Jumamosi, 11 Juni 2016

PrismPhotolab Ndani Ya Industry Ya Picha Tanzania




PrismPhotolab ni company mpya Hapa jijini Dar-es-salaam inayojihusisha na maswala ya kupiga picha za aina zote kwa bei nafuu kabisa kuliko studio nyingine HAPA jijini Dar-es-salaam. Quality ya picha na bei zao zipo fair kabisa kuliko company nyingnine, kitu kingine kizuri ni kwamba utapata picha zako haraka zaidi kuliko kawaida kutokana company hii kujali zaidi wateja.
                                                        Moja ya Picha kutoka PRISM
Company hii inamilkiwa na kijana mdogo tu ambae pia ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM) Ambae anajulikana kama BRIGHTON IVOD a.k.a Brandroid ambae tangu zamani alikua akipenda maswala ya picha kutoka moyoni na hii ndo ilikua ndoto yake ya kila siku ambayo sasa inaanza kutimia
                                                           Brighton, C.E.O wa PRISM
Tulifanikiwa kuzungumza nae kwa kirefu zaidi ambapo amesema mwaka huu mambo mazuri yanakuja ni watu wakae tayari kwa kazi nzuri pia support yao ni muhimu, "kazi nzuri zinzkuja mwaka huu kwasababu huu ndo mwanzo tu kwaio muda unahitajika ili tuendelee kufanya kazi nzuri na zenye ubora" na nilimuuliza kuhusu kufanya kazi na models wakubwa hapa nchini "Huo mpango upo sana ilikuweza kuitangaza kampuni ifike mbali zaidi lazima pia watu maarufu watumike kutangaza kazi nzuri, tushaongea na mastaa kadhaa kupitia mtandaoni though siwezi kuweka wazi ni staa gani na gani lakini muda ukifika kilakitu kitakua sawa"
waswahili wanasema tusiandikie mate na wino ungalipo bhasi na mimi niliomba nipigwe picha angalau moja ili niweze na mimi kupima ubora wa kazi zake
                                                     MunishiJr, www.munishijr.blogspot.com
kusema ule ukweli huyu jamaa anaweza kupiga picha tuache masihara kipaji anacho hio picha hapo juu ni picha yangu amabayo nilipiga kwenye company yake ya PRISMPHOTOLAB aise hii iko tofauti na picha zangu zote nilizopiga sehemu mbalimbali
Kwaio kama na wewe unapenda utokelezee kama mimi na watu wengine hapo kwenye Picha usipoteze muda njoo PRISM kwa mawasiliano zaidi unaweza ukamcheki Brighton kwenye namba zake za simu, +255689419414 Facebook->Prism Photolab Instagram->prism_photolab

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni