Jumapili, 10 Januari 2016

Gareth Bale kwenda Man United......

DILI: 

ADVERTISEMENT

MANCHESTER, ENGLAND

RYAN Giggs ametumwa kazi ya kumshawishi Gareth Bale ajiunge na Manchester United katika dirisha la usajili wa Januari hii.

Bale yupo tayari kung’oka Real Madrid baada ya kocha aliyekuwa akimkubali sana na kumwacha huru ndani ya uwanja, Rafael Benitez,  kutimuliwa kazi Jumatatu iliyopita, hivyo maisha yake yatakuwa kama ilivyokuwa chini ya Carlo Ancelotti.

Kocha mpya, Zinedine Zidane amemtuliza Bale akimweleza kwamba bado atapata nafasi kwenye kikosi chake baada ya kupewa mikoba wiki hii, lakini hilo haliwezi kumzuia staa huyo wa Wales kuachana na maisha ya Bernabeu.

Bale amefichua kwamba yupo tayari kurudi kwenye Ligi Kuu England huku Man United ikidaiwa kuwa na mipango thabiti na winga huyo.

Hata hivyo, Man United italazimika kulipa kiasi cha Pauni 150 milioni kuinasa sahihi ya winga huyo ambaye alisajiliwa Real Madrid kwa Pauni 85 milioni kutoka Tottenham Hotspur miaka mitatu iliyopita.

Bale amemwambia Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, kwamba alikuwa na uhusiano mzuri na Benitez, hivyo kuondolewa kwake kutakuwa na athari kubwa kwenye maisha yake ya soka.

ADVERTISEMENT

Man United ilitumia wiki kadhaa kwenye dirisha lililopita la usajili kumtaka mchezaji huyo, lakini Perez hakuwa tayari kumuuza staa huyo na alisema labda kwa ada ya Pauni 150 milioni, huku mshahara wa mchezaji huyo akitaka uanzie Pauni 300,000 kwa wiki.

Bale anataka kuondoka, lakini Perez anagoma kumuuza, huku miamba hiyo ya La Liga ikipiga hesabu za kumsajili winga, Eden Hazard.

Zidane alisema: “Naelewa, Bale atakuwa ameumizwa sana kwa kuondoka Benitez kwa sababu alikuwa kocha muhimu kwake. Lakini, chini yangu bado atakuwa muhimu kama alivyokuwa kwa Rafa.

“Ni mchezaji muhimu kwenye kikosi, muhimu kwa timu. Ni wa aina yake na amekuwa matata sana katika siku za karibuni. Nitampa sapoti, hivyo ataendelea kucheza vizuri tu.”

Bale amefunga mabao saba katika mechi saba zilizopita na anataka kuendelea kupewa nafasi muhimu kwenye kikosi kwa sababu inamfanya kuwa bora zaidi uwanjani.

Zidane alisisitiza kwamba atatumia washambuliaji watatu kwa pamoja, Bale, Cristiano Ronaldo na Karim Benzema. Akisema: “Ndiyo, nitawachezesha washambuliaji watatu. Ndiyo.  Huo ndiyo mpango.”

Benitez (55), amefutwa kazi Real Madrid baada ya kuinoa timu hiyo kwa miezi saba tu na akidumu na timu hiyo katika mechi 25.

RYAN Giggs ametumwa kazi ya kumshawishi Gareth Bale ajiunge na Manchester United katika dirisha

GARETH BALE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni