Ijumaa, 4 Machi 2016

Sanches:Arsenal Tunatatizo La Kutojiamini

ImageGettyImageAlexi Sanchez

Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa Arsenal haina imani kwamba itashinda ligi ya Uingereza baada ya kushindwa mara mbili mfululizo na Manchester United na Swansea.

The Gunners walipoteza 3-2 katika uwanja wa Old Trafford na 2-1 nyumbani dhidi ya Swansea na hivyobasi kuwa pointi sita nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.

''Mara nyingine tunakosa motisha kwamba tayari tumeshinda 1-0 tunapoelekea uwanjani'',aliiambia Directiv Sport kabla ya mechi dhidi ya United.''Tunakosa ile ari kwamba tunaweza kuwa mabingwa''.

Sanchez aliongea:Iwapo tutaingia katika uwanja na ari ya kuwa mabingwa ,kushinda ligi ama hata kombe la vilabu bingwa Ulaya,tunaweza kuafikia hilo.

ImageAll SportImageRushford akifunga mojawapo ya mabao yake mawili dhidi ya Arsenal

''Ninakumbuka mechi dhidi ya Manchester United mwaka uliopita.Wachezaji walikuwa na motisha ya kushinda taji tulipoingia uwanjani.Tuliwashinda katika dakika 20 na kupata 3-0.Tulikuwa na ari na kujiamini siku hiyo''.

Arsenal imeshinda mara tatu pekee kutoka mechi 11 katika mashindano yote na wako katika nafasi ya tatu katika ligi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni