Jumapili, 24 Januari 2016

Mkwasa Amlilia Cannavaro

Charles Boniface Mkwasa amesema hajapata taarifa rasmi na kuongeza kuwa, Cannavao bado yupo kwenye mipango yake ya timu ya taifa ya Tanzania

Wiki moja baada ya aliyekuwa nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutangaza kustaafu kuichezea timu ya hiyo kocha mkuu wa kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema hajapata taarifa rasmi na kuongeza kuwa, Cannavao bado yupo kwenye mipango yake ya timu ya taifa ya Tanzania.

Mkwasa ameiambia Goal, bado hajapata ujumbe wowote kutoka kwa beki huyo na kama itakuwa hivyo anashangazwa na maamuzi yake kwasababu hata wakati anachaguliwa kuwa nahodha sidhani kama aliandikiwa barua na kutangazwa kwenye vyombo vya habari kama ilivyo sasa.

“Mimi nafikiri si vizuri kuzungumza kwasababu nimekuwa nikizungumza muda mrefu na nikizungumza tutazidi kuchochea, mimi nafikiri maamuzi yatakuwa yamebaki kama nilivyozungumza”, amesema Mkwasa.

“Ninaheshimu maamuzi ya Cannavaro, ni mchezaji mzuri nime kaa naye, ni kiongozi mzuri anahamasisha vizuri na bado mimi namuhitaji. Lakini nilichokifanya ni mabadiliko ya kawaida tu kwenye timu kwakuwa yeye niliamini anaweza kuwaongoza watanzania kwenye mashindano ya CHAN na nilimpa taarifa mapema lakini sasa sitaki kulumbana nafikiri hivyo ndivyo itakuwa imebakia”.

“Nimshauri kwamba, bado anahitajika na nasikia kwenye vyombo vya habari kwamba amestaafu lakini bado mimi sitambui kustaafu kwake. Hata kama kustaafu lazima astaafu kwa heshima na lazima tufanye utaratibu na mimi nitasimamia utaratibu wake ili tuweze kuandaa atastaafu vipi”.

Cannavaro alitangaza kustaafu soka la kimataifa akipinga utaratibu uliotumika kumvua kitambaa cha unahodha na kumkabidhi Mbwana Samatta. Cannavaro alisema yeye kama nahodha hakupewa taarifa rasmi ya kubadilishiwa majumumu zaidi ya kupata raarifa hiyo kupitia vyombo vya habari, hivyo kwake ilikuwa ni kudharauliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni