Return of the King Kong. Baada ya kukosekana kwenye muziki kwa kipindi kirefu, msanii wa Hip Hop Bongo, Chidi Benz amerejea tena machoni mwa watu na muonekano mpya.
Hivi karibuni kuliibuka tetesi kuwa rapper huyo ametoroka kwenye kituo cha LIFE AND HOPE REHABILITATION kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani alipokuwa akipata matibabu ya kupambana kujitoa kwenye uraibu wa madawa ya kulevya alipopelekwa kwa msaada wa Babu Tale na Kala Pina, lakini hilo lilionekana halikuwa na nguvu kutokana na hivi karibuni hali yake imeonekana kuimarika na kurejea kama awali.
Safari ya ‘sober house’ Bagamoyo
Baada ya hali ya Chidi Benz kuonekana kuwa mbaya zaidi, March 21 mwaka huu Babu Tale na Kala Pina walichukuwa hatua ya kumpeleka kwenye kituo cha LHRC kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kupata tiba ya kujiondoa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya yaliyopelekea hali yake ya kiafya kuwa mbaya.
Kupitia akaunti ya Instagram ya Babu Tale aliandika: “Mwana amekubaLi kukaa Soba ila anasisitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii safari ya matumaini.”
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Babu Tale alisema sababu yake iliyompelekea kumsaidia ChidI Benz kuwa alidhani msanii huyo kuwa ana ngoma [ukimwi].
“Kusema ukweli nilipoona picha ile nilipata wasiwasi nikidhani Chidi Benz labda ameungua na maradhi yetu ya sasa, sikuamini kama ni madawa ya kulevya ndiyo yamempelekea hali ile. Lakini sikuweza kuamini kesho yake ilibidi nimchukue Chid Benzi na kwenda nae kwenye kituo cha afya na kufanya check up ya mwili mzima, lakini baada ya vipimo kutoka akaonekana yuko poa kabisa ila wakagundua tu ni hayo madawa.”
Baada ya siku 27 akiwa ndani ya kituo hicho, alipotembelewa na Kala Pina, Chidi alisema, “Sina mengi ya kuongea, niko sawa, nipo okay, niko fresh na msaada naupata.”
Tetesi za kutoroka sober house
May 25 zilisambaa tetesi za kutoroka kwa Chidi Benz kwenye kituo hicho alichopelekwa kwaajili ya kupata matibabu ya kupambana kujitoa kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.
Kwa kipindi hicho watu waliompeleka huko walishindwa kuongea chochote zaidi ya kusema kuwa hakutoroka bali aliruhusiwa na uongozi wa kituo hicho kurudi nyumbani.
Tetesi za kujiunga na WCB
Chid Benz akiwa na Diamond kwenye studio ya WCB
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Chidi Benz amepost picha alizopiga kwenye studio ya WCB zinazomuonyesha akiwa na Diamond, Babu Tale na Harmonize hali inayozua shaka kuwa huenda King Kong akawa ameshamwaga wino wa kujiunga kwenye lebo hiyo ili kurudisha makali yake kama zamani.
Chid Benz akiwa na Meneja wa WCB, Babu Tale
Aidha inadaiwa kuwa tayari Chidi ameshapika ngoma ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni japo bado haijajulikana iwapo wimbo huo umefanyika chini ya menejimenti ya WCB au laah.
Chid Benz akiwa na Harmonize
Kila la kheri King Kong aka Chuma, nafasi yako kwenye muziki bado ipo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni