Ijumaa, 25 Machi 2016

App ya FACEBOOK kuondoka Kwenye simu za Blackberry

ImageReutersImageMaafisa wa Blackberry wameshindwa kushawishi Facebook kubadili msimamo

Kampuni ya Facebook imetangaza kwamba app yake haitatumika tena kwenye simu za Blackberry.

Uamuzi huo umesikitisha sana kampuni hiyo ya kutengeneza simu Blackberry.

Wanaotumia simu hizo za Blackberry watalazimika kutumia visakuzi vya kawaida iwapo wanataka kutumia mtandao huo wa kijamii kwenye simu zao.

Bado haijabainika hatua hiyo itatekelezwa lini

Mapema mwezi huu, WhatsApp, ambayo humilikiwa na Facebook, ilitangaza pia kwamba simu aina ya Priv za kampuni ya Blackberry.

Simu zitakazotupwa na WhatsApp

Whatsapp itaacha kutumika katika mfumo wa simu za Blackberry kufikia mwisho wa mwaka 2016.

"Tulijaribu sana kushawishi WhatsApp na Facebook wabadilishe msimamo wao, lakini kwa sasa, uamuzi wao haujabadilika,” mtaalamu wa programu za simu wa Blackberry Lou Gazzola, aliandika kwenye blogu.

"Tumejibidiisha sana kutafuta njia ya kuwafaa wateja wetu na tunaendelea kutafuta suluhu mbadala.”

Bw Gazzola alitoa wito kwa wateja au watu wanaozipenda simu za Blackberry kutumia kitambulisha mada cha #ILoveBB10Apps (Nazipenda app za Blackberry 10) kulalamika

Maoni 1 :