Jumatatu, 11 Januari 2016

MESSI AIBUKA KIDEDEA TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA DUNIA

ZURICH,USWISI

Mchezaji mahiri na mwenyekipaji cha hali ya juu kutoka nchini ARGENTINA almaarufu kama LIONEL MESSI ameibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo ya mchezaji bora wa dunia ballon d'Or ambapo kati mchuano huo alikua akiwania tuzo hiyo sambamba na wachezaji wenzie mahiri kabisa ambao wanacheza ligi moja ya la liga nchini HISPANIA wachezaji hao ni NEYMAR ambae wanakipiga pamoja katika club ya BARCELONA na mchezaji mwingine ni CHRISTIANO RONALDO ambae anakipiga katika club ya REALMADRID.
Kwa upande wa MESSI hii ni mara ya  tano kuchukua tuzo hii ambapo alichukua 2009,2010,2011,2012 na hii ya mwaka huu pia amechukua hivyo kufanya hesabu ya jumla ya tuzo tano pia kuweka historia ya aina yake katika mchezo wa soka.

          JE ALISTAHILI????
jibu moja ni NDIO bila shaka kutokana na kiwango ambacho alikionyesha tangu mwaka jana 2015 kwa kuisaidia sana club yake ya BARCELONA hivyo basi kufanya tuzo hii kuwa halali kwake kwasababu alipigiwa pia kura za kutosha kutoka nchi mbalimbali kupitia makepteni,makocha na waandishi kwenye pembe mbalimbali za dunia

MESSI ni mchezaji wa aina yake akiwa uwanjani hivyo kuwa kivutio kwa watu wengi wanaomtazama
Hivyo basi kufikia hatua hiyo MESSI Amebakisha kitu kimoja tu katika maisha yake ambacho ni KOMBE LA DUNIA tuliona mwaka 2014 kule nchini BRAZIL hakufanikiwa au tuseme haikua bahati yake hivyo basi juhudi zinahitajika ilikuisaidia nchi yake kupata ushindi huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni