Alhamisi, 4 Februari 2016

Arsene Wenger Amekubali Yaishe Kuhusu Ubingwa EPL

ARSENE WENGER ASALIMU AMRI ARSENAL

By Meshack Brighton

04:15PREMIER LEAGUESHARE

0

Getty Images

Arsene Wenger amekiri ni za haki na za kweli hukumu za EPL baada ya kulazimishwa sare tasa na Southampton Emirates na tumaini la ubingwa halipo tena

Kama ilikuwa imepangwa vile, wameshindwa kufunga mechi ya tatu mfululizo katika mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Barclays na sare ya nyumbani ya 0-0 dhidi ya Southampton imeitupa Arsenal mbali kabisa katika mbio za ubingwa.

Arsenal wana pengo la pointi tano kutoka kwa vinara wa ligi Leicester na pointi tatu nyuma ya Manchester City wakikaribia kufikiwa na Tottenham wanaoshika nafasi ya nne.

Je! hali ni ile ile ya siku zote na hadithi zile zile za Profesa Wenger?

Arsene Wenger amekubali kuwa klabu yake ipo kwenye wakati mgumu katika mbio za ubingwa wa Ligi ya Uingereza kwa sasa.

Katika mahojiano na Daily Mail Arsene Wenger alinukuliwa akisema maneno haya kufuatia mwendo mbovu wa timu yake katika mechi tatu mfululizo.

“Tutaona mwisho wa msimu huu. Ni mapema sana kusema chochote”.

“Ni dhahiri tumekuwa na msimu mbaya hasa kuanzia ile mechi ya kwanza dhidi ya Liverpool na ile mechi dhidi ya Stoke ambayo kimsingi tumekuwa na tofauti kubwa sana katika michezo yetu miwili”, alisema Wenger.

 Pia kuhusu usajili wa mshambuliaji bora katika umaliziaji Arsene Wenger amekuwa akijitetea mara kwa mara na kusema kuwa hakuna washambuliaji bora sokoni kwa sasa ambao wanaweza kuimarisha safu aliyo nayo.

Amesema washambuliaji hawatafutwi mtaani bali kila mshambuliaji mkubwa yupo kwenye timu yake na ana mkataba.

"Huwezi tu kupita mtaani ukaanza kutafuta mshambuliaji."

"Wala huwezi kupata mshambuliaji atakayekwambia nipo hapa njoo unisajili."

Hayo ndiyo maneno ya Wenger, ni dhahiri ameona maji yamefika shingoni na hakuna ujanja anaweza kufanya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni