Jumatatu, 11 Januari 2016

SIMBA YATOLEWA NJE MICHUANO YA MAPUNDUZI

   SIMBA YATOLEWA NJE MICHUANO YA MAPINDUZI

ZANZIBAR,
Timu ya Tanzania bara ambayo ni moja ya klabu maarufu na kongwe nchi ambayo makao makuu yake yapo mtaa wa Msimbazi,kariakoo hii sio nyingine bali ni SIMBA SC jana ilikua katika siku mbaya kabisa katika visiwa vya ZANZIBAR Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya mapinduzi kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wakata miwa kutoka MOROGORO,MTIBWA SUGAR
Mpaka muamuzi anapuliza kipenga chake SIMBA SC Walikua nyuma kwa goli moja hivyo basi kufanya washindi wawe MTIBWA SUGAR ambao wananolewa na mchezaji wa zamani wa Taifa Stars,MECK MEXIME
Hivyo basi timu ya MTIBWA SUGAR itacheza fainali siku ya tarehe 13 dhidi ya URA ya Uganda ambao waliwatoa watani wao wa jadi YANGA SC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni