Idadi ndogo wajitokeza uchaguzi wa marudio Z’bar
Uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar umefanyika kwa amani na utulivu huku kukiwa na idadi ndogo
Uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar umefanyika kwa amani na utulivu huku kukiwa na idadi ndogo ya wapiga kura.
Zanzibar Uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar umefanyika kwa amani na utulivu huku kukiwa na idadi ndogo ya wapiga kura, ikilinganishwa na idadi ya waliojitokeza katika uchaguzi uliofutwa wa Oktoba 25, mwaka jana.
Takwimu za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), zinaonyesha kuwa waliojiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura kwa Unguja na Pemba ni 503,860, na sehemu zote hizo zilikuwa na jumla ya vituo vya kupigia kura 1,580, na kila kituo kina wastani wa wapiga kura 350.
Katika uchaguzi huo vyama vya CCM, AFP, ADC na CCK vimeshiriki katika uchaguzi huo na kuweka mawakala wake vituoni huku chama cha CUF kikiwa hakina wakala yeyote kwenye vituo vyote vya kupiga kura vya kisiwani Unguja.
Pamoja na kuwepo kwa hali ya taharuki katika siku za karibuni visiwani hapa, hali hiyo imekuwa tofauti ambapo leo maeneo mengi yalionekana kuwa na amani, pia vikosi vya ulinzi havikujitokeza barabarani kama ilivyozoeleka.
Maduka mengi yalionekana kufungwa na katika vituo vya kupiga kura ambavyo inadaiwa ni ngome ya CUF, watu walijitokeza kwa idadi ndogo ikilinganishwa na wale waliojitokeza kwenye maeneo ambayo ni ngome ya CCM.
Katika Kituo cha Shule ya Sekondari Bububu pamoja na msimamizi wa kituo hicho Mohammed Zamani, kusema kuwa watu walijitokeza kwa wingi kupiga kura, wakala wa chama cha AFP, Fumo Machano Fumo alieleza kuwa tokea kufunguliwa kwa kituo hadi sita mchana watu waliokuwa wamepiga kura katika chumba chake walikuwa 25.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni