Jumatano, 27 Januari 2016

Bunge Kutorushwa Live Kwazua Kizazaa

Mwenyekiti wa kikao cha Bunge Andrew Chenge.

Mwenyekiti wa kikao cha Bunge Andrew Chenge ameahirisha kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea leo mjini Dodoma baada ya kutokea sintofahamu.

Chenge amefikia uamuzi huo kutokana na kuibuka kwa mjadala mkali kutoka kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kulitaka bunge liahirishe kikao cha kujadili hotuba ya Rais Dk. Magufuli ili wabunge wajadili hoja ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Hoja ya Waziri Nape Nnauye ilikuwa ni kwamba Television ya Taifa (TBC) haitarusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge (live) bali kutakuwa na kipindi maalumu kitakachoitwa leo katika Bunge litakachokuwa kikirekodiwa na kuonyeshwa usiku.

Hoja hiyo imezua mjadala mkali na kumfanya mwenyekiti wa Bunge kuahirisha kikao cha bunge kwa muda wa saa moja ili kikao cha kamati ya bunge kikakae na baadaye waje na njia muafaka ya kuweza kutatua jambo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni