Jumatatu, 8 Februari 2016

Wenger:Arsenal Itaichakaza Leicester Jumapili

JUMAPILI

By Meshack Brighton

19:24ENGLISH FOOTBALLSHARE

0

Getty

Arsene Wenger anaamini Arsenal yake ina uwezo wa kutosha kuwapiga vinara wa Ligi Kuu Leicester City Jumapili ijayo

Washika mtutu wa London wapo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya ushindi mwepesi dhidi ya Bournemouth. Magoli kutoka kwa Mesut Ozil na Alex Oxlade-Chamberlain yaliyopishana kwa muda wa sekunde 88 – kuhitimisha mwenda wa Arsenal wa saa tano na nusu bila ya goli.

 “[Kuifunga Bournemouth] ni vizuri sana kwa ajili ya mustakabali kwani sasa tuna mechi kubwa nyumbani dhidi ya Leicester ambao wana nafasi kubwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu,” Wenger alikiambia Arsenal.com. “Ushindi kwa namna Fulani unakuweka katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo unaofuata.

“Tuna wiki moja ya kujiandaa na mchezo huo na ninautafakari sana. Leicester ni timu imara lakini nasi tupo imara pia. Nyumbani tukiwa na mashabiki wetu tutawafunga tu.”

Mfaransa huyo aliwamwagia misifa Chamberlain na Gabriel kwa kushiriki kuwezesha ushindi kupatikana Jumapili.

 “Oxlade-Chamberlain ana nguvu, mbinu na mwenye uwezo wa kufunga magoli lakini anaweza kutengeneza nafasi pia,” aliongeza Wenger. “Mara nyingi hana bahati [na mashuti yake] lakini nadhani hilo litamshawishi kujaribu Zaidi na Zaidi.

“Gabriel amefanya vizuri. Ameonyesha kiwango safi na kwa ujumla nadhani anazidi kujiamini kadiri anavyocheza mechi nyingi, jambo linalofurahisha.”

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni