Jumanne, 15 Machi 2016

Kortini kwa kusema Mugabe 'mzee'

ImageReutersImageRais Mugabe

Afisa mmoja wa polisi amefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baada ya kulaumiwa kwa kusema kuwa rais Robert Mugabe ambaye sasa ana umri wa miaka 92 ni mzee sana kuwa kiongozi.

Thomson Joseph Mloyi pia anadaiwa kumtusi mkewe rais Mugabe, Grace, kuwa kahaba kwa mujibu wa gazeti la kibinafsi nchini humo.

ImageAPImageThomson Joseph Mloyi pia anadaiwa kumtusi mkewe rais Mugabe, Grace, kuwa kahaba

Bwana Mloyi aliachiliwa kwa dhamana ya dola 100 na anatarajiwa kufikishwa mahakamani tena tarehe 15 mwezi huu.

Mugabe ndiye kiongozi wa umri mkubwa zaidi duniani baada ya kutimia umri wa miaka 92 mwezi uliopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni