ImageAFPImageIbrahimovic hakufunga bao hata moja Euro 2016
Mshambuliaji nyota kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovicn amethibitisha kwamba atajiunga na klabu ya Manchester United.
Amethibitisha hayo kupitia mitandao ya kijamii.
"Ningependa kuufahamisha ulimwengu. Kwamba ninaelekea Manchester United," ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada yake kuondoka Paris St-Germain.
Anatarajiwa kutia saini mkataba wa mwaka mmoja Old Trafford.
Ibrahimovic atakuwa mchezaji wa pili kununuliwa na meneja mpya wa United Jose Mourinho, aliyemrithi Louis van Gaal mwezi Mei.
Beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 22, alikuwa wa kwanza kununuliwa.
United walilipa £30m kumchukua kutoka Villarreal ya Uhispania.
United pia wanaendelea kumuwinda Henrikh Mkhitaryan, 27, raia wa Armenia anayechezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
ImageEPA
Ibrahimovic aliongoza ufungajji mabao Ligue 1 msimu uliopita, akifunga mabao 38.
Hata hivyo, hakuweza kufaa sana taifa lake la Sweden ambalo liliondolewa michuano ya Euro 2016 hatua ya makundi. Ibra hakufunga hata bao moja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni