Pengo atoka hospitali
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo aliyekuwa
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo
Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo aliyekuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili ameruhusiwa baada ya afya yake kuimarika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohammed Janabi alisema jana kuwa Kardinali Pengo aliruhusiwa saa 6.30.
“Amepata nafuu, ametoka na ametushukuru kwa huduma tulizokuwa tunampatia,” alisema Profesa Janabi.
“Kitengo kimemshughulikia na mimi ndiye daktari wake mkuu, afya yake sasa imeimarika na anaendelea vizuri, tatizo lake halikuwa kubwa sana, atalizungumzia mwenyewe baadaye,” alisema Profesa Janabi.
Awali, Profesa Janabi alisema Kardinali Pengo alilazwa katika kitengo hicho mwaka jana kabla ya kuruhusiwa siku 10 baadaye baada ya kupata nafuu na alipewa siku tisa kurudi hospitalini hapo kwa ajili ya kuendelea kufuatilia zaidi afya yake.
Kardinali Pengo alilazwa katika kitengo hicho Desemba 31 mwaka jana na kuruhusiwa siku 10 baadaye. Januari 18 alirudi hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya ufuatilizi kabla ya jana kuruhusiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni