Msanii kutoka Rockcity Mwanza Anaejulikana kwa jina la YOUNGKILLER MSODOKI ameachia Ngoma Mpya inayokwenda kwa jina la MTAFUTAJI audio imefanywa na Mr.T touches
Jumatatu, 15 Agosti 2016
DOWNLOAD Ngoma Mpya Ya YOUNGKILLER -Mtafutaji Mp3
Jumanne, 2 Agosti 2016
Meneja wa Diamond 'Babutale' Amekamatwa na Polisi
HABARI
Meneja wa Diamond akamatwa tena
Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’
By James Magai na Hadija Jumanne, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.
Mwanafunzi Wa UDOM Auwawa Akitokea Bar
HABARI
Mwanafunzi wa Udom auawa akitokea baa
By mwananchipapers@mwananchi.co.tz Rachel Chibwete, Mwananchi
IN SUMMARY
Tukio hilo limetokea jana usiku eneo la Chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akigalagala njiani.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Dodoma. Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Fredrick Joseph (25), ameuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akitoka baa.
Tukio hilo limetokea jana usiku eneo la Chuo hicho ambapo mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele ndipo walinzi wakafika na kumkuta akigalagala njiani.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa, amesema mwanafunzi huyo ambaye ametokea Musoma mkoani Mara ameshambuliwa kwa kupigwa na watu wasiofahamika
Jumapili, 31 Julai 2016
Msanii Diamond Platnumz na Idea nyingi za kucopy video za wasanii wengine
Idea za kukopi ambazo anafanya msanii wa kizazi kipya hapa Tanzania Almaarufu kama diamond platnumz zimeanza kuwa nyingi ambapo hali inaweza kumshusha kisanii kutokana kwamba ubinifu sasa hivi anaanza kuishiwa
Kwa kirefu zaidi endelea kusoma HAPA
Ijumaa, 15 Julai 2016
Jumapili, 10 Julai 2016
Download Nyimbo Mpya Ney wa Mitego - 'PALE KATI PATAMU'
Msanii Asiyeishiwa na Vituko kunako kwa Bongofleva ambae jina lake halisi ni Emmanuel Elibariki almaarufu kama Ney wa Mitego Leo ameachia Ngoma yake Mpya Inayokwenda kwa jina la 'PALE KATI PATAMU' Producer ni Mr.T touches
Ijumaa, 8 Julai 2016
Hii Ndo Prism Photolab Ingia Hapa Uone Picha Kali >>>>>>>>
0689419414- Brighton
0686257790- Marc dee
0716837444- Geofrem
0655447427- Munishijr
Kwenye Mitandao Ya kijamii Pia unaweza kuwapata;
Facebook - Prism Photolab
Instagram - @Prism_photolab
WhatsApp - 0689419414
Alhamisi, 30 Juni 2016
Ibrahimovic Huyoo Man United
ImageAFPImageIbrahimovic hakufunga bao hata moja Euro 2016
Mshambuliaji nyota kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovicn amethibitisha kwamba atajiunga na klabu ya Manchester United.
Amethibitisha hayo kupitia mitandao ya kijamii.
"Ningependa kuufahamisha ulimwengu. Kwamba ninaelekea Manchester United," ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada yake kuondoka Paris St-Germain.
Anatarajiwa kutia saini mkataba wa mwaka mmoja Old Trafford.
Ibrahimovic atakuwa mchezaji wa pili kununuliwa na meneja mpya wa United Jose Mourinho, aliyemrithi Louis van Gaal mwezi Mei.
Beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 22, alikuwa wa kwanza kununuliwa.
United walilipa £30m kumchukua kutoka Villarreal ya Uhispania.
United pia wanaendelea kumuwinda Henrikh Mkhitaryan, 27, raia wa Armenia anayechezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
ImageEPA
Ibrahimovic aliongoza ufungajji mabao Ligue 1 msimu uliopita, akifunga mabao 38.
Hata hivyo, hakuweza kufaa sana taifa lake la Sweden ambalo liliondolewa michuano ya Euro 2016 hatua ya makundi. Ibra hakufunga hata bao moja.
Jumamosi, 25 Juni 2016
Prof. Mkilaha wa UDSM amefariki dunia kwa kujipiga risasi
Profesa Mkilaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
By Herieth Makwetta, Mwananchi hmakweta@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema polisi wanaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha tukio hilo.
Dar es Salaam. Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idd Mkilaha, inadaiwa amefariki dunia jioni hii nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam baada ya kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema polisi wanaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha tukio hilo.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, amekufa kwa kujipiga risasi, lakini tunachunguza kubaini kama ilikuwa ni bahati mbaya au alidhamiria kufanya hivyo,” amesema Sirro.
Hata hivyo, amesema taarifa zaidi atazitoa kesho.
Profesa Mkilaha alikuwa pia Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).
Msanii Black Coffee Ashinda tuzo ya BET
Diamond aliteuliwa kushiriki katika kipengere cha ‘Best International Act Afrika 2016’ kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka mmoja uliopita ambapo tuzo ilikwenda kwa Davido kutoka Nigeria.
Los Angeles, Marekani. Mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Black Coffee ameshinda tuzo ya BET na kuwapiku mastaa wengine saba walioteuliwa kuwania tuzo hiyo moja tu Afrika akiwamo, Diamond Platnumz kutoka Tanzania.
Diamond aliteuliwa kushiriki katika kipengere cha ‘Best International Act Afrika 2016’ kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka mmoja uliopita ambapo tuzo ilikwenda kwa Davido kutoka Nigeria.
Diamond alikuwa akichuana na baadhi ya mastaa wa Afrika akiwamo Yemi Alade, Wizkid kutoka Nigeria, maarufu ‘Black Coffee’ na Cassper Nyovest wote kutoka Afrika Kusini, huku wengine wakiwa ni Mzvee (Ghana) na Serge Beynaud (Cote D’ivoire).
Hata hivyo, Diamond atafanya shoo katika jukwaa hilo na itakuwa ni shoo ya kwanza kwake tangu kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo baada ya shoo hiyo, ametangaza ratiba ya shoo zake zingine zinazofuatia.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kuteuliwa kuwania tuzo hiyo kubwa duniani.
Majina Ya Waliochaguliwa Kujiunga na kidato cha tano na Vyuo vya ufundi haya hapa ->>>>>>>
Majina ya vijana wa kidato cha nne waliofaulu vizuri wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali za serikali na pamoja na vyuo vya ufundi
Jumanne, 21 Juni 2016
Askari Aliyetukanwa na Mke wa Waziri Bado Hajapandishwa Cheo
Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI
Dar es Salaam: Mapya yameibuka kumhusu askari wa usalama barabarani (trafiki), Koplo Deogratius Mbango wa Kituo cha Oysterbay ambaye wiki chache zilizopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliagiza apandishwe cheo kutokana na kufurahishwa na utendaji kazi wake ambapo habari mpya ni kwamba, hadi juzi (Jumapili), bado hakuwa amepandishwa cheo kama rais alivyoagiza.
Trafiki huyo, alipata umaarufu mkubwa baada ya kumdhibiti dereva wa mke wa waziri mmoja (jina kapuni) aliyevunja sheria za usalama barabarani kwa kusimama kwenye alama za pundamilia (zebra) ambazo kimsingi hutumiwa na watembea kwa miguu wanaovuka barabara.
Akiwa anatekeleza majukumu yake, Aprili 24, mwaka huu, inadaiwa kuwa mke wa waziri aliyekuwa amebebwa ndani ya gari hilo, amlijia juu Koplo Deogratius huku akimtolea vitisho kwa kutumia cheo cha mumewe, lakini askari huyo hakutetereka zaidi ya kuendelea kusimamia sheria na kuwataarifu wakubwa wake wa kazi, akiwemo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni (RTO) Awadh Haji.
Katika uchunguzi wake wa chini kwa chini, Uwazi limebaini kuwa bado askari huyo anaendelea kukitumikia cheo chake cha zamani, jambo ambalo ni kinyume na maagizo aliyoyatoa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.
Ili kujiridhisha zaidi, Uwazi liliwahoji baadhi ya watu wa karibu wa askari huyo ambao kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini kwani siyo wasemaji, walisema Koplo Deogratius hajapandishwa cheo kama Rais Magufuli alivyoagiza kwani kama ingekuwa hivyo, angekuwa anaonekana.
Uwazi halikuishia hapo, lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga na kumuulizia sababu zilizokwamisha afande huyo kupandishwa cheo mpaka sasa ambapo alisema:
“Aaah ni kweli ndugu mwandishi hilo agizo lilitolewa na rais lakini hata mimi sijui kwa nini hajapandiswa cheo mpaka leo. Unajua suala la upandishwaji wa vyeo vya kipolisi hata hawa wa usalama barabarani walio chini yangu, huwa sihusiki bali anayewapandisha ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. Muulize mwenyewe au mtafute msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimbo wao ndiyo watakaoweza kukupa majibu ya uhakika.”
Gazeti lilianza kumtafuta Advera kwa njia ya simu ambapo simu yake haikuwa hewani kila alipopigiwa. Baada ya kumkosa, Uwazi lilimtafuta, IGP Mangu kwa njia ya simu lakini naye simu yake haikuwa hewani kila alipopigiwa.
Ijumaa, 17 Juni 2016
Askofu Gwajima Anatafutwa na Polisi 'usiku na mchana'
Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima.
By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewataka watu wenye taarifa za mahali aliko, Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, waisaidie polisi kwa kuwa bado wanaendelea kumtafuta.
Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.
Sauti kwenye mkanda huo inasema Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo Rais wa sasa, John Magufuli anayashughulikia.
Juzi, askari wa jeshi hilo, walishinda mbele ya geti la nyumba ya askofu huyo kwa saa saba bila kufunguliwa na kuondoka.
Kamanda Sirro amesema kuwa “Kama amejificha, tukimbaini alipo tutamkamata na atambue bado tunamtafuta.”
Alhamisi, 16 Juni 2016
'Burger Movie Selfie remix' by Belle9 ft. Jux, Gnako, Blue, Izzobusiness, Mauasama
Remix ya wimbo wa Burger Movie Selfie msanii Belle9 tayari ishatoka ambapo ndani kawashirikisha Gnako, Izzobusiness, jux, Maua sama
Enjoy the song chini hapo
👇👇👇👇👇👇👇👇👇














