kuporomoka kwa majengo

Maafisa nchini Japan wanasema kuwa tetemeko kubwa la ardhi limewaua takriban watu 19 na kusababisha uharibifu mkubwa.

Tatemeko hilo ambalo ni la pili kukumba kisiwa cha Kyushu ndani ya siku mbili, limesababisha kuporomoka kwa majengo, limeharibu barabara pamoja na mifumo ya maji na umeme.

Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 7.3 kwenye vipimo vya Richter.

Tetemeko hilo la ardhi, ambalo chanzo chake ni kilomita 10 chini ya ardhi karibu na mji wa Kumamoto, lilikuwa kubwa na liliathiri eneo kubwa kuliko la kwanza lililotokea katika mji huo wa Kumamoto Alhamisi usiku.

ImageReutersImageWatu wengi wamejeruhiwa

Afisa wa serikali wa Kumamoto Tomoyuki Tanaka ameambia AP kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.

Wanajeshi 20,000 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji lakini jitihada za uokoaji zimetatizwa na mitetemeko mingine midogomidogo.

Waziri mkuu Shinzo Abe amekuwa na mipango ya kuzuru kisiwa cha Kyushi hii leo lakini safari hiyo imefutwa.

SudanKusini rasmi AfricaMashariki

Rais John Magufuli (Kushoto) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kulia) 

Dar es Salaam. Hatimaye Sudan Kusini imeingia rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Rais wa taifa hilo, Salva Kiir kusaini mkataba na Rais John Magufuli unaorasimisha taifa hilo kujiunga katika jumuiya hiyo.

Kwa mantiki hiyo, EAC ina jumla ya wanachama sita ambao ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na mwanachama mpya wa sasa, Sudan Kusini.

Rais Magufuli ambaye ndiye mwenyekiti wa EAC amesema  mkataba huo unafungua fursa muhimu kwa Watanzania za kibiashara na uchumi zilizopo katika taifa hilo lililojitenga kutoka Sudan miaka mitano iliyopita.

Rais Salva Kiir ameahidi kufanya mabadiliko makubwa nchini humo ili kuendana na mahitaji ya EAC ikiwemo kuimarisha amani, umoja na mshikamano katika taifa hilo changa lililokumbwa na mapigano ya wao kwa wao.

Rais Magufuli amesema atatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha safari ya Sudan Kusini katika kufikia hatua zilizofikiwa hadi sasa ndani ya EAC ikiwemo soko la pamoja.

Alhamisi, 14 Aprili 2016

OmbaOmba Waanza kusombwa jijini DSM

POSTED THURSDAY, APRIL 14, 2016 | BY- VICKY KIMARO, MWANANCHI VKIMARO@MWANANCHI.CO.TZ

Ombaomba waanza kusombwa

Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Dar es Salaam. Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.

Makonda alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.

‘Mchakamchaka’ wa kuwaondoa watu hao ulianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo.

Mwananchi ilizunguka maeneo mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa, lakini yalikuwa tupu.

Maeneo hayo ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu wa kundi hilo.

Mmoja wa ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari hizi katika maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa barabara, huku akisema: “Tumetoka Dodoma, hatutaki kurudi.”

Akizungumza na gazeti hili, Makonda alisema ikifika Jumatatu kama hawajajisalimisha Serikali itachukua hatua kali na kuwarudishwa walikotoka. “Kwanza ni kinyume cha sheria, pili ni hatari kwa maisha yao na watoto wanatakiwa warudi shule sasa,” alisema.

Kadhalika, operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.

Baadhi ya wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa wanachofanya ni kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.

Agizo la kutaka ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi kutolewa pia na waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, Abbas Kandoro na Said Mecky Sadiki

Jumapili, 10 Aprili 2016

Pacquiao Amchapa Bradley na Kustaafu Ndondi

ImageAFPImageManny Pacquiao amchapa Tim Bradley

Bondia Mfilipino Manny Pacquiao amemchapa bondia kutoka Marekani Tim Bradley katika pigano lake la mwisho.

Mfilipino huyo ambaye alishindwa katika pigano lake kuu dhidi ya bondia tajiri zaidi duniani Floyd Mayweather amekuwa bingwa katika vitengo mbali mbali katika kipindi cha miaka 21 iliyopita tangu alipoanza ndondi.

Pacquiao alishinda kwa wingi wa pointi katika pigano hilo lililokuwa likitazamiwa na wengi.

ImageAFPImagePacquiao alishinda kwa wingi wa pointi katika pigano hilo

Pacquiao, amekuwa mbunge tangu mwaka wa 2010.

Amesema kuwa anastaafu ndondi za kulipwa iliawahudumie wananchi kisiasa.

Mfilipino huyo mcha mungu na muaniaji kiti cha useneta nchini kwao alithibitisha udedea wake ulingoni alipomuadhibu vikali mmarekani huyo.

Jinsi ya kujua Simu Fake


1. Kabla hujanunua simu mpya hakikisha unaandika namba hii *#06#, kwenye simu hiyo au ambayo tayari umenunua.
2. Ukishaandika itaonyesha namba ya pekee (serial number) au IMEI (International Mobile Equipment Identity) ambayo ni lazima ziwe tarakimu 15 au zaidi na ni lazima ianze na 35.
3. Angalia kwa makini kama namba unazoziona zinafanana moja kwa moja na namba zilizoandikwa katika simu yako kwenye sehemu ambayo betri inakaa. Namba hizi zinapaswa kufanana kwa simu ambayo ni halisi. Kama hazifananani simu hiyo ni feki.
4. Tuma namba ya pekee (IMEI) kwenda namba 15090 na utapokea ujumbe mfupi unaoelezea kama simu yako ni orijino au feki.


KUJUA UBORA WA SIMU
1. Katika namba hizo namba ya sasa (7) na ya nane (8) ndizo zinazohakikisha ubora wa simu yako.
2. Kama namba ya saba na ya nane ni 00 ina maana kuwa simu yako imetengenezwa kwa ubora wa juu kabisa katika viwanda vya kuaminika.
3. Kama namba ya saba na ya nane ni 01 au 10 ina maana simu yako imetengenezwa Finland na ina ubora wa juu pia.
4. Kama namba ya saba na ya nane ni 13 ina maana simu yako imeunganishwa katika nchi za Azerbaijan na ni hatari kwa matumizi ya afya yako.
5. Kama namba ya saba na ya nane ni 02 au 20 ina maana simu yako imeunganishwa katika nchi ya Emirates na ina kiwango cha chini, lakini siyo feki.
6. Kana namba ya saba na ya nane ni kati ya 03 au 30 au 04 au 40 ina maana simu yako imentengenezwa China, lakini ina ubora mzuri ila haijafikia zile zenye 00, 01 au 10.
7. Kama namba yako ya saba na ya nane ni 05 au 50 ina maana simu yako imetengenezwa labda Brazil au USA ama Finland.
8. Kama namba ya saba na ya nane ni 06 au 60, simu yako imetengenezwa Hong Kong, China au Mexico.
9. Kama namba ya saba na ya nane ni 08 au 80, simu yako imetengenezwa Ujerumani na ina ubora wa kawaida

Jumatano, 6 Aprili 2016

Ufaransa Yapiga Marufuku Biashara ya Ngono

ImageAFPImageMnara wa Ufaransa

Bunge la Ufaransa limeidhinisha sheria mpya, inayopinga biashara ngono

Hatua hiyo inadaiwa kwamba huenda ikaathiri maisha ya watu zaidi ya elfu thelathini ambao wanategemea shughuli za ngono katika kujipatia kipato ambao wengi wao ni raia wa kigeni.

Chini ya sheria hiyo mpya, watu watakaokutwa wakilipia huduma hiyo wataadhibiwa kwa kulipa dola 1,700.

Mmoja wa mbunge anayeunga mkono sheria hiyo ameitetea na kusema kuwa inalengo la kuhamasisha watu kujiondoa katika biashara hiyo.

Hata hivyo kundi dogo la makahaba waliandamana nje ya bunge wakipinga sheria hiyo kwa madai kuwa wapewe uhuru wa kujilinda wenyewe na si kukatazwa kufanya biashara hiyo.

Jumanne, 5 Aprili 2016

Aubameyang Avunja rekodi Nchini Ujerumani

ImageapImageAubameyang amefunga mabao 23 Bundesliga msimu huu

Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amevunja moja ya rekodi za uchezaji soka nchini Ujerumani.

Mchezaji huyo kutoka Gabon ndiye mchezaji kutoka Afrika aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi kuu ya soka ya Ujerumani Bundesliga msimu mmoja.

Aubameyang, ambaye alitawazwa mchezaji bora wa mwaka 2015 Afrika wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) alifunga bao lake la karibuni zaidi dhidi ya Werder Bremen Jumamosi na kufikisha 23, idadi ya mabao aliyofunga msimu huu.

Rekodi ya awali ilikuwa ya mabao 22 na iliwekwa na Cisse Papiss wa Senegal msimu wa 2010/11.

Papiss kwa sasa huichezea Newcastle United ya Uingereza.

Samatta, Aubameyang majogoo wa AfrikaAubameyang:Yaya Toure aliniudhi sana

Msimu huu wa 2015/16 pia, Aubameyang alikuwa ameweka rekodi kwa kufunga bao katika kila mechi mechi nane za kwanza za msimu wa Bundesliga, akiipita rekodi ya awali kwa mechi mbili.

Kwa kuwa alikuwa amefunga mabao mechi mbili za mwisho za msimu wa 2014-15, alivunja rekodi nyingine ya kufunga mabao mfululizo katika mechi 10 za Bundesliga. Mtu pekee aliyekuwa ameifikia ni Klaus Allofs miaka 30 iliyopita.

Antonio Conte Kocha Mpya wa Chelsea

ImageAPImageConte kwa sasa ni meneja wa timu ya taifa ya Italia

Meneja wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea ya Uingereza, kwanzia mwisho wa msimu huu.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Juventus mwenye umri wa miaka 46 ataanza kutumikia mkataba wake wa miaka mitatu baada ya kuongoza Italia michuano ya Euro 2016.

"Ninajivunia kuwa kocha wa timu ya taifa langu na ni wadhifa wa kuvutia sana kama kuwa meneja wa Chelsea ambao unaweza kufuata,” amesema.

Conte kuacha kazi Italia, atahamia Chelsea?Jose Mourinho afutwa kazi ChelseaHiddink ateuliwa meneja mpya Chelsea

Guus Hiddink, aliyechukua majukumu baada ya Jose Mourinho kufutwa, ataendelea kunoa Blues hadi mwisho wa msimu.

Fainali za Euro 2016 zitachezwa 10 Julai.

Conte atakuwa Mwitaliano wa tano kuwa meneja wa Chelsea baada ya Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto di Matteo.

CUF:Hatumtambui Shein kama Rais

ImageChama cha CUF kilisusia uchaguzi wa marudio

Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimesema hakimtambui Dkt Mohamed Ali Shein aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi uliopita.

Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakizungumza kwa mara ya kwanza tangu kufanyika kwa uchaguzi huo ambao chama hicho kilisusia, wamesema hawamtambui Dkt Shein kama rais wa visiwa hivyo.

“Tangu mapema, tangu Jecha (Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha) alipofuta uchaguzi, tulisema waziwazi kwamba haikuwa halalali. Walipoitisha uchaguzi wa marudio, tulisema waziwazi uchaguzi huo sisi hatuutambui na tukawataka wananchi wasipige kura,” amesema Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad.

Bw Hamad alikuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na ambao matokeo yake yalifutwa na tume.

“Kama Rais ametokana na mchakato ambao hamkuutambua nyinyi tangu mwanzo, sasa leo kuja kusema hatumtambui kwa nini iwe ni haramu? Hatumtambui.”

Chama hicho kimesema kitatumia njia za kidemkrasia kulalamika dhidi ya Dkt Shein na serikali yake.

Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCCMabalozi wakosoa uchaguzi wa Zanzibar

Aidha, kimeiomba jamii ya kimataifa kuwawekea vikwazo watu binafsi waliofanikisha uchaguzi huo wa marudio ambao chama hicho kimesema ulikuwa “uongozi haramu”.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama Twaha Taslima amesema chama hicho hakiko tayari kuwa sehemu ya serikali mpya.

"CUF haitoshirikiana na serikali itakayoundwa kwa sababu ni kinyume na katiba ya Zanzibar, kinyume na sheria ya uchaguzi na haikutokana na ridhaa ya watu," amesema.

Wiki iliyopita, Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC) lilisitisha ufadhili wa $472milioni kwa Tanzania likilalamikia uchaguzi visiwani Zanzibar na utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.

Pesa hizo zilikuwa za kutumiwa katika miradi ya kusambaza umeme.

