Jumamosi, 16 Januari 2016

VITUO 27 VYA RADIO NA TV VIMEFUNGIWA NA TCRA

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy.

MAMLAKA ya Mawasiliano TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati.

Akitangaza uamuzi huo, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema vituo hivyo vimefungiwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Jumatatu ya January 18 mwaka huu na kwamba mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho saa 6 usiku (yaani Jumapili usiku kuamkia Jumatatu), na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili.

Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA mteja.

Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka wadau wote wa mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.

1. Sibuka FM
2. Breez FM
3. Country FM
4. Ebony FM
5. Hot FM
6. Impact FM
7. Iringa Manicipal TV
8. Kiss FM
9. Kitulo FM
10. Kifimbo FM
11. Mbeya City municipal TV
12. Radio 5
13. Radio Free Afrika
14. Musa Television Network
15. Pride FM Radio
16. Radio Huruma
17. Radio Uhuru
18. Star TV
19. Rock FM Radio
20. Standard FM Radio
21. Sumbawanga Municipal TV
22. Tanga City TV
23. Top radio FM limited
24. Ulanga FM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni