Jumatatu, 30 Mei 2016

Vanessa na Shilole hawana bifu zile zilikua kiki tu... Hawa hapa kwenye stage moja

Kwa takribani week mbili hivi kwenye mitandao mingi ya kijamii kulizuka habari kwamba wanamuziki wawili wa bongofleva,Shilole a.k.a shishi baby pamoja na msanii mwenzie wa kike,Vanessa Mdee a.k.a Vee money 

Kila mmoja kwenye account yake ya INSTAGRAM alipost video akimpondea mwenzie ambapo Vanessa Mdee ndo alianza kumpost shilole afu baadae shilole nae akajibu mashambulizi 

Mitandao mingi kulikua na headline kwamba wasanii hawa wanabifu zito. Lakini kumbe ni tofauti kabisa na matarajio ya watu wengi ishu ni kwamba zile zilikua kiki tuu kwaajili ya show yao iliyofanyika weekend hii pale kwenye ukumbi wa BILLCANS ambapo show hio ilikua na surprise nyingi sana zilizofanywa na wasanii hawa ikiwa pamoja na kula ugali jukwaani BONYEZA HAPA KUCHECK SHOW YAO KAMA ULIKOSA baada ya show hio yapo mambo mengi ya kujiuliza ikiwa pamoja na uwezekano wa wasanii hawa kufanya collabo yoyote kwahio bado tunasubiri mambo mengi tuu kutoka kwao 

Jumatano, 25 Mei 2016

Download Nyimbo Mpya ya Youngkiller ft. Mr. BLUE-KUMEKUCHA

Youngkiller msodoki baada ya kufanya kazi nzuri na mkongwe sir Nature kwenye POPOTE KAMBI.Safari hii imekuja na mkongwe mwingine kwenye game anaitwa BLUE nafikiri kila mtu anamjua huyu jamaa katika tasnia hii ya Bongofleva basi mkongwe huyu kakutana na mdogo wake kwenye game afu wakafanya ngoma inakwenda kwa jina la KUMEKUCHA. 


👉BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD 👈

Download Nyimbo Mpya ya Raymond-Natafuta kiki

Raymond WCB msanii chipukizi kutoka lebo ya wasafi classic baby (WCB)  baada ya kufanya vizuri kwenye ngoma yake ya kwanza inayoitwa KWETU. Safari hii amekuja kivingine kwa ngoma kali pia inayokwenda kwa jina la NATAFUTA KIKI.

Katika ngoma hii amefanya ubunifu flani hivii wa mashairi akiwa kama mtu ambae anajiuliza afanye nini iliaweze kujulikana kwa watu almaarufu kama 'kiki'

Producer wa ngoma hii ni yuleyule wa ngoma ya kwanza 'KWETU' anaefahamika kama Laizer classic kutoka studio za WCB 

👉DOWNLOAD HAPA👈 ngoma mpya RAYMOND 

Nyimbo Mpya ya Giggy Money -SUPU

Staa maarufu wa kwenye video za wasanii mbali mbali hapa bongo maarufu kama GIGGY MONEY wengi wanamjua kwa vituko vyake kwenye mtandao wa kijamii hususani INSTAGRAM.Mwanadada huyu kipaji cha kuimba pia anacho sana kwasababu tushasikiliza ngoma zake nyingi tu hapo mwanzo lakini sahivi anakuja na jiwe la tofauti linakwenda kwa jina SUPU ambapo kamshirikisha mkali wa bongofleva ambae si mwingine bali ni MATONYA 

nyimbo ni kali sana halafu ni ngoma flani hivi ya kuchezeka club kwahiyo GIGGY kajitahidi sana kufanya kitu kizuri expectation zangu ngoma itafika mbali sanaa.

DOWNLOAD HAPA nyimbo mpya ya GIGGY MONEY FT. MATONYA-SUPU

Jumamosi, 21 Mei 2016

Makanisa Kuwekewa Wi-fi hotspot Nchini Ujerumani

ImageISTOCKImageKanisa la French Cathedral, Berlin litakuwa miongoni mwa makanisa ya kwanza kunufaika

Makanisa ya Kiprotestanti maeneo ya kati nchini Ujerumani yatakuwa yakiwapa waumini fursa ya kuingia katika mtandao, kwa kuwawekea huduma ya wi-fi bila malipo.

Huduma hiyo itapatikana katika maeneo ambayo, kwa kufuata ‘hostpots’ ambalo ni jina la vitovu vya huduma, yamepewa jina "Godspots".

Huduma hiyo ya Wi-fi itawekwa katika makanisa 220 katika majimbo ya Berlin na Brandenberg.

Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha RBB, mpango huo baadaye utatekelezwa katika makanisa 3,000.

Makaburi matatu kuwekwa wi-fi Moscow

Makanisa ya kwanza kupata huduma hiyo yatakuwa kanisa kuu la French Cathedral eneo la Gendarmenmarkt na kanisa la Kaiser Wilhelm Memorial Church.

Watu wataweza kutumia huduma hiyo kutoka ndani nan je ya kanisa.

Wanaotumia huduma hiyo watalakiwa na ukurasa wa tovuti yenye maelezo kuhusu kanisa lenyewe, jamii na maelezo ya kidini.

Lakini baadaye, wataweza kuchakura chochote watakacho katika mtandao wote.

Jumamosi, 14 Mei 2016

Lyrics za Wimbo Mpya wa Alikiba hizi hapa

[Verse 1 – Alikiba]

Ucheshi na sauti

Amenifanya nam-miss tu

Mwambie asiogope

Ali ni kipenzi cha watu

Ntafanya party nyumbani

Hiyo yote kwa ajili yake

Tena asije peke yake

Asiogope aje na wenzake

Ntafanya party nyumbani

Hiyo yote kwa ajili yake

Tena asije peke yake

Asiogope aje na rafiki zake eh

[Chorus – Alikiba]

Basi mwambie aje (aje)

Oh aje (aje)

Aje na rafiki zake (aje)

Asije peke yake (aje)

Oh aje (aje)

Aje, oh aje (aje)

Aje jamani aje (aje)

Aje nam-miss aje (aje)

[Verse 2 – Alikiba]

Uzuri wake timilifu

Nshamuona na watu maarufu tu

Kina Wema Sepetu

Nikaomba namba bichwa akanishushua shuu!

Ilinikosesha raha

Lulu nae kandanganya

Kwamba mi ni wa kwake

Aniogope tena asinichekee

Ilinikosesha raha

Lulu nae kandanganya oh

Kwamba mi ni wa kwake

Aniogope tena asinichekee

[Chorus – Alikiba]

Basi mwambie aje (aje)

Oh aje (aje)

Aje na rafiki zake (aje)

Asije peke yake (aje)

Oh aje (aje)

Aje, oh aje (aje)

Aje jamani aje (aje)

Aje nam-miss aje (aje)

[Verse 3 – M.I]

I say, I say, I say…

I’m gonna marry you one day

Come through baby girl

I just want us to speak

See we met on a Monday

You must be next Monday

Cause you make it one week

Have you been to the West side?

Forget whatever you seen on them Nollywood films

I wanna be your best guy

So let’s try till you testify no one’s better than him

So baby, give me your digits

Let me google map location, come and visit

You should show up in something exquisite

I can come over to yours, girl, where is it?

You could teach me to speak in Swahili

Like “sawa sawa, mambo vipi?”

Can you tell that I’m feeling you really?

Alikiba and M.I, my baby, I know that you feel me

[Chorus – Alikiba]

Basi mwambie aje (aje)

Oh aje (aje)

Aje na rafiki zake (aje)

Asije peke yake (aje)

Oh aje (aje)

Aje, oh aje (aje)

Aje jamani aje (aje)

Aje nam-miss aje (aje)

[Outro]

Come through, baby

I want you to come through, baby

Come through, baby

I want you to come through, baby

Come through, baby

I want you to come through, baby

Come through, baby

I want you to come through, baby

Lyrics za nyimbo mpya ya Alikiba hizi hapa


[Verse 1 – Alikiba]

Ucheshi na sauti

Amenifanya nam-miss tu

Mwambie asiogope

Ali ni kipenzi cha watu

Ntafanya party nyumbani

Hiyo yote kwa ajili yake

Tena asije peke yake

Asiogope aje na wenzake

Ntafanya party nyumbani

Hiyo yote kwa ajili yake

Tena asije peke yake

Asiogope aje na rafiki zake eh

[Chorus – Alikiba]

Basi mwambie aje (aje)

Oh aje (aje)

Aje na rafiki zake (aje)

Asije peke yake (aje)

Oh aje (aje)

Aje, oh aje (aje)

Aje jamani aje (aje)

Aje nam-miss aje (aje)

[Verse 2 – Alikiba]

Uzuri wake timilifu

Nshamuona na watu maarufu tu

Kina Wema Sepetu

Nikaomba namba bichwa akanishushua shuu!

Ilinikosesha raha

Lulu nae kandanganya

Kwamba mi ni wa kwake

Aniogope tena asinichekee

Ilinikosesha raha

Lulu nae kandanganya oh

Kwamba mi ni wa kwake

Aniogope tena asinichekee

[Chorus – Alikiba]

Basi mwambie aje (aje)

Oh aje (aje)

Aje na rafiki zake (aje)

Asije peke yake (aje)

Oh aje (aje)

Aje, oh aje (aje)

Aje jamani aje (aje)

Aje nam-miss aje (aje)

[Verse 3 – M.I]

I say, I say, I say…

I’m gonna marry you one day

Come through baby girl

I just want us to speak

See we met on a Monday

You must be next Monday

Cause you make it one week

Have you been to the West side?

Forget whatever you seen on them Nollywood films

I wanna be your best guy

So let’s try till you testify no one’s better than him

So baby, give me your digits

Let me google map location, come and visit

You should show up in something exquisite

I can come over to yours, girl, where is it?

You could teach me to speak in Swahili

Like “sawa sawa, mambo vipi?”

Can you tell that I’m feeling you really?

Alikiba and M.I, my baby, I know that you feel me

[Chorus – Alikiba]

Basi mwambie aje (aje)

Oh aje (aje)

Aje na rafiki zake (aje)

Asije peke yake (aje)

Oh aje (aje)

Aje, oh aje (aje)

Aje jamani aje (aje)

Aje nam-miss aje (aje)

[Outro]

Come through, baby

I want you to come through, baby

Come through, baby

I want you to come through, baby

Come through, baby

I want you to come through, baby

Come through, baby

I want you to come through, baby










Kudownload nyimbo yenyewe ingia hapa 👇👇👇👇👇

http://www.johventuretz.com/2016/05/alikiba-aje.html?m=1

Jumatano, 11 Mei 2016

Falsafa 20 za DONALD TRUMP

ImageGETTYImageTrump amekuwa na mapendekezo makali hasa kuhusu wahamiaji na ugaidi

Donald Trump anaongoza katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea urais atakayewakilisha chama cha Republican katika uchaguzi mkuu mwaka ujao. Wajua sera zake na mambo anayoyaamini?

1. Waarabu-Wamarekani jimbo la New Jersey walishangilia shambulio la Septemba 11, 2001 liliotekelezwa. Hakuna habari za kuthibitisha haya.

2. Kunafaa kuwa na mfumo wa kufuatilia misikiti Marekani kama njia ya kukabiliana na ugaidi.

3. Marekani inafaa kutumia njia kali za kuhoji washukiwa katika vita dhidi ya Islamic State.

4. Trump amesema akiwa rais anaweza kuwaangamiza Islamic State kwa mabomu na pia kuwazuia kupata mafuta.

5. Kuundwe mfumo rahisi wa ulipaji ushuru, watu wanaolipwa chini ya $25,000 (£16,524) wasiwe wakilipa ushuru wa mapato.

6. Watu wenye hazina za uwekezaji ng’ambo hawalipi ushuru wa kutosha. Lakini baadaye alibadilika na kusema watapunguziwa ushuru sawa na watu wa pato la wastani.

7. Anataka kujenga ukuta mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji kutoka Mexico.

8. Anataka kuwafurusha wahamiaji wote 11 milioni ambao waliingia Marekani kwa njia haramu.

9. Yeye na Vladmir Putin wanaweza “kusikizana vyema”.

10. Ili kuzuia visa vya watu kupigwa risasi Marekani, nchi hiyo inafaa kuwekeza katika afya ya akili.

11. Uchina inafaa kuchukuliwa hatua kali katika masuala kadha ili kuhakikisha usawa wa kibiashara kati yake na Marekani.

ImageAFPImageTrump amekuwa akisema haja yake kuu ni kurejesha hadhi ya Marekani

12. Kundi la The Black Lives Matter ambalo hutetea haki za watu Weusi Marekani ni hatari.

13. Takwimu za sasa za Marekani ni za kupotosha. Anasema ukosefu wa ajira umefikia 20% kinyume na takwimu rasmi zinazoonyesha ni 5.1%.

14. Utajiri wake ni $10bn.

15. Mfumo wa kutoa huduma za afya kwa wanajeshi wa zamani unafaa kufanyiwa mabadiliko makubwa.

16. Mpango wa Obamacare ambao ulilenga kuongeza idadi ya Wamarekani wanaopata bima ya afya ni “mkasa”.

17. Mabadiliko ya tabia nchi ni hali ya kawaida tu ya hewa.

18. Ulimwengu ungekuwa pahala pema pa kuishi kama Saddam Hussein na Muammar Gaddhafi wangekuwa bado madalakani.

19. Angewarejesha makwao wahamiaji kutoka Syria wanaotafuta hifadhi Marekani.

harusi ya wapenzi wa jinsia moja, hakufaa kazi hiyo.

20. Yeye ni “mtu mzuri sana” na anataka sana kurejesha hadhi ya Marekani.

Msanii KINYAMBE Afariki dunia

 Mchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah  "KINYAMBE" amefariki dunia leo usiku huko nyumbani kwako Mbeya. Mmoja wa wanandugu wa Kinyambe ameithibitishia Saluti5 kuwa msanii huyo wa filamu  ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/05/mchekeshaji-kinyambe-afariki-dunia.html?m=0

Msanii huyu alikua mahiri sana kwa staili yake ya uchekeshaji kama tahira hivi,Alifanya kazi nyingi na kampuni ya Alriyam production iliopo Jijini Tanga na wasanii wengine kama masele,kazi,masai, 

Pia kinyambe alishawahi kuimba muziki na nyimbo zake zipo nyingi tuu mtandaoni 

 

 

Hapo juu 👆👆👆 ndo post ambayo watu wengi waliiona katika mtandao wa kijamii wa FACEBOOK hapo habari za kifo cha msanii huyu zilipoanza kusambaa kwa kasi sana

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya msanii wetu KINYAMBE .......REST IN PEACE KINYAMBE

Jumamosi, 7 Mei 2016

Msichana Asiye na Mikono Ashinda Tuzo ya Mwandiko Mzuri

ImageMsichana asiye na mikono ashinda shindano la muandiko bora Marekani

Msichana wa miaka saba aliyezaliwa bila mikono ameshinda shindano la muandiko mzuri nchini Marekani.

Anaya Ellick kutoka Chesapeake,Virginia hatumii viungo vya kumsaidia wakati anapoandika.

Wakati anapoandika yeye husimama huku akishikilia kalamu yake katika mikono.

Mwalimu wake mkuu Tracy Cox kutoka shule ya Greenbrier Christian amemtaja kuwa mtu wa mfano mwema.

''Yeye uhakikisha kuwa hakuna kitu kinachomzuia kufanya atakalo'',alisema Cox.''Ni mkakamavu na ana muandiko mzuri katika darasa lake''.

Msichana huyo anadaiwa kuwashinda washindani wengine 50 ili kushinda taji hilo la kitaifa.

Orodha hiyo ya tuzo huwazawadi wanafunzi wenye akili, matatizo ya kimwili, au ulemavu endelevu

Jumapili, 1 Mei 2016

VOTE for MSHANGAMA SHAMIRA Daruso Vice President

Habari za mda huu ndugu zangu wana UDSM.

Jina langu kamili ni MSHANGAMA SHAMIRA  mgombea nafasi ya umakamu wa Raisi DARUSO 2016/2017 kwa moyo mkunjufu ndugu zangu wa udsm naomba mnipe ridhaa hii ya kuwatumikia ili nikatimize matakwa ya wana udsm ya mda mrefu niliyoyafanyia utafiti jinsi gani ya kuyatekeleza:

1. Nitarudisha utaratibu wa kuwepo na revolution square movement ambayo ni haki yetu, eneo hili huwa linatumika na wana udsm haswa wana harakati kujadili mambo ya msingi yanayohitaj ufafanuzi na utatuzi, mfano kwa boom kutoka 5000-7500 movement yake ilianzia revolution square... Nikiwa kama makamu wa raisi nikishirikiana na raisi wangu kikatiba tutamwandikia barua DVC academic juu ya matakwa yetu ya kukutana revolution square na kuweza kufanya makutano hayo kama students by-law inavyosema.

2. Ili kujiridhisha na utendaji wa viongozi wetu tuliowachagua, nitahakikisha suala la students BARAZA linakuwepo angalau Mara mbili kwa semester kama katiba inavyoelekeza katika ibara ya 28, ili kujadili masuala mbali mbali kati ya wanafunzi na viongozi na kupitia utendaji kazi wa kila kiongozi ikiwa pamoja na taarifa za mapato na matumizi ya DARUSO, viongozi kuhojiwa, kukosolewa na kushauriwa.

3. Katiba ya DARUSO inaainisha ushirikiano wangu na raisi katika kuunda baraza la mawaziri katika ibara ya 15(3) ya katiba ya Daruso nitahakikisha tunapanga baraza dogo la mawaziri, wizara ziwe 10 na mawaziri 22, kutoka wizara 11 na mawaziri 25 waliopo hivi sasa, hii itapunguza gharama za DARUSO kujiendesha na hizi pesa zitatumika katika mambo mengine yatakayotukabili ikiwemo kuzitumia katika majanga yanayojitokeza.

4. Nitahakikisha kwa kushirikiana na Rais, ofisi ya bunge na cabinet tunamshauri na kumtaka DEAN OF STUDENTS katika utekelezaji wa majukumu yake azingatie majukumu yake halisi ambayo ni kushauri tu na siyo kuliingilia au kulitisha bunge, wanafunzi au viongozi wa Daruso au kususia vikao ili vikose uhalali.

Hili litawezekana kwani kisheria, Dean of students mamlaka yake yanatajwa katika ibara ya 28 (3), ya kwamba atakuwa mshauri mkuu mwenye 'uhalali' wa kuhudhuria vikao vya Daruso.

5. Nitaendeleza timu ya mpira wa miguu ya wanawake ambayo tumeshaanza nayo mazoezi ili iwe bora na chuo chetu kipate sifa kwenye sekta ya mpira wa miguu...timu ya wanaume ntahakikisha inapata mechi nyingi za kirafiki na timu kubwa za uraiani ili kukitangaza vyema chuo chetu lakini pia nitasimamia kuhakikisha Inter-colleges competitions inafanyika ili kutafuta wachezaji katika college zote za UDSM.



6. Nitahakikisha kila waziri anatimiza wajibu wake ipasavyo kwa kufanya monthly review mwenyewe kama makamu wa raisi na kumshauri raisi kuondoa wote wanaofanya kazi kwa uzembe, Lakini pia nitahakikisha serikali yote ya Daruso haihamii main campus na badala yake angalau Naibu au waziri katika wizara za Makazi (accomodation), Ulinzi na wizara ya usafiri na wanakuwa wakazi wa Mabibo ili kukabiliana kero zinazojitokeza na kuhojiwa na wana UDSM juu ya kero za masuala tajwa na kuzitatulia ufumbuzi.

7. Nitahakikisha Mimi na raisi tunateua waziri wa elimu mchapakazi na atakayeshirikiana na wenyeviti, makatibu na wabunge wa college zote na kuhakikisha mazingira ya usomaji ambayo ni rafiki wa wana udsm wote, kukabiliana na changamoto zote za kitaaluma na pia kuzingatia makundi maalum ya walemavu.

8. Katika uchaguzi wa mafood tester watawekwa mafood tester ambao watakua wanafuatuliwa ufanyaji wao wa kazi wao kila wiki na kuondoa wote wanaozembea kwa kutoka Fanya kazi zao.

9. Nitahakikisha nashirikiana bega kwa bega na raisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku kwa kumshauri, kumkumbusha na kumshinikiza katika masuala ya msingi yanayotuhusu wana DARUSO .

10. Kwa wenzetu mnaosoma COICT na SJMC kwa kushirikiana na raisi nitahakikisha kunakuwa na permanent shuttle kwa ajili ya route za kila Siku.

Kuhimiza kuharakishwa kwa ukarabati mdogo uliosalia wa hosteli za CoICT- Kijitonyama zenye uwezo wa kubeba wanafunzi takribani 500 ukamilike kwa wakati ili kupunguza angalau kidogo adha ya tatizo la hostel.

MUNGU atubariki tufikie matarajio yetu, naombeni kura zenu.

MSHANGAMA SHAMIRA

mgombea nafasi ya umakamu wa Rais, Daruso.

Jina langu litakuwa la pili katika ballot paper siku ya Jumatatu.



MIMI NI MTUMWA WENU, NITUMENI.