CUF imesema upo uwezekano wa kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo ka ikiwa uchaguzi huo utarudiwa basi usimamiwe na ujumbe wa kimataifa kwani wasimamizi wa ndani wamepoteza uhalali

Chama tawala visiwani humo kimebeza tamko hilo la CUF ana kusema kuwa Wazanzibari ni watu makini na kwamba hawawezi kumnyima ushirikiano Rais wao ambaye anafanya kazi kuwaletea maendeleo

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai ameiambia BBC kwamba Rais Shein anao pia uwezo wa kutengeneza serikali hata bila ushiriki wa chama cha CUF

"CUF wanafanya upotoshaji. Katiba haijamfunga Rais kukamilisha utengenezaji wa serikali yake. Na hivi tunapozungumza, muda si mrefu atakamilisha serikali yake na atajumuisha Wazanzibari na kufanya nao kazi" alisema Vuai.

Hii ni mara ya kwanza kwa Chama cha CUF kutoa tamko tangu kurudiwa kwa uchaguzi ambao waliususia

Jumapili, 3 Aprili 2016

Mtoto Avutishwa Bangi,Alawitiwa

Bibi wa mtoto huyo.

NA GLADNESS MALLYA
Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Huu ni ukatili wa kutisha! Mtoto mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa) mkazi wa Mji Mpya, Kata ya Saranga jijini Dar, amedaiwa kufanyiwa ukatili wa kuvutishwa bangi, kunyweshwa madawa ya kulevya kisha kulawitiwa na kijana aliyetambulika kwa jina la Ibrahimu.

Akizungumza kwa huzuni, mtoto huyo alisema kijana huyo humuita akiwa anacheza na kumpeleka chumbani kwake ambako humlewesha kwanza ili kumpoteza fahamu, lakini anapozinduka hujikuta amelawitiwa.

Eneo anakoishi mtuhumiwa.

“Ibrahimu alikuwa akinivutisha bangi, anachukua maji anachanganya na unga ananinywesha kwa lazima, akishamaliza hivyo nakuwa sijielewi ndipo anaponilalia na kunifanyia vitendo hivyo.

“Alikuwa akinipa hela, siku ya kwanza alinipa 2,400 akaniambia nisiseme, nikisema ataniua, hivyo nikawa nanyamaza, sikuwaambia bibi wala babu, siku nyingine alinituma nije nichome nyumba ili wafe, anichukue nikakae naye kwake, nikaja nikawasha moto lakini walishtuka na kuja kuuzima,” alisema mtoto huyo.

Babu wa mtoto huyo aitwaye Daudi, alisema aligundua kwamba mjukuu wake hayupo sawa kutokana na kushindwa kutembea vizuri pamoja na kushindwa kukaa ndipo alipoamua kumkagua na kukuta ameharibika vibaya sehemu za siri.

Mtoto anayedaiwa kuvutishwa bangi na kulatiwa.

Baada ya kushuhudia tukio hilo, alikwenda kutoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi aliyemtaja kwa jina moja la Said, Novemba mwaka jana, lakini hakuna hatua zozote alizochukua zaidi ya kuwaambia anafanya uchunguzi.

“Kiukweli mjukuu wangu alikuwa anatembea kwa shida, nguo alizovaa zilichafuka sana na akienda chooni alitoa damu, kitu kilichombadili tabia, akaanza kuwa mkorofi huku akisinzia kama teja.

“Ilibidi bibi yake arudi tena kwa mjumbe wa nyumba kumi ambaye alimpa barua na kupeleka ya serikali za mtaa, maana sisi tulishindwa kwenda polisi.

“Tuangalie sisi tumeshakuwa watu wazima, tumeshindwa tufanyeje, tunaomba msaada kwa Watanzania wenzetu watusaidie ili huyu kijana akamatwe maana anamtuma huyu mtoto aje atuchomee moto huku ndani, tunaishi kwa wasiwasi sana,” alisema babu huyo.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mji Mpya, Daniel Mumba alithibitisha kupokea barua ya mjumbe ambapo alimhoji mtoto na kumweleza vitendo hivyo vya kikatili anavyofanyiwa na kuchukua jukumu la kwenda nao katika Kituo cha Polisi Kimara Temboni na kufungua kesi yenye namba KMR/RB/4480/2016 KULAWITI.

Aidha, mwenyekiti huyo alilaani vikali kitendo cha mjumbe huyo kutolifanyia kazi suala hilo mapema na kuchukua muda mrefu jambo ambalo siyo sahihi, hivyo kuwataka wajumbe wa mitaa kutimiza majukumu yao na kuepuka kuwalinda wahalifu.

Alipotafutwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime kuhusiana na tukio hilo, simu yake iliita bila kupokelewa hadi tunakwenda mitamboni