ImageMessi na mtanagazaji aliyempatia viatu vyake
Hatua ya mchezaji maarufu wa soka duniani Lionel Messi kutoa viatu vyake viuzwe kusaidia watu wasiojiweza imeibua mjadala mkali nchini Misri.
Messi alifanya hivyo akidhani labda kwamba alikuwa anafanya hisani bila kufahamu kwamba viatu huwa na maana nyingine nchini Misri na pia katika mataifa ya mengine ya Uarabuni.
Wakati wa mahojiano ya runingani ''katika kipindi cha Yes am Famous'' kinachopeperushwa hewani na runinga ya MBC Misri, mchezaji huyo wa Argentina aliwaambia watangazaji hao kwamba angependa kutoa viatu vyake vipigwe mnada.
Kitendo chake kilipokelewa tofauti kabisa na wiki chache zilizopita alipopongezwa na kusifiwa sana kwa kutimiza ndoto ya kijana mmoja wa Afghanistan alipomtumia mpira na fulana yake.
ImageAPImageMchezaji Lionel Messi katikati
Alipokuwa akivitoa viatu vyake Misri, hakujua kwamba viatu huchukuliwa kama matusi au kukosea watu heshima katika maeneo mengi ya Mashariki ya Kati.
Muda mfupi baadaye wakazi wa maeneo hayo walimkashutumu sana kupitia mitandao ya kijamii.
ImageMbunge aliyetoa viatu vyake ili kumpatia Messi
Na ili kujibu matusi hayo mbunge mmoja wa Misri said Hassin anayetangaza kipindi kwa jina 'Infirad' alitoa kiatu chake na kusema kwamba atampatia Messi.