Jumapili, 20 Machi 2016

NIKE kuzindua Viatu Vinavyojifunga Kamba

ImageNike

Kampuni ya Nike imezindua viatu vinavyojifunga kamba zake vyenyewe.Inadaiwa kuwa viatu hivyo vitatolewa kwa uma kabla ya mwisho ya mwaka huu.

Viatu vinavyojifunga kamba zake vyenyewe vilionekana katika filamu ya Future II mwaka 1989,lakini ndoto ya utengenezaji wa viatu hivyo ikaanza kuafikiwa mwaka 2013 ambapo Nike ilianza kuvitengeza viatu hivyo.

Katika hatua kushangaza ,kampuni hiyo ya Marekani imesema kuwa viatu hivyo vitatumiwa na wateja wa programu zake.

Huku wengi wakiona viau hivyo kama njia ya kujitafutia umaarufu,programu hiyo itaisaidia kampuni hiyo kukuza bidhaa zake.

Programu za Nike+ kwa sasa zinaangazia ufuatiliaji wa data kuhusu vitendo vya watumizi wake na kuwapatia mafunzo.

ImageGettyImageNike

Lakini kuanzia mwezi Juni,mpango huo utazindua mapendekezo ya ununuzi wa kibinafsi pamoja na duka la mtandaoni.

''Nike imepoteza kiasi cha soko lake la vifaa vya michezo ikiwemo kampuni ya Under Armour,ilionunua programu ya MyFitnessPal na Asics ambayo ilichukua Runkeeper'',alisema McLaren,muhariri wa mtandao wa jarida linalooangazia teknolojia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni