Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima.
By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewataka watu wenye taarifa za mahali aliko, Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, waisaidie polisi kwa kuwa bado wanaendelea kumtafuta.
Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.
Sauti kwenye mkanda huo inasema Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo Rais wa sasa, John Magufuli anayashughulikia.
Juzi, askari wa jeshi hilo, walishinda mbele ya geti la nyumba ya askofu huyo kwa saa saba bila kufunguliwa na kuondoka.
Kamanda Sirro amesema kuwa “Kama amejificha, tukimbaini alipo tutamkamata na atambue bado tunamtafuta.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni