Mshambuliaji Mbwana Ally Samatta wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ameshinda Tuzo ya Mchezaji bora anayecheza soka barani Afrika na kuwamwaga Baghdad Boundjah (Algeria/: Etoile du Sahel) na Robert Kidiaba (DR Congo/ TP Mazembe) Usiku huu mjini Abuja, Nigeria.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (kushoto) akiwa mshambuliajinwa Gabon, Pierre-Emerick Emiliano François Aubameyang katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa mjini Abuja, Nigeria usiku huu wakati hafla ya Tuzo za Wachezaji Bora wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwaka 2015.
Kufuatia mchezaji huyu kuchukua tuzo hii kubwa africa lazima tutegemee mambo makubwa sana katika sekta hii ya michezo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni