Jumapili, 24 Januari 2016

Tibohora Aachia Ngazi Yanga


Goal Tanzania

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha ametangaza kujiuzulu kuiongoza klabu hiyo kwa sababu mbalimbali na tayari amewasilisha barua kwa Mwenyekiti, Yussuf Manji

Tiboroha ameiambia Goal muda mfupi baada ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kuwa amechukua uamuzi huo  ili  apate muda zaidi wa kufanya shughuli zake za Uhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Nimeamua kuondoka ili kupata muda wa kutosha kufanya shuhuli zangu za uhadhiRi, unajua mimi nipo kitivo cha Elimu ya Viungo (PE), na sina ugomvi na mtu bali ni maamuzi yangu binfsi,”amesema.

Pamoja na Tiboroha kutozama ndani sana juu ya kujiuzulu kwake, lakini inaelezwa alikuwa hana maelewano na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu, Isaac Chanji ambaye kwa sasa ndiye mtu anayesikilizwa na kuaminiwa zaidi na Manji.

Tiboroha aliingia Yanga 2014 akichukua nafasi ya Benno Njovu aliyeondolewa katika nafasi hiyo kwa tuhuma mbalimbali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni