Huu hapa ni mkusanyiko wa picha zinazosimulia matukio muhimu katika maisha ya Muhammad Ali, bingwa wa ndondi na mwanamichezo mashuhuri.
OTHER
Muhammad Ali alizaliwa na kupewa jina Cassius Marcellus Clay mjini Louisville, kentucky mnamo 17 Januari 1942. Alianza kucheza ndondi akiwa na umri wa miaka 12 na baadaye akaishia kushinda dhahabu katika uzani wa light-heavyweight Michezo ya Olimpiki ya Roma mwaka 1960.
OTHER
Ali alianza kucheza ndondi ya kulipwa Oktoba 1960 akiwa na umri wa miaka 18 na akashinda mara 18 mfululizo kabla ya kusafiri kwenda London Juni 1963 kwa pambano lake la kwanza la kulipwa ng'ambo. Alibashiri kwamba angemshinda bingwa wa Uingereza henry Cooper kupitia knockout raundi ya tano.
OTHER
Cooper alimbwaga Ali raundi ya nne lakini Mmarekani Ali alitimiza ubashiri wake kwa kumshinda raundi ya tano mbele ya watazamani 55,000 uwanja wa Wembley.
OTHER
Ali alijaribu kupigania taji la ubingwa duniani februari 1964 alipokabiliana na bingwa wa dunia Sonny Liston. Liston alisema: "Nafikiri nitampiga vibaya sana kijana huyo."
OTHER
Alidunishwa na wataalamu wengi wa masumbwi kabla ya pambano hilo lakini Ali alicheza kwa ustadi mkubwa Miami na kumlazimisha Liston kusalimu amri kabla ya raundi ya sita. Ali alitawazwa bingwa wa dunia uzani wa heavyweight akiwa na umri wa miaka 22.
OTHER
Ushindi wa Ali dhidi ya Liston ulikuwa, na bado ni, moja ya matokeo ya kushangaza zaidi katika historia ya ndondi. Ali alijisifu: "Mimi ndiye bingwa zaidi! Mimi ndiye bora zaidi! Mimi ni mfalme wa dunia!".
OTHER
Ali, alitangaza kujiunga na kundi la Nation of Islam na akaacha kutumia majina yake ya awali na kuwa Muhammad Ali baada ya pambano hilo dhidi ya Liston. Alitetea ubingwa wake dhidi ya Liston mjini Lewiston, Maine mwezi mei 1965.
OTHER
Ali alishinda Liston baada ya kumpiga knock-out dakika ya kwanza ya raundi ya kwanza. Hadi wa leo, wengi wanaamini Liston aliuza pambano hilo, lakini Ali amesisitiza kwamba alishinda kwa njia safi.
OTHER
Novemba 1965, Ali alitetea taji lake dhidi ya bingwa wa zamani Floyd Patterson akishinda kwenye raundi ya 12. Patterson alikuwa amemshambulia sana Ali kuhusu msimamo wake kisiasa na kidini.
OTHER
Ali alirejea London kupigana na Henry Cooper kwa mara ya pili Mei 1966 katika uwanja wa zamani wa Arsenal wa Highbury. Mashabikji wake Uingereza, ambao hawakuwa wamemtambua mara ya kwanza, walimshabikia sana.
OTHER
Angelo Dundee, anayeonekana hapa akifunga mikono ya Ali kabla yake kupambana na Cooper, alikuwa akimsaidia Ali tangu alipoanza kucheza ndondi. "Kuna Cassius Clay mmoja," alisema Dundee. "Namshukuru Mungu."
OTHER
Ali alimshinda Cooper baada ya raundi sita na kumuumiza vibaya karibu na jicho lake la kushoto. Baada ya kifo cha Cooper 2011, Ali alisema: "Nitamkosa sana rafikin yangu wa zamani - alikuwa mpiganaji hodari na mwanamume muungwana."
OTHER
Ali alitetea taji lake mara ya nane dhidi ya Ernie Terell Februari 1967. Ali alimchezea Terrel ambaye alikuwa ametumia jina lake la kuzaliwa kumrejelea yeye kabla ya mechi, kwa raundi 15. Kila mara alikuwa akimwuliza: "Jina langu ni nani, Mjomba Tom?"
OTHER
Baada ya kutetea taji lake tena mara nyingine dhidi ya Zora Folley, Ali alipokonywa taji lake baada ya kukataa kujiunga na jeshi la Marekani lililokuwa likipigana vita Vietnam. Ilikuwa ni miaka mitatu baadaye aliporejea ulingoni tena.
OTHER
Ali alishindwa mara ya kwanza na bingwa mpya wa dunia Joe Frazier katika Madison Square Garden mwezi Machi 1971. Pambano hilo hujulikana tu kama "The Fight" yaani Pambano Lenyewe. Ilikuwa mara ya kwanza kwa mabingwa wawili wa dunia wa heavyweight ambao hawakuwa wameshindwa kukutana ulingoni.
OTHER
Ali alishinda marudio ya pambano hilo dhidi ya Frazier ingawa pambano lake linalosifika sana lilijiri baadaye 1974 alipopigana na George Foreman katika pambano linalojulikana kama "Rumble in the Jungle" maana yake "Mngurumo Msituni". Ali alikaa raundi nane za kwanza akiwa amejibanza kwenye kamba, mbinu aliyoiita 'rope-a-dope'.
OTHER
Lakini alichomoka raundi ya nane na kumwangusha Foreman kwa ngumi kali na kuwa mwanamume wa pili kutwaa tena ubingwa wa heavyweight, akiwa na umri wa miaka 32.
OTHER
Ali alimshinda Mwingereza Joe Bugner mjini Kuala Limpur, malysia Juni 1975. Miezi minne baadaye, Ali alipata ushindi mwingine dhidi ya hasimu wake mkuu Frazier katika pambano la 'Thrilla in Manila'. Ali baadaye alisema lilikuwa jambo la kukaribia kifo zaidi alilowahi kuhisi.
OTHER
Ali alipoteza taji lake kwa Leon Spinks 1978 kabla ya kulitwaa tena kwa mara ya tatu baadaye mwaka huo. Alitangaza kustaafu kwake miezi tisa baadaye. Lakini alirejea 1980 na kupigana na bingwa mpya Larry Holmes.
OTHER
Baada ya kushindwa an Holmes, Ali alipigana pambano moja, dhidi ya Trevor Berbick ambapo alishindwa kabla ya kustaafu kabisa akiwa na umri wa miaka 40. Kuondoka kwake kuliacha pengo katika tasnia ya ndondi, lililojazwa tu na kufika kwa Mike Tyson katikati mwa miaka ya 1980.
OTHER
Ali aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa Parkinson (ugonjwa wa kutetemeka) mwaka 1984 lakini alikabiliana na hali hiyo kwa ujasiri na staha. Mwaka 1996, alitazamwa na ambilioni ya watu akiwasha mwenye wa Olimpiki mjini Atlanta.
OTHER
Atlanta pia, alipewa tena nishani yake ya dhahabu kutoka kwa Michezo ya Olimpiki ya 1960. Ali alidai aliirusha nishani tyake ya kwanza Mto Ohio baada ya kukosa kuhudumiwa katika mgahawa wa Wazungu pekee, ingawa wengi hutilia shaka hilo.
OTHER
Wakati wa kufunga karne, Ali alijizolea sifa tele. Watazamaji wa BBC walimpigia kura kuwa Mchezaji Bora zaidi wa Karne, mwaka ambao bondia wa Uingereza Lennoz Lewis alishinda tuzo kuu.
OTHER
Bintiye Ali, laila alianza kucheza ndondi akwia na umri wa miaka 15 na akaanza kucheza ndondi ya kulipwa 1999 kabla ya kumshinda bintiye Frazier, jackie Frazier-Lyde mwaka 2001. Laila alishinda taji la super-middleweight mwaka 2002 kabla ya kustaafu 2007.
OTHER
Mwaka 2001, filamu kuhusu maisha ya Ali ilitolewa, Ali akiigizwa na Will Smith. Ali aliendelea kusifika kote duniani, licha ya afya yake kudorora.
OTHER
Baada ya kutimiza umri wa miaka 70, afya yake ilidhoofika zaidi. "Nafikiri kuugua kwangu ugonjwa wa Parkinson ni njia ya Mungu kunikumbusha ni nini cha muhimu zaidi," ndivyo alivyosema. Amefariki akiwa na umri wa miaka 74.