ImageEPAImageLionel Messi
Mshambuliaji wa kilabu ya Barcelona Lionel Messi alikosa mazoezi siku ya Jumatatu ili kupimwa figo yake.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikosa kucheza mechi ya nusu fainali ya kilabu bingwa duniani baada ya kupatikana na tatizo la figo,baada ya kuwa na maumivu ya tumbo yanayosababishwa na mawe ndani ya figo.
Hatahivyo alifanikiwa kushiriki katika fainali ya michuano hiyo siku tatu baadaye na ameichezea timu yake katika mechi zake zote za ligi.
Taarifa ya kilabu ya Barcelona imesema kuwa Messi mwenye umri wa miaka 28 atarudi katika hali yake ya kawaida siku ya jumatano.
''Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi atafanyiwa vipimo kadhaa Jumatatu na Jumanne ili kubaini hali ya tatizo hilo la figo alilopata mwezi Disemba'',ilisema.
Messi amefunga mabao 12 katika mechi 17 za ligi ya La Liga msimu huu na kuisaidia Barcelona kupanda pointi tatu juu ya jedwali la ligi hiyo.
Alicheza dakika 90 siku ya jumapili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya kilabu iliopo chini ya jedwali ya Levante.
Siku ya Jumatano ,Barcelona itaitembelea Valencia katika awamu ya pili ya nusu fainali ya Kombe la Copa del Rey ambapo wanaongoza kwa jumla ya mabao 7-0.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni