Jumatano, 23 Machi 2016

Japan Kufanya Kilimo Kwenye Mchanga Bandia

ImageREUTERSImageLicha ya kuwa vyombo vya dola vimepitisha ukuzaji wa vyakula katika eneo hilo la Fukushima ,wenyeji wengi wamesusia kula vyakula vilivyokuzwa huko wakihofia kuathirika na miale ya nyuklia.Wakulima katika mji wa Fukushima Japan eneo lililoathirika na kuyeyuka kwa tanuri ya nyuklia mwaka wa 2011 wamegundua njia mbadala ya kukuza mazao,,,,wakitumia mchanga bandia!

Katika Jaribio la kwanza katika wilaya ya Ojima mimea 2,000 aina ya 'ornamental anthurium' ilimea kwa njia nzuri na kuwaridhisha watafiti, jarida la Asahi Shimbun limeripoti.

Wilaya hiyo ya Ojima iliyoko takriban kilomita 50 kutoka kiwanda kilichoathirika vibaya zaidi cha nyuklia cha Fukushima Daiichi.

Kiwanda hicho kiliyeyuka baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukumba eneo hilo na kusababisha mafuriko.

ImageAFPImageKiwanda hicho kiliyeyuka baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukumba eneo hilo na kusababisha mafuriko.

Licha ya kuwa vyombo vya dola vimepitisha ukuzaji wa vyakula katika eneo hilo la Fukushima ,wenyeji wengi wamesusia kula vyakula vilivyokuzwa huko wakihofia kuathirika na miale ya nyuklia.

Wengi wao hawaamini vipimo vilivyotolewa na wizara ya afya kuwa ni salama kula vyakula hivyo kuwaacha wakulima wengi wakiwa hawana wateja wa vyakula vyao.

''kwa kutumia mchanga huu wa bandia,tunatarajia wakulima wa Fukushima huenda wakafufua biashara yao ambayo imeathirika sana na uvumi wa kuwepo kwa miale ya nyuklia yenye sumu.'' alisema Profesa Takahiro Hayashi kutoka chuo kikuu cha Kinki.

Chuo hicho ndicho kinachoendesha utafiti huo wa mchanga bandia.

ImageReutersImageWakulima katika mji wa Fukushima Japan eneo lililoathirika na kuyeyuka kwa tanuri ya nyuklia mwaka wa 2011 wamegundua njia mbadala ya kukuza mazao

Mkulima mmoja aliyeathirika zaidi 76 Yukichi Takahashi, amewasihi wapenzi wa maua kununua maua hayo ya kwanza yanayofanyiwa majaribio katika mchanga huo wa bandia.

''Nia yangu ni kushuhudia maua kutoka Fukushima ikituzwa washindi wa michezo mbalimbali katika mashindano ya Olimpiki ya 2020 inayoratibiwa kufanyika mjini Tokyo Japan.'' aliongezea Takahashi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni