Diamond aliteuliwa kushiriki katika kipengere cha ‘Best International Act Afrika 2016’ kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka mmoja uliopita ambapo tuzo ilikwenda kwa Davido kutoka Nigeria.
Los Angeles, Marekani. Mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Black Coffee ameshinda tuzo ya BET na kuwapiku mastaa wengine saba walioteuliwa kuwania tuzo hiyo moja tu Afrika akiwamo, Diamond Platnumz kutoka Tanzania.
Diamond aliteuliwa kushiriki katika kipengere cha ‘Best International Act Afrika 2016’ kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka mmoja uliopita ambapo tuzo ilikwenda kwa Davido kutoka Nigeria.
Diamond alikuwa akichuana na baadhi ya mastaa wa Afrika akiwamo Yemi Alade, Wizkid kutoka Nigeria, maarufu ‘Black Coffee’ na Cassper Nyovest wote kutoka Afrika Kusini, huku wengine wakiwa ni Mzvee (Ghana) na Serge Beynaud (Cote D’ivoire).
Hata hivyo, Diamond atafanya shoo katika jukwaa hilo na itakuwa ni shoo ya kwanza kwake tangu kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo baada ya shoo hiyo, ametangaza ratiba ya shoo zake zingine zinazofuatia.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kuteuliwa kuwania tuzo hiyo kubwa duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni