Jumapili, 31 Julai 2016

Msanii Diamond Platnumz na Idea nyingi za kucopy video za wasanii wengine

Idea za kukopi ambazo anafanya msanii wa kizazi kipya hapa Tanzania Almaarufu kama diamond platnumz zimeanza kuwa nyingi ambapo hali inaweza kumshusha kisanii kutokana kwamba ubinifu sasa hivi anaanza kuishiwa 

Kwa kirefu zaidi endelea kusoma HAPA

Jumapili, 10 Julai 2016

Download Nyimbo Mpya Ney wa Mitego - 'PALE KATI PATAMU'

Msanii Asiyeishiwa na Vituko kunako kwa Bongofleva ambae jina lake halisi ni Emmanuel Elibariki almaarufu kama Ney wa Mitego Leo ameachia Ngoma yake Mpya Inayokwenda kwa jina la 'PALE KATI PATAMU'  Producer ni Mr.T touches 

DOWNLOAD HAPA - NEY WA MITEGO_PALE_KATI_PATAMU_MP3

Ijumaa, 8 Julai 2016

Hii Ndo Prism Photolab Ingia Hapa Uone Picha Kali >>>>>>>>

Prism Photolab bado wapo on fire kwa kufanya kazi nzuri sana za kupiga picha ambazo ni bora pia kwa bei nzuri sana ambapo watu wengi wanashindwa kuamini, Ukizicheki picha ambazo kampuni hii inapiga (quality) na bei  zake huwezi kuamini. Ngoja nikuonyeshe Picha zao kadhaa labda utanielewa nini namaanisha
Unacheki picha hio ilivyokua kali lakini sasa uliza bei ndo utashangaa mwenyewe, Bei flani ya kawaida sana. Ebu nikuonyeshe nyingine
Hio Picha nyingine kutoka Prism Photolab ambayo nayo kali sana ambapo dada yetu @reen.momo ametokelezea sana hio haina ubishi hichi ndicho kinachoitofautisha Prism na kampuni nyingine za Picha kwasababu kupata kitu cha quality kama hio kwa bei ya kawaida ni ngumu sana hapa jijini Dar-es-salaam Lakini Prism Photolab wanakupa unachoitaji.
Nashindwa kuelewa kwanini bado tu huichagui Prism Photolab kama Mpiga picha wako kwasababu ya vitu vikubwa viwili 1.ubora wa picha (quality) 2.Bei rahisi sana. Najua mara ya kwanza ukiziona picha unaweza ukastuka kujiuliza bei itakuaje lakini sasa cha kukutoa hofu ni kwamba bei ipo kwaajili yako wewe mwenye Hali ya chini na unapenda kutisha kwenye picha .... watoto wa mjini wanasema Photogenic we usisite kuwatafuta Prism Photolab kwenye mawasiliano yao chini hapo
Pia kitu kingine kizuri Eneo (location) ya kupigiwa picha unachagua mwenyewe japokua unaweza pia kushauriwa na wadau wa Prism lakini wewe mwenyewe unakua huru kusema wapi unataka kufanya picha zako.
Habari njema kwa wale wenye couples zao na wanapenda kupiga picha ili kudumisha penzi lao bhasi msihangahike tena kwasababu Prism ndo mtatuzi wa shida zenu zote kwa bei ya kawaida sana, Prism Photolab wanafanya picha couples seheme yoyote wakati wowote ule kwa bei maridhawa tu. Ngoja nikuonyeshe Moja ya Picha za couples ambazo Prism washawahi kufanya

Kama unavyoona mwenyewe hapo haina haja ya maelezo mengi kujua hio picha inamaanisha nini ila yote tisa kumi ni kwamba Prism Photolab ndo sehemu sahihi kwa nyie wapendanao kama mnahitaji picha kama hizo za pamoja msisite kuwatafuta PrismPhotolab.
Kazi ya Prism ni kuhakikisha kwamba watu wanapendeza na kufurahi wakati wote na hayo ndo maisha yanavyotakiwa yawe sikuzote. Unawekwa kwenye Ulimwengu mwingine unaweza ukahisi ni ndoto lakini kwa Prism kilakitu na kinatimizwa na kufanywa kweli.
Pia Prism inafanya kazi kwenye sherehe zote na kwa wakati wowote tu mfano Birthday Party, Harusi, Anniversary, au Event ambayo itahitaji Picha Bhasi Prism ipo kwaaajili yako.
Kama mnavyoona Picha hio hapo ilipigwa kwenye boti hivi maeneo flani hapa hapa jijini Dar.

Unaweza kuwapata Prism Photolab kupitia namba zifuatazo;
0689419414- Brighton
0686257790- Marc dee
0716837444- Geofrem
0655447427- Munishijr

Kwenye Mitandao Ya kijamii Pia unaweza kuwapata;
Facebook - Prism Photolab
Instagram - @Prism_photolab
WhatsApp - 0689419414

                                                                                                                                                                                           

Alhamisi, 30 Juni 2016

Ibrahimovic Huyoo Man United

ImageAFPImageIbrahimovic hakufunga bao hata moja Euro 2016

Mshambuliaji nyota kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovicn amethibitisha kwamba atajiunga na klabu ya Manchester United.

Amethibitisha hayo kupitia mitandao ya kijamii.

"Ningependa kuufahamisha ulimwengu. Kwamba ninaelekea Manchester United," ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada yake kuondoka Paris St-Germain.

Anatarajiwa kutia saini mkataba wa mwaka mmoja Old Trafford.

Ibrahimovic atakuwa mchezaji wa pili kununuliwa na meneja mpya wa United Jose Mourinho, aliyemrithi Louis van Gaal mwezi Mei.

Beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 22, alikuwa wa kwanza kununuliwa.

United walilipa £30m kumchukua kutoka Villarreal ya Uhispania.

United pia wanaendelea kumuwinda Henrikh Mkhitaryan, 27, raia wa Armenia anayechezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

ImageEPA

Ibrahimovic aliongoza ufungajji mabao Ligue 1 msimu uliopita, akifunga mabao 38.

Hata hivyo, hakuweza kufaa sana taifa lake la Sweden ambalo liliondolewa michuano ya Euro 2016 hatua ya makundi. Ibra hakufunga hata bao moja.

Jumamosi, 25 Juni 2016

Prof. Mkilaha wa UDSM amefariki dunia kwa kujipiga risasi

Profesa Mkilaha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

By Herieth Makwetta, Mwananchi hmakweta@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema polisi wanaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha tukio hilo.

Dar es Salaam. Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idd Mkilaha, inadaiwa amefariki dunia jioni hii nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam baada ya kujipiga risasi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema polisi wanaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha tukio hilo.

“Ni kweli tukio hilo limetokea, amekufa kwa kujipiga risasi, lakini tunachunguza kubaini kama ilikuwa ni bahati mbaya au alidhamiria kufanya hivyo,” amesema Sirro.

Hata hivyo, amesema taarifa zaidi atazitoa kesho.

Profesa Mkilaha alikuwa pia Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Msanii Black Coffee Ashinda tuzo ya BET

Diamond aliteuliwa kushiriki katika kipengere cha ‘Best International Act Afrika 2016’ kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka mmoja uliopita ambapo tuzo ilikwenda kwa Davido kutoka Nigeria.

Los Angeles, Marekani. Mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Black Coffee ameshinda tuzo ya BET na kuwapiku mastaa wengine saba walioteuliwa kuwania tuzo hiyo moja tu Afrika akiwamo, Diamond Platnumz kutoka Tanzania.

Diamond aliteuliwa kushiriki katika kipengere cha ‘Best International Act Afrika 2016’ kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka mmoja uliopita ambapo tuzo ilikwenda kwa Davido kutoka Nigeria.

Diamond alikuwa akichuana na baadhi ya mastaa wa Afrika akiwamo Yemi Alade, Wizkid kutoka Nigeria, maarufu ‘Black Coffee’ na Cassper Nyovest  wote kutoka Afrika Kusini, huku wengine wakiwa ni Mzvee (Ghana) na Serge Beynaud (Cote D’ivoire).

Hata hivyo, Diamond atafanya shoo katika jukwaa hilo na itakuwa ni shoo ya kwanza kwake tangu kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo baada ya shoo hiyo, ametangaza ratiba ya shoo zake zingine zinazofuatia.

Hii ni mara ya pili kwa Diamond kuteuliwa kuwania tuzo hiyo kubwa duniani.

Majina Ya Waliochaguliwa Kujiunga na kidato cha tano na Vyuo vya ufundi haya hapa ->>>>>>>

Majina ya vijana wa kidato cha nne waliofaulu vizuri wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali za serikali na pamoja na vyuo vya ufundi 

CLICK HAPA KUONA MAJINA YOTE

Jumanne, 21 Juni 2016

Askari Aliyetukanwa na Mke wa Waziri Bado Hajapandishwa Cheo

   Koplo Deogratius Mbango.

Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI

Dar es Salaam: Mapya yameibuka kumhusu askari wa usalama barabarani (trafiki), Koplo Deogratius Mbango wa Kituo cha Oysterbay ambaye wiki chache zilizopita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliagiza apandishwe cheo kutokana na kufurahishwa na utendaji kazi wake ambapo habari mpya ni kwamba, hadi juzi (Jumapili), bado hakuwa amepandishwa cheo kama rais alivyoagiza.

Trafiki huyo, alipata umaarufu mkubwa baada ya kumdhibiti dereva wa mke wa waziri mmoja (jina kapuni) aliyevunja sheria za usalama barabarani kwa kusimama kwenye alama za pundamilia (zebra) ambazo kimsingi hutumiwa na watembea kwa miguu wanaovuka barabara.

Akiwa anatekeleza majukumu yake, Aprili 24, mwaka huu, inadaiwa kuwa mke wa waziri aliyekuwa amebebwa ndani ya gari hilo, amlijia juu Koplo Deogratius huku akimtolea vitisho kwa kutumia cheo cha mumewe, lakini askari huyo hakutetereka zaidi ya kuendelea kusimamia sheria na kuwataarifu wakubwa wake wa kazi, akiwemo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni (RTO) Awadh Haji.

Katika uchunguzi wake wa chini kwa chini, Uwazi limebaini kuwa bado askari huyo anaendelea kukitumikia cheo chake cha zamani, jambo ambalo ni kinyume na maagizo aliyoyatoa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Ili kujiridhisha zaidi, Uwazi liliwahoji baadhi ya watu wa karibu wa askari huyo ambao kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini kwani siyo wasemaji, walisema Koplo Deogratius hajapandishwa cheo kama Rais Magufuli alivyoagiza kwani kama ingekuwa hivyo, angekuwa anaonekana.

Uwazi halikuishia hapo, lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga na kumuulizia sababu zilizokwamisha afande huyo kupandishwa cheo mpaka sasa ambapo alisema:

“Aaah ni kweli ndugu mwandishi hilo agizo lilitolewa na rais lakini hata mimi sijui kwa nini hajapandiswa cheo mpaka leo. Unajua suala la upandishwaji wa vyeo vya kipolisi hata hawa wa usalama barabarani walio chini yangu, huwa sihusiki bali  anayewapandisha ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. Muulize mwenyewe au mtafute msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimbo wao ndiyo watakaoweza kukupa majibu ya uhakika.”

Gazeti lilianza kumtafuta Advera kwa njia ya simu ambapo simu yake haikuwa hewani kila alipopigiwa. Baada ya kumkosa, Uwazi lilimtafuta, IGP Mangu kwa njia ya simu lakini naye simu yake haikuwa hewani kila alipopigiwa.

Ijumaa, 17 Juni 2016

Askofu Gwajima Anatafutwa na Polisi 'usiku na mchana'

Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima.

By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.

Kamanda wa Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewataka watu wenye taarifa za mahali aliko, Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, waisaidie polisi kwa kuwa bado wanaendelea kumtafuta.

Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.

Sauti kwenye mkanda huo inasema Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo Rais wa sasa, John Magufuli anayashughulikia.

Juzi, askari wa jeshi hilo, walishinda mbele ya geti la nyumba ya askofu huyo kwa saa saba bila kufunguliwa na kuondoka.

Kamanda Sirro  amesema kuwa “Kama amejificha, tukimbaini alipo tutamkamata na atambue bado tunamtafuta.”

Alhamisi, 16 Juni 2016

'Burger Movie Selfie remix' by Belle9 ft. Jux, Gnako, Blue, Izzobusiness, Mauasama

Remix ya wimbo wa Burger Movie Selfie msanii Belle9 tayari ishatoka ambapo ndani kawashirikisha Gnako, Izzobusiness, jux, Maua sama

Enjoy the song chini hapo

👇👇👇👇👇👇👇👇👇

👉DOWNLOAD HAPA👈 

ChidiBenz Kasaini lebo ya Wasafi??? (WCB)

Return of the King Kong. Baada ya kukosekana kwenye muziki kwa kipindi kirefu, msanii wa Hip Hop Bongo, Chidi Benz amerejea tena machoni mwa watu na muonekano mpya.

Hivi karibuni kuliibuka tetesi kuwa rapper huyo ametoroka kwenye kituo cha LIFE AND HOPE REHABILITATION kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani alipokuwa akipata matibabu ya kupambana kujitoa kwenye uraibu wa madawa ya kulevya alipopelekwa kwa msaada wa Babu Tale na Kala Pina, lakini hilo lilionekana halikuwa na nguvu kutokana na hivi karibuni hali yake imeonekana kuimarika na kurejea kama awali.

Safari ya ‘sober house’ Bagamoyo

Baada ya hali ya Chidi Benz kuonekana kuwa mbaya zaidi, March 21 mwaka huu Babu Tale na Kala Pina walichukuwa hatua ya kumpeleka kwenye kituo cha LHRC kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kupata tiba ya kujiondoa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya yaliyopelekea hali yake ya kiafya kuwa mbaya.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Babu Tale aliandika: “Mwana amekubaLi kukaa Soba ila anasisitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii safari ya matumaini.”

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Babu Tale alisema sababu yake iliyompelekea kumsaidia ChidI Benz kuwa alidhani msanii huyo kuwa ana ngoma [ukimwi].

“Kusema ukweli nilipoona picha ile nilipata wasiwasi nikidhani Chidi Benz labda ameungua na maradhi yetu ya sasa, sikuamini kama ni madawa ya kulevya ndiyo yamempelekea hali ile. Lakini sikuweza kuamini kesho yake ilibidi nimchukue Chid Benzi na kwenda nae kwenye kituo cha afya na kufanya check up ya mwili mzima, lakini baada ya vipimo kutoka akaonekana yuko poa kabisa ila wakagundua tu ni hayo madawa.”

Baada ya siku 27 akiwa ndani ya kituo hicho, alipotembelewa na Kala Pina, Chidi alisema, “Sina mengi ya kuongea, niko sawa, nipo okay, niko fresh na msaada naupata.”

Tetesi za kutoroka sober house

May 25 zilisambaa tetesi za kutoroka kwa Chidi Benz kwenye kituo hicho alichopelekwa kwaajili ya kupata matibabu ya kupambana kujitoa kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Kwa kipindi hicho watu waliompeleka huko walishindwa kuongea chochote zaidi ya kusema kuwa hakutoroka bali aliruhusiwa na uongozi wa kituo hicho kurudi nyumbani.

Tetesi za kujiunga na WCB


Chid Benz akiwa na Diamond kwenye studio ya WCB

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Chidi Benz amepost picha alizopiga kwenye studio ya WCB zinazomuonyesha akiwa na Diamond, Babu Tale na Harmonize hali inayozua shaka kuwa huenda King Kong akawa ameshamwaga wino wa kujiunga kwenye lebo hiyo ili kurudisha makali yake kama zamani.


Chid Benz akiwa na Meneja wa WCB, Babu Tale

Aidha inadaiwa kuwa tayari Chidi ameshapika ngoma ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni japo bado haijajulikana iwapo wimbo huo umefanyika chini ya menejimenti ya WCB au laah.


Chid Benz akiwa na Harmonize

Kila la kheri King Kong aka Chuma, nafasi yako kwenye muziki bado ipo.

Jumatano, 15 Juni 2016

Ufaransa Yatinga hatua ya 16 bora Euro

HABARI

POSTED 2 HOURS AGO

Ufaransa yatinga 16 bora ya Euro

By Mwandishi wetu, Mwananchi

IN SUMMARY

Katika mchezo huo wa awali wa kundi A uliofanyika katika Uwanja wa Stade Velodrome mjini Marseille, mabao ya wenyeji yalifungwa na Antoine Griezmann and Dimitri Payet.

Paris, Ufaransa. Timu ya soka ya Ufaransa imekuwa ya kwanza kutinga katika hatua ya mtoano wa michuano ya mataifa ya Ulaya (Euro 2016) itakayokuwa na timu 16, baada ya kuitungua Albania mabao 2-0.

 Katika mchezo huo wa awali wa kundi A uliofanyika katika Uwanja wa Stade Velodrome mjini Marseille, mabao ya wenyeji yalifungwa na Antoine Griezmann and Dimitri Payet.

 Kutokana na ushindi huo Ufaransa imefikisha pointi sita katika michezo miwili iliyocheza.

 Mchezo mwingine wa kundi hilo uliopigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes ulishuhudia Uswisi ikitoka sare ya 1-1 na Romania. Matokeo hayo yameifanya Romania ifikishe pointi sita wakati Uswisi ina moja mkononi.

 Kipute kingine kilikuwa kati ya Slovakia na Russia ambacho kilishuhudia Russia ikitoka ulimi nje kwa kubugia mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade Pierre-Mauroy mjini Lille.

Jumanne, 14 Juni 2016

Brazil Yamtimua kocha wake, Carlos Dunga


Brazil imemtimua kocha wao Carlos Dunga baada ya kikosi hicho kushindwa hata kuingia hatua ya mtoano ya michuano ya Copa America kufuatia nchi hiyo kutupwa nje na Peru..

Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, limetoa taarifa ya kumtimua Dunga ambaye pia alitarajiwa kuiongoza Nchi hiyo kwenye Michezo ya Olimpiki ambayo itachezwa nchini Brazil mwezi Agosti.

Pamoja na Dunga, pia Wasaidizi wake wote wa Benchi la Ufundi wameondolewa, na CBF imesema itateua Watu wengine kuingoza Timu hiyo.

Brazil ilifungwa 1-0 na Peru, Goli linaloelezwa kuwa la mkono, na kutupwa nje ikiwa ni mara yao ya pili tu katika Historia ya Miaka 100 ya Mashindano hayo kushindwa kuvuka hatua ya Makundi.

Dunga, ambae alikuwa nahodha wa Brazil Mwaka 1994 walipobeba Kombe la Dunia, aliteuliwa kuwa Kocha wa Brazil mara baada ya Nchi hiyo kutolewa kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zilizochezwa kwao Brazil.

Lakini tangu atwae wadhifa huo, ikiwa ni mara yake ya pili kuwa Kocha wa Brazil, Nchi hiyo haijafanya vyema na kutolewa Nusu Fainali ya Copa America ya 2015 kwa Penati na Paraguay ambayo ilifanyika nchini Chile