3/4/16TRANSFER ZONESHARE
0
Getty Images
Real Madrid inataka kusafisha kikosi chake kwa kuwatema wachezaji nyota 10 ambao kiwango chao ni cha kusua-sua, Man Utd na Arsenal zakaa macho
Bosi wa sasa Zinedine Zidane na raid Florentino Perez wamechoshwa na wachezaji mizigo wanaocheza chini ya kiwango katika kikosi chao na wanataka kufanya mabadiliko makubwa kwa mujibu wa The Sun.
Klabu za Ligi ya Uingereza kama Manchester United, Arsenal, Chelsea na Manchester City zitakuwa zimepata fursa ya kujia ni wachezaji gani wataruhusiwa kuondoka Bernabeu.
Habari zinawataja Cristiano Ronaldo, Sergo Ramos, Isco, Jesse, James Rodriguez, Alvaro Arbeola, Toni Kroos, Danilo na Casemiro kama wachezaji watakaokumbwa na panga hilo.
Ronaldo amehusishwa sana na tetesi za kurejea kwenye klabu yake ya zamani na Ramos na Rodriguez wanafuatiliwa pia na vigogo wa Old Trafford.
Arsene Wenger kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na kazi ya Isco, na pia anaitamani huduma ya Jese.
Mshindi wa Kombe la Dunia wa Ujerumani Kroos huenda akazivutia klabu nyingi kama Chelsea na Liverpool zinazotaka kuimarisha safu zao majira ya joto.
Mpango huo wa Real Madrid si habari njema kwa Ligi Kuu ya Uingereza kwani watataka kuziba mapengo ya mastaa hao kwa baadhi ya wachezaji kutoka Uingereza.
Mlinda mlango wa United David De Gea, supastaa wa Chelsea Eden Hazard na Sergio Aguero wa Man City wanaweza kuingia kwenye rada za Real Madrid.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni