Fifa yaamuru Simba ilipwe chake
UNAZIKUMBUKA zile Dola 300,000 (Sh600 milioni) za mauzo ya Emmanuel Okwi kutoka Simba kwenda
ADVERTISEMENT
UNAZIKUMBUKA zile Dola 300,000 (Sh600 milioni) za mauzo ya Emmanuel Okwi kutoka Simba kwenda Etoile du Sahel na namna klabu hiyo ya Tunisia ilivyozungusha kuilipa Simba karibu miaka mitatu sasa?
Sasa ni hivi, klabu hiyo imeamriwa kuilipa Simba fedha hizo ndani ya sita 60 kuanzia Januari 7, 2016.
Agizo hilo limetolewa na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kupitia Kamati yake ya Nidhamu iliyokutana Desemba 15, mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya Fifa na nakala yake kutumwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Etoile na Simba, inasema maamuzi hayo yamefikiwa na kamati hiyo baada Watunisia kupuuza kuilipa Simba na kutaka ndani ya miezi miwili iwe imeshawalipa Wekundu wa Msimbazi mkwanja wao.
Katika barua hiyo ya maamuzi ya kikao hicho, Kamati ya Nidhamu imesema baada ya siku sitini (60) zilizotolewa kwa klabu ya Etoile kuwa imeilipa Simba SC kumalizika bila malipo hayo kufanyika, wataagiza Etoile du Sahel kukatwa pointi sita katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Tunisia.
Na kama klabu ya Etoile itashindwa kulipa deni hilo hata baada ya kukatwa pointi sita, Kamati ya Nidhamu ya FIFA itaamua kuishusha daraja klabu hiyo kutoka Ligi Kuu mpaka Ligi Daraja la Kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni