Hali ilivyokuwa kwenye kikao hicho cha uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na naibu wake kilichofanyika katika Ofisi za Manispaa ya Kinondoni.
Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (katikati) akishiriki kikao hicho.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Tulia Ackson (katikati) akiwa amehudhuria mkutano huo wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni.Wajumbe wa kikao hicho wakishiriki kupiga kura za kumtafuta Naibu Meya.Zoezi la kupiga kura likiendelea.Zoezi la kuweka kura kwenye sanduku la kupigia kura likifanyika.Wajumbe walioshiriki kupiga kura wa upande wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakishangilia baada ya washindi kutangazwa.Kutoka kushoto ni Meya Mteule wa Kinondoni kupitia Chama Cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema), Boniphace Jacob, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumnjuri na mwenyekiti wa usimamizi wa huo, Celestine Onditi.Meya Mteule wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob akizungumza jambo mara baada ya kukabidhiwa cheti cha matokeo ya ushindi.Naibu Meya Mteule, Jumanne Amir akizungumza jambo.Wafuasi wa Ukawa walivyoonekana nje baada ya kutangazwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni.Wafuasi wa Ukawa wakiwa nje ya Ofisi za Manispaa ya Kinondoni wakishangilia ushindi wa meya wao.Ulinzi ukiimarishwa eneo hilo.
Hatimaye leo uchaguzi wa meya wa halmashauri wa Kinondoni jijini Dar es Salaam umefanyika ambapo diwani wa Ubungo kutoka UKAWA, Boniface Jacob (CHADEMA) amekuwa meya na na Naibu Meya ni diwani wa Tandale, Jumanne Amir Mbunju (CUF).
Akitangaza matokeo Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Celestine Onditi alimtangaza mshindi wa Umeya Manispaa ya Kinondoni kuwa ni Boniphace Jacob ambaye ni diwani wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema aliyepata kura 38 wakati mpinzani wake Benjamini Sitta wa CCM akipata kura 20.
Kwa upande wa kiti cha Naibu Meya, Bwana Celestine alimtangaza, Jumanne Amir ambaye ni diwani wa Tandare kwa tiketi ya CUF kuwa ndiye mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 38 wakati mpinzani wake wa CCM akipata kura 19 huku kura 1 ikiharibika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